Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,606
- 4,259
Kwa kuwa mimi si mtaalam wa uchumi nitaanza kwa kuomba radhi pale nitakapoandika mambo yatokayo kwa mtu wa kawaida (lay person). Ni kuhusu bei ya mafuta inayozidi kupaa kila siku. Sasa hivi bei mahali fulani inakaribia kufika shiling 2000 kwa lita moja.
Kipindi fulani hapo awali kulikuwa na hali kama hii na EWURA walikuja juu na kupanga bei elekezi za mafuta na bidhaa zinazotokana na mafuta hayo. na kuna vituo tulishuhudia vikifungwa kutokana na kukaidi agizo la kutumia bei hizo, pamoja na uchakachuaji ulioibuka ili kufidia mapungufu yatokanayo na bei kushushwa.
Hali iliendelea taratibu lakini kidogo kidogo bei ilianza kupanda si ghafla ila kwa viji-shilingi kidogo kidogo (labda ndiyo maana EWURA haikushtuka), mara 1,250/-...1,265/-...1,300/-...1,305/-...1,575/-...1,800/-...etc.
Swali langu ni hili, bei zimekuwa zikipanda sasa kwa muda na zimerudi kule kule ambako EWURA walikuwa wamekataa. Wafuatiliaji wa mambo, na EWURA napenda wanisaidie, wanijuze kama bei za sasa zinaendana na bei kwenye soko la kimataifa au ni yale yale ya mwanzo?
Nahitaji msaada maana naona hatuwasikii tena EWURA wakilizungumzia japo twaendelea kulipia gharama za uendeshaji wao katika kila huduma tunayopata yenye kuhusiana na nishati!!