Kosa langu nini ni Vannesa?

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
891
1,379
Kosa langu nini ni Vannesa?


Mchana usiku bado nakuwaza Vannesa. Siku wiki miaka inapita bado nakuwaza Vannesa . Kosa langu nini Vannesa?

Kwa jina naitwa Assenga Mashauri . Ni kijana wa miaka 28 kwa sasa. Bila shaka wengi mshajua mimi ni mzaliwa wa wapi kutokana na jina nililo watajia ila kwa ambao hamjapata kujua nilizaliwa Wilaya ya Rombo mkoani kilimanjaro. Ni kijana wa pili kuzaliwa kutoka kwenye familia ya Mzee Assenga na mamasawe . Familia yetu niya maadili sana na imekolea itikadi kali ya kidini. Tokea nikiwa mdogo nimelelewa kumjua Mungu kusoma maandiko na kuhudhuria kwenye nyumba ya ibada mara nyingi sana. Mimi mwenyewe nilipenda maisha hayo . Nilipata kuijua sana Dini na kujua kufundisha vizuri sana.


Mwaka 2003 nilianza darasa la kwanza mpaka nafika darasa la tano nilikuwa nikishika nafasi ya 30 mpaka 40 na kwa darasa letu lililokuwa na wanafunzi 60 na . Ila kufikia Darasa la tano kuna mwalimu alihamia shuleni kwetu anaitwa Madam Ngowi . Huyu mwalimu sijui kwanini alitokea kunipenda sana na akawa karibu sana na mimi na kunisisitiza kusoma . Alinibadilisha nikaanza kupenda kusoma . Nilibadilika haraka sana mpaka walimu wa masomo mengine walinishangaa pale nilipotoka nafasi za 30 na mpaka kuwa mtu wa tano kwenye mitihani ya mwisho wa mwaka . Huyu mwalimu alinibadilisha sana mpaka namaliza darasa la saba haikuwa ajabu tena kuwa mtu wa pili au watatu . Namshukuru sana huyu mwalimu kwani mpaka nafika chuo naamini mwamko alionipa ndio ulionifikisha.

Mpaka nafika kidato cha sita niliendelea kuwa kijana mcha Mungu sana kwa imani na vitendo . Baadhi ya mapadre walijaribu kunishawishi nikawe padre lakini naamini huo wito sikuwa nao . Mpaka namalizia kidato cha sita sikuwa nimekutana kimwili na msichana au kutumia kiungo changu cha uzazi kwa matumizi mengine zaidi ya kutolea haja ndogo. Niliendelea kuishi kimaadili sana hata nilipopata smartphone nilijiingiza tu kwenye magroup ya kidini Facebook na watsap. Wakati huo niliandika makala mbalimbali zinazotoa ufafanuzi wa maeneo mengi linapolalamikiwa kanisa katoliki na makala hizo zilienda mbali sana . Nilikuwa nimeiva sana kwenye biblia na imani yangu.

Huo ulikuwa utangulizi tu wa stori nzima ya kweli kunihusu. kosa langu nini ni Vannesa. ?
Nilikukosea nini Vannesa ?

Sehemu ya pili ............
 
KOSA LANGU NINI NI VANNESA?

Ni miaka imepita sasa bado hunitoki akilini Vannesa kwanini lakini? Nilikosea wapi?

Mwendelezo . Sehemu ya 2

Sasa mtihani ulianza nilipoingia chuo mwaka wa kwanza 2016. Mwaka huo ndio nilitoka rasmi kuishi nje ya mkoa niliozaliwa na kusomea mpaka kidato cha sita .kwa Dar es salaam nilitua nyumbani kwa uncle Mbezi msakuzi . Nisiingie ndani sana kwani mbezi msakuzi napo pamebeba historia kubwa inayonihusu haswa kibiashara.

Nilianza chuo nikiwa bado mshamba mshamba . Baada ya kama miezi miwili kuna jengo kuwa naingia pale chuo . Kuna kigeti cha kuvuka ndio uingie kwenye hilo jengo sasa nilipokuwa naingia nikiwa nimezubaa si unajua tena kaushamba flani nikagongana na mrembo mmoja mkali sana . Simu yake ikadondoka nikafanya kumwambia samahani huku nikimwokotea nilipo kuwa nampa ile simu kukutanisha macho tu nilijikuta kama nimeganda hivi confidence ilishuka alipokea simu akiniambia usijali na kuanza kuondoka. Sasa baada ya kuachana pale nilijishangaa kubaki naiwaza ile sura ya yule mrembo kitu ambacho sikuwa nimezoea . Kwenye maisha yangu kabla ya hapo nilikuwa bize sana na dini sikuwahi kutumia muda kabisa kuwaza mapenzi lakini ni kama yule mrembo alianza kunitoa kwenye reli.

Baada ya kama wiki nilikutana nae tena alikuwa anaingia tena jengo nililokuwa nahitaji kuingia pia . Hilo jengo lazima uoneshe kitambulisho ndio uingie . Akawa anakitafuta kwenye pochi nilipofika akaniwahi kunisalimu mambo nikaitika poa nikaonesha kitambulisho na kuingia nae akawa ashakitoa akaonesha na kuingia .

Alipoingia moja kwa moja akaja kukaa karibu yangu na tukaanza kuongea na siku hiyo ndio tulitambulishana majina nikapata kumfahamu anaitwa Vannesa. Vannesa alikuwa mchangamfu na mwongeaji hivyo haikunipa wakati mgumu sana kumzoea japokuwa mimi ni mkimya sana alinichangamsha bila kupenda. Na mimi mpaka leo sipendi mwanamke mkimya japokuwa ni ngumu kupata mchangamfu mzuri na mstaarabu kama Vannesa. Asiyemchangamfu ndani kutakuwa kama ICU maana na mimi ni mkimya. Hata ukitoka nae mtabaki mnaambiana niambie Mwenzio naye anajibu niambie mtabaki hapo hapo mnaangaliana tu. Vannesa alijaza pengo nikamzoea mpaka nikaanza kuwa mwongeaji kuliko nilivyokuwa . Alinifanya niwe social sana. Alinipa confidence ambayo kuwa sina . Siku moja aliniuliza . Uzuri wa mwanamke ni tabia je unajua uzuri wa mwanaume nini ni?. Nikamjibu sijui . Akaniambia uzuri wa mwanaume ni kujiamini , haijalishi unakasoro gani una hela au huna una elimu au huna una cheo au huna kujiamini ndio uzuri wa mwanaume. Vannesa alinifanya nijione mwamba mpaka leo hii najichanganya popote naingia popote namfuata yeyote.

Tuendelee . Ndani ya huo huo mwezi tuliendelea kukutana na nilijagundua yeye ndio ananifuatilia na haikuwa bahati tu sisi kukutana kila mara. Kiukweli nilivutiwa na Vannesa sana . Alikuwa na asili ya kihindi mweupe mrefu . Shape hakunyimwa alipewa umbo la kuvutia mguu uliojaa vizuri kwa hakika Muumba alimpendezesha sana . Naweza kusema ilikuwa zali la mentali kwangu kupendwa na mwanamke mzuri kama Vannesa . Mpaka leo sijawahi kuwa na mwanamke mzuri mwenye makeke kama Vannesa ndio maana hasahauliki

:::::::: kosa langu ni nini Vannesa?

sehemu ya tatu ..... soon ....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom