Ewe msichana, kwanini uzae kabla ya kuolewa?

Ewe msichana, kwanini uzae kabla ya kuolewa?

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,297
Habari wakuu,

Kumekuwa na wimbi kubwa la wasichana walioamua kuzaa wenyewe baada ya kukosa wa kuwaoa, wenyewe hujiita 'single mothers'.

Siku moja tukiwa katika kujumuika sehemu, msichana mmoja kati yao akauliza; nataka kuzaa maana umri umeenda na sijapata wa kunioa.

Msichana mwingine akasema mimi sitaki kuolewa, eti sababu nataka kuwa huru na mambo yangu.

Karibuni kwa michango yenu

Mbarikiwe...

Donatila
 
Kuoa au kuolewa sio lazima.
Kila mtu afuate hitaji la moyo wake.
Binafsi nawafahamu wanawake ambao hawataki kusikia swala la ndoa.
Wameamua kuzaa na hawataki mawasiliano na hao wanaume waliozaa nao.
 
Kupanga ni kuchagua, kila mtu anao uhuru wa kuamua lile litakalompa furaha ya moyo wake..

Akiona kuolewa ndiko kutakakokamilisha furaha yake na afanye hivyo..

Akiona useja ndio furaha kwake basi kila la kheri.

Walioamua kuwa 'single mothers' good for them,wangapi wameolewa lakini ndoa kwao zimekuwa 'mwiba'? badala ya kuwa' wake'wamefanywa 'punda'
 
Hapo ni maamuzi ya mtu na kila mtu ana Uhuru wa kufanya atakalo ili mradi tuu havunji sheria. Mie nilijua unazungumzia wale ambao wanabeba mimba bila kupanga halafu wanaume wanaingia mitini, kumbe ni hao ambao wanapenda wenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom