Ewe Kijana Mchakalikaji, katika Kutafuta, usifanye kosa la kujiwekea Deadline!

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,144
71,805
Et nikifikisha miaka 30 nitakua tayari na nyumba, Gari, Mke, Biashara kadhaa ,kazi nzuri n.k ?.... Hivi Kijana kama wewe uwazaye haya wee ni Mungu.

Toka juzi Kuna nyuzi naziona ona humu..

Mara... Ulijisikiaje ulipokutana na jama mlosoma ,yeye kafanikiwa.

Mara... unajisikiaje kufika miaka 30, hujafanikiwa .

Acheni kabisa kuwaza Ujinga wa namna hiyo , Mtajikuta mnajiingiza kwenye HARAMU na MISONGO YA MAWAZO NA KUJIUA.

Nawapa Mfano ...
Jiji la California Na New York yote yapo marekani ,ila huwezi amini yamepishana Masaa 3.

OBAMA Amekua Rais wa Marekan, akiwa na miaka 47.

Donald Trump Kawa Rais akiwa namiaka 70.

Mtu Mmoja mpaka anapata Degree ya kwanza ,kaipata akiwa namiaka 35 ila kazi kaja ipata anamiaka 36.

Mtu mwingine Kapata Degree anamiaka 23 ila mpaka anagonga 36 HANA AJIRA WALA KAZI YA KUELEWEKA.

Mtu Fulani, anafanikiwa akiwa na miaka 30, Ila anakuja KUFA akiwa na miaka 40.,, mwingine anafanikiwa akiwa na miaka 40 anaishi Miaka 90.

Hapa Duniani, Mungu alimpa Kila mtu na wakati wake, hamna aliyechelewa Wala kuwahi, wewe jua MUDA wako wa kuzaliwa Kufanikiwa Hadi kufa unatofautiana na muda wangu.

Maana yake ni nini? Msikae kujiwekea Deadline, msiishi kwenye kanuni au Muongozo ya watu wengine walojiwekea wao.

Pambana

Omba Mungu

Toa Zaka na Sadaka.
 
Una point ila hapo kwenye kutoa zaka ni kuendeleza umaskini, Mungu hana shida na ela ni kheri umsaidie jirani yako ambaye unajua hana uwezo hata wa kununua unga

kuliko kuzitupa kanisani, zinaishia kunenepesha wachungaji na kuijenga vatican city.
 
Maisha ni ufala.

Zamani nilikua nawaza nikiweza kumiliki kiwango fulani cha pesa then itakua ni kuenjoy tu na totoz mwanzo mwisho saiv muda wote nipo bize.. ohooo
 
Umeongea kitu kikubwa sana.

Tunapaswa kutafuta namna ya kupata furaha ambayo haitatufanya tujiangamize wenyewe.

Pesa, mali na vyeo, haviridhishi nafsi, ukiweka amani yako humo hutokaa ujihisi mkamilifu

Lakini ukiamua labda kazi yako ndo inakupa maana, au familia, au uhuru wako, utakuwa umepiga hatua sana....
 
Mm nilipanga mwaka huu nitakuwa na getto, ila ndo kwanza kazi niliyokuwa naitegemea imekuja kuzingua juzi kati hapa kwahy hapa kwa shangazi najiona bado nipo nipo sana 😔
Mungu akutie wepesi kwenye mambo yako vijana tuna pressure sana.
 
Sema haya maisha bwana yanakuchapa mpaka unawaonea wivu merehemu waliokufa wakiwa taasisi nono .
 
Back
Top Bottom