Everything goes wrong (naelekea nisipotaka kuelekea)

Iamvitalis04

Member
Jul 20, 2019
38
48
Habari zenu wakubwa kwa wadogo! Nia na dhumuni la kuandika uzi huu nibaada ya kupitia changamoto zilizonifanya niwaze mengi juu ya aya maisha ninayopitia.


Kifupi mimi nikijana mdogo mwenye spirit ya mapambano kweli kweli


Safari ya mapambano yangu katika maisha ilianza mda mrefu kipindi bado hata sijamaliza shule nilikua mpambanaji kweli nakumbuka kipindi nipo form2 nilikua nauwezo wa kufanya wiring ya umeme bila kupitia chuo chochote kile, hata baada ya kumaliza kidato cha4 watu waliamini mimi nifundi umeme ila haikua kweli nikaachana na iyo kazi nikaingia sasa kwenye maswala ya media nilikua napenda kuona watu wanavyopiga picha ilinivutia nikaanza kujifunza taratibu, mungu si athumani nikapata kazi kwenye kampuni kubwa tu hapa nchini ya mambo ya production nilienda pale kujifunza mwsho nikawa nimeiva nikawa naweza kupiga picha na kuedit maisha yalienda safi sana tulifurah pamoja na wafanyakaz wenzangu tuliishi kama ndugu nilichokipata kilikua sio haba ila niliona naikaribia njia ya mafanikio.
Nilikua najituma kwenye kazi boss akaniamin nikawa dereva wa kampuni pia mpiga picha tulifanya kaz kwa kupokezana ila ubora wangu ulikua hapo kwamba nacheza miguu yote.


SIKU ILIYOBADIRISHA MAISHA YANGU
Nakumbuka tulitoka kwenye kazi usiku kama saa7 ivi na gari ilikua mbovu taa haziwak mpaka uwashe full wakat na pishana na mtu nikazpunguza ile kushtuka mbele nikalipanda tuta kwa nguvu gari ikawa sawa na sisi tulikua sawa baada ya hapo tukafka ofisni tulishusha kila kitu ila tukasema tukague kwanza vifaa viko salama kwasababu ni vingi tukasema tukague vile ambavyo vilikua kwenye hatar ya kuharibika zaid tukakita viko sawa vyote, kesho yake ilikua jpili mimi sikwenda kazin jamaa yangu aliekua rafiki yangu saana akanipigia simu kuniambia bwana nimefika hapa ofsni kuna kifaa kimeharibika kati ya vile ambavyo tulihisi vikosafe nikamwambia sawa nitakuja ofsni kumweleza boss, bahati mbaya alhamis ndio nikafka ofsni na moja kwa moja nikaenda kuonana na boss nikamulezea ilivyokua mpaka sikufika siku zote izo na imekuaje mpaka kifaa kuharibika akanilaumu sana nikamsihi sana ni bahati mbaya na siwez kutoka nyumbani nije ofsni kwa nia ya kuharibu kifaa cha kazi mimi ninapopatia ugali siwez kuharibu akasema hapana hatuwez kufanya kazi pamoja tena kwaiyo niende akinihitaji atanipigia simu.

Kweli nikaanza maisha mapya bila usimamizi wa mtu bila vifaa bila mtaji nikaingia kwenye mapambano mambo yalikua tofauti nilikua nakodisha kifaa cha elfu50 kwa kazi ya elfu70 mpaka60 mwisho na kazi zenyewe zikakoma nikipata basi lazima itokee sababu tu mpaka iyo kazi nisifanye ndio ya kawa maisha yangu napata kaz 8 nafanya 3 izo 5 hata sielewi kinatokea nini zinapotea tu. Maisha yakachange hali ikazid kua ngumu nimefkia hatua mpaka500 nakosa nikaona nijaribu hata uber sababu leseni ninayo napo nikatoka kapa gari ikipatikana kuna kua na sababu ya kukwamisha nisianze kazi kazi zangu za picha zikakoma kabisa simu za kazi haziiti tena nipo tu sina hata senti kula yangu ya kusaidiwa na majirani, marafiki siwaoni tena ndugu wameshanichoka


Kuna mmama akajaribu kunisaidia akanipeleka kwa mganga kwa gharama zake mwenyewe nikaambiwa rafiki zako uko ulipokua unafanya kazi ndio wamekutengeneza kwa mganga wa kitabu ili mambo yako yasiende chozi lilinidondoka nikasema kwa ubaya gani niliowafanyia nimeishi nao kama ndugu mbona, nikaanza sasa kupata picha pale ofisni aliekua best yangu saaaanaaa baada ya kuondoka pale sikuwah kuona call yake wala sms yake nikimtxt mimi hajibu nikaona sawa kilichonishangaza mara ya kwanza nakutana nae baada ya kupotezana mda mrefu nikafurah kumuona nikampa mkono wa salamu na tabasamu juu jamaa hakuongea chochote namimi wala hakunipa mkono iliniumiza sana ile kitu.
Kuna jamaa yangu tena akaniamba bwana jamaa yako kapita hapa kwangu juzi kakuongelea vbaya sana nikasema mi mbona sijawah kugombana nae, akaniambia nilipita na pale ofsni kwenu nikakuta wanakusema vbaya nikawaambia sio vizuri mbona jamaa nyie hawaongelei vbaya akaniambia kua makini na jamaa zako usiwaambie mambo yako


Sasa baada ya kutoka kwa yule mgananga simu za kazi zikaanza kuita kweli tena kwa fujo ila nikajitasmini vizuri mimi ni nani na nikweli ninapoenda ndio napataka hapo ndani nilikua na madawa kibao ya kutumia nikajifkilia mara mbilimbili imani yangu ya kikristo hairuhusu aya mambo nikakusanya zile dawa nikaenda kutupa.
Yule mama alienipeleka akiuliza vip dawa namwambia nimemaliza
Sasa maisha yangu yamekua ya fedheha kutoka kupigania ndoto zangu mpaka kupigania mlo mmoja wa siku, mbele naona kiza tu sioni wa kumshika mkono natamani hata niokoke sijui wapi pakuanzia makanisa ya uongo yamekua mengi
Kiza kinapotanda sitamani kukuche nikiwaza jinsi gani nitaimudu kesho yangu deal hata za elfu5 tu nw sizioni tena najiona ninavyopukutika na mawazo kila kitu kimebadirika kwenye maisha yangu hata mahusiano niliodumu nayo since2011 yamepukutika, nimepoteza kila kitu sasa nakula ili nisife tu


Yoyote anaeweza kunisaidia ndugu zangu anishike hata mkono uku nilipo ni kiza kinene sioni unafuu kila uchwao, nauhitaji wa kazi ndugu zangu maisha yangu yaendelee, sasa nimekua mtu wa kusaidiwa mpaka vocha ya500 natamani nile milo mitatu kama watu wengne ila inashindikana,natamani kutimiza ndoto zangu ningali kijana lakini sioni dalili nzuri mbele yangu, kuna muda nakata tamaa kabisa kikubwa nashkuru mungu tu kanipitishia mbali magonjwa gonjwa sijui kama ningekua hai leo.....pamoja na yote na mshkuru mungu kwa kila jambo
 
Usikate tamaa hayo yataisha ni mambo ya muda tu. Mwenyewe hapa nilitimliwa kazi 2013, msoto niloupitia ni noma Bora hata wewe unapakukaa. Ilifika tym nkawa Kama nmedata Hadi mwenyewe najistukia.washkaj wote walinikataa wakidai mimi ni mwizi. 2017 Hali ilikua mbaya zaidi, mambo yalibadilika yenyewe tu. leo hali ngumu naiskia kwa watu ni mwendo wa Bata tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Bro Unapiga picha za video au Mnato


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Pole Boss, ila jaribu usijifunge na mambo ya Passion yako, fanya mishe yoyote itayokupa pesa ukiwa huna kitu mfukoni.

Follow your passion ukishapata pesa.

Portfolio | 2020

Nimejaribu kaka ila vitu haviendi huwezi amini leo yenyewe asubuhi nimeenda kufatilia kazi sehemu muhusika kaniacha kwenye mataa hapokei simu zangu tena yani laiti angejua iyo nauli niliotumia kumfata kwangu ilikua ni zaidi ya nauli asingeniacha mataa
 
Yaani ulipokosea ni pale Ambapo uliamua kwenda kwa mganga yaani hawa jamaa ni waongo hawana jipya
Nikukuumbusha sio jambo la kurudia
Na kwa habari ya makanisa ni kweli kabisa makanisa ya uongo ni mengi ila yupo MUNGU wa kweli mwenye uwezo thabiti wa kubadilisha maisha yako

Yaani kama ulivyo pambana na kumtafuta mganga na solution ya maisha yako ndipo kwa formula Hiyo Hiyo mtafute MUNGU

Nina uhakika na hili juu ya maisha yangu MUNGU lazima akupiganie Hakika kama ukimtafuta kwa bidii kabisa
 
Pole changamoto ni sehemu ya maisha ila pia usiwe na mawazo Sana kwamba umelogwa itakua hivyo kweli pia uwe na tabia ya kuomba Mungu wew mwenyew sio mpaka uombewe au uende kwenye makanisa ukiomba Mungu kwa bidii na kwa Imani atakusikia funga siku 3 maombi ya ester, maombi ya ester ni maombi ya kibali omba Mungu akupe kibali kwa watu uku ukiwa na Imani lazima atakufanyia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Husda ipo, Mitume nayo ilifanyiwa Husda, Josef, Isa aka Yesu, Muhammad wote walifanyiwa Husda na vijicho,..

Huyo mama alijaribu kusaidia bila ya kujali dini yako, sasa wewe hizo dawa ulizopewa zikusadie umezitupa,..

Sasa unataka usaidiwe nini? Umechanganyikiwa, Udini umekushika.,hujitambui,.. maisha yako yatakuwa hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom