Ewe mwanaume, usimchunge mwanamke!

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
10,416
15,971
Kuna sekeseke limetokea hapa limenihuzunisha sana, ipo hivi. Kuna jamaa yeye alikua anamchunga sana mke wake, haruhusiwi kutoka bila taarifa ikafikia akamnyang'anya simu kabisa kiasi kwamba mwanamke akawa haruhusiwi kumiliki hata kitochi tu.

Jamaa akajiona YES nimemaliza hamna tena mabaharia kumlia mke wake, bwana bwana kumbe ule msemo wa wahuni sio watu wazuri una maana kubwa sana. Ilitokea mwalimu wa madrasa akawa anamtaka mke wa jamaa. Unajua mbinu gani alikua anatumia!?

Eeeeh walaaaa umepatia kabisa, kuna mtoto wa jamaa alikua anasoma madrasa ambapo huyo mwalimu ndio anafundisha. Mtoto akitoka madrasa anarudi na ujumbe (barua) na wakati wa kwenda anaenda na feedback (barua) hivyo yaani, ustaadh akitaka mzigo anampa mtoto barua dogo anapeleka kwa mama ake (sijui alikua anajua ni matokeo ya pepa za madrasa au vipi) na mwanamke akipokea anatafuta udhuru anaenda kupigwa mkuyenge.

JAMANI WANAUME WENZANGU MWANAMKE HACHUNGWI.
 
Ushauri kwa vijana wenzangu hembu kwanza swala zima la wanawake tuweke pembeni tu pambane kujiweka sawa kiuchumi. Swala zima la kuoa sasahivi ni gumu wanawake kwa wanaume sasahivi hali ni tete swala la kuchepuka ni kama hamna dawa, ewe kijana hembu tumia nguvu zako sasahivi wakati bado una nguvu kujiwezea uwe na kwako au biashara yako. wanawake wapo tu na wataendelea kuwepo wazuri kila siku wana zaliwa ila kupata pisi ya kuoa mtihani. Hembu kuwa serious na maisha yako kwanza jipende kwanza kama mtoto wa kiume alafu utaona kama hawata kutafuta wenyewe.

NO MONEY NO HONEY.
KEEP HUSTLING NIGGER!
 
Umekosa vya kuchunga mpaka umchunge mwanamke.

Kachunge hata mbuzi huko.

Ukiona unatumia vinguvu fulani kumfanya mwanamke awe wako hasa kuchungana chungana, jua tayari umefeli mahala.

Anajichunga mwenyewe tu, kwa hofu ya mola wake na mapenzi mazito aliyonayo juu yako.
 
Unaambiwa ivi "USIKOSEE KUOWA" na vile vile kwa mwanamke kumpata mwanamme alietulia na mchamungu ni bahati sana, omba Mungu upate wa style iyo, na kwa mwanamme vile vile omba sana upate binti wa style iyo.
 
Huo mkasa ni kweli kabisa! Na huyu ndiye Ostaadh akiwa na mke wa jamaa.
20210222_151557.jpg
 
Back
Top Bottom