EWURA: Nchi ina Mafuta ya Kutosha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1694085061766.png
Tamko hilo la EWURA linalofafanua kuhusu taarifa yao ya Septemba 4, 2023 linakuja muda mfupi tangu Waziri Mkuu akiri Bungeni kuwa kuna changamoto ya upatikanaji wa Nishati hiyo katika baadhi ya maeneo Nchini.

Kupitia taarifa yake kwa Umma, #EWURA imefafanua inaposema akiba ya Mafuta iliyopo inatosha kwa siku 19 maana yake inakidhi mahitaji ya Kisheria yanayotaka Maghala ya Hifadhi kuwa na Mafuta yanayotosha kwa siku 15.

Aidha, EWURA umeongeza kuwa inaposema mafuta yanatosha kwa Siku 19 haina maana baada ya siku hizo kutakuwa hakuna Mafuta Nchini.
 
Sisi bodaboda tunataka tuyakute kwenye vituo. Kama yapo ya kutosha halafu Handeni na Tabora Kuna uhaba tutawaelewa kweli? Mara Kuna mtu kafa kwasababu ya ukosefu wa petroli, Leo hii mchana kweupe MTU anasema mafuta yapo ya kutosha, inahitaji degree ya kiwango Cha PhD ili kunuelewa.
CEO wa EWURA ni mume wa Spika hakuna namna
 
Mbona hii kero ya foleni kwenye vituo umeanza Mara tu baada ya jamaa kuanza kazi? Halafu jamaa Ni msomi mzuri tu, mbona badala ya kutatua tatizo ndio kila mwezi linaongezeka?
Kusoma ni jambo moja na kutenda ni jambo jingine, nchi yetu inataka mtu mfuatiliaji wa kwenda field na siyo kuletewa report mezani, dikteta Magu aliweza hilo watu walikuwa wanaogopa kutoa taarifa za uongo, PhD mume wa Spika wa mchongo umewahi kumuona hata anazunguka kwenye hizo sheli?
 
Viongozi wa EWURA acheni kuwachonganisha wananchi na Serikali yao.
Simamieni sheria, fanyeni kazi kwa weledi na uzalendo.
 
Mume wa Betina afukuzwe,

Siri za kupanda Bei zinavuja vp Kwa wafanyabiashara Hadi kusababisha uhaba wa kutengeneza?
Hakuna sababu ya msingi ya kupanga bei ya mafuta kila mwezi.
Mbona bidhaa nyingine hazipangiwi?
Tatizo linaanzia hapa.
Hasara halisi inayosababishwa na huo ukokotoaji wa bei ni kubwa kuliko faida inayotajwa kinadharia.
 
Back
Top Bottom