Everything goes wrong (naelekea nisipotaka kuelekea)

if cap fits

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
1,102
2,000
Yataisha wangu,siku zote wanaume tunapitia mengi,kikubwa tuliza mawazo mambo yatakaa vizuri tu,ulichelewa kuna sehem walitoa kazi ningekuunganisha ukapata hela ya kula ila ndo ivo deadline tayar,pole sisi wote tunapitia changamoto,uko mkoa gani lakin

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wanu

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
354
250
Husda ipo, Mitume nayo ilifanyiwa Husda, Josef, Isa aka Yesu, Muhammad wote walifanyiwa Husda na vijicho,..

Huyo mama alijaribu kusaidia bila ya kujali dini yako, sasa wewe hizo dawa ulizopewa zikusadie umezitupa,..

Sasa unataka usaidiwe nini? Umechanganyikiwa, Udini umekushika.,hujitambui,.. maisha yako yatakuwa hivyo hivyo.

Pia nimeliwaza hili mama aliamua kumsaidia kulingana na uwezo na maono yake na akakiri kuwa chakula hakikuwa shida tena then akaamua kutupa Dawa. Akawaza aanze kwenda kwa kina mwamposa then anataka msaada gan mwingine??


Sent using Jamii Forums mobile app
 

James Comey

JF-Expert Member
May 14, 2017
5,850
2,000
Habari zenu wakubwa kwa wadogo! Nia na dhumuni la kuandika uzi huu nibaada ya kupitia changamoto zilizonifanya niwaze mengi juu ya aya maisha ninayopitia.


Kifupi mimi nikijana mdogo mwenye spirit ya mapambano kweli kweli


Safari ya mapambano yangu katika maisha ilianza mda mrefu kipindi bado hata sijamaliza shule nilikua mpambanaji kweli nakumbuka kipindi nipo form2 nilikua nauwezo wa kufanya wiring ya umeme bila kupitia chuo chochote kile, hata baada ya kumaliza kidato cha4 watu waliamini mimi nifundi umeme ila haikua kweli nikaachana na iyo kazi nikaingia sasa kwenye maswala ya media nilikua napenda kuona watu wanavyopiga picha ilinivutia nikaanza kujifunza taratibu, mungu si athumani nikapata kazi kwenye kampuni kubwa tu hapa nchini ya mambo ya production nilienda pale kujifunza mwsho nikawa nimeiva nikawa naweza kupiga picha na kuedit maisha yalienda safi sana tulifurah pamoja na wafanyakaz wenzangu tuliishi kama ndugu nilichokipata kilikua sio haba ila niliona naikaribia njia ya mafanikio.
Nilikua najituma kwenye kazi boss akaniamin nikawa dereva wa kampuni pia mpiga picha tulifanya kaz kwa kupokezana ila ubora wangu ulikua hapo kwamba nacheza miguu yote.


SIKU ILIYOBADIRISHA MAISHA YANGU
Nakumbuka tulitoka kwenye kazi usiku kama saa7 ivi na gari ilikua mbovu taa haziwak mpaka uwashe full wakat na pishana na mtu nikazpunguza ile kushtuka mbele nikalipanda tuta kwa nguvu gari ikawa sawa na sisi tulikua sawa baada ya hapo tukafka ofisni tulishusha kila kitu ila tukasema tukague kwanza vifaa viko salama kwasababu ni vingi tukasema tukague vile ambavyo vilikua kwenye hatar ya kuharibika zaid tukakita viko sawa vyote, kesho yake ilikua jpili mimi sikwenda kazin jamaa yangu aliekua rafiki yangu saana akanipigia simu kuniambia bwana nimefika hapa ofsni kuna kifaa kimeharibika kati ya vile ambavyo tulihisi vikosafe nikamwambia sawa nitakuja ofsni kumweleza boss, bahati mbaya alhamis ndio nikafka ofsni na moja kwa moja nikaenda kuonana na boss nikamulezea ilivyokua mpaka sikufika siku zote izo na imekuaje mpaka kifaa kuharibika akanilaumu sana nikamsihi sana ni bahati mbaya na siwez kutoka nyumbani nije ofsni kwa nia ya kuharibu kifaa cha kazi mimi ninapopatia ugali siwez kuharibu akasema hapana hatuwez kufanya kazi pamoja tena kwaiyo niende akinihitaji atanipigia simu.

Kweli nikaanza maisha mapya bila usimamizi wa mtu bila vifaa bila mtaji nikaingia kwenye mapambano mambo yalikua tofauti nilikua nakodisha kifaa cha elfu50 kwa kazi ya elfu70 mpaka60 mwisho na kazi zenyewe zikakoma nikipata basi lazima itokee sababu tu mpaka iyo kazi nisifanye ndio ya kawa maisha yangu napata kaz 8 nafanya 3 izo 5 hata sielewi kinatokea nini zinapotea tu. Maisha yakachange hali ikazid kua ngumu nimefkia hatua mpaka500 nakosa nikaona nijaribu hata uber sababu leseni ninayo napo nikatoka kapa gari ikipatikana kuna kua na sababu ya kukwamisha nisianze kazi kazi zangu za picha zikakoma kabisa simu za kazi haziiti tena nipo tu sina hata senti kula yangu ya kusaidiwa na majirani, marafiki siwaoni tena ndugu wameshanichoka


Kuna mmama akajaribu kunisaidia akanipeleka kwa mganga kwa gharama zake mwenyewe nikaambiwa rafiki zako uko ulipokua unafanya kazi ndio wamekutengeneza kwa mganga wa kitabu ili mambo yako yasiende chozi lilinidondoka nikasema kwa ubaya gani niliowafanyia nimeishi nao kama ndugu mbona, nikaanza sasa kupata picha pale ofisni aliekua best yangu saaaanaaa baada ya kuondoka pale sikuwah kuona call yake wala sms yake nikimtxt mimi hajibu nikaona sawa kilichonishangaza mara ya kwanza nakutana nae baada ya kupotezana mda mrefu nikafurah kumuona nikampa mkono wa salamu na tabasamu juu jamaa hakuongea chochote namimi wala hakunipa mkono iliniumiza sana ile kitu.
Kuna jamaa yangu tena akaniamba bwana jamaa yako kapita hapa kwangu juzi kakuongelea vbaya sana nikasema mi mbona sijawah kugombana nae, akaniambia nilipita na pale ofsni kwenu nikakuta wanakusema vbaya nikawaambia sio vizuri mbona jamaa nyie hawaongelei vbaya akaniambia kua makini na jamaa zako usiwaambie mambo yako


Sasa baada ya kutoka kwa yule mgananga simu za kazi zikaanza kuita kweli tena kwa fujo ila nikajitasmini vizuri mimi ni nani na nikweli ninapoenda ndio napataka hapo ndani nilikua na madawa kibao ya kutumia nikajifkilia mara mbilimbili imani yangu ya kikristo hairuhusu aya mambo nikakusanya zile dawa nikaenda kutupa.
Yule mama alienipeleka akiuliza vip dawa namwambia nimemaliza
Sasa maisha yangu yamekua ya fedheha kutoka kupigania ndoto zangu mpaka kupigania mlo mmoja wa siku, mbele naona kiza tu sioni wa kumshika mkono natamani hata niokoke sijui wapi pakuanzia makanisa ya uongo yamekua mengi
Kiza kinapotanda sitamani kukuche nikiwaza jinsi gani nitaimudu kesho yangu deal hata za elfu5 tu nw sizioni tena najiona ninavyopukutika na mawazo kila kitu kimebadirika kwenye maisha yangu hata mahusiano niliodumu nayo since2011 yamepukutika, nimepoteza kila kitu sasa nakula ili nisife tu


Yoyote anaeweza kunisaidia ndugu zangu anishike hata mkono uku nilipo ni kiza kinene sioni unafuu kila uchwao, nauhitaji wa kazi ndugu zangu maisha yangu yaendelee, sasa nimekua mtu wa kusaidiwa mpaka vocha ya500 natamani nile milo mitatu kama watu wengne ila inashindikana,natamani kutimiza ndoto zangu ningali kijana lakini sioni dalili nzuri mbele yangu, kuna muda nakata tamaa kabisa kikubwa nashkuru mungu tu kanipitishia mbali magonjwa gonjwa sijui kama ningekua hai leo.....pamoja na yote na mshkuru mungu kwa kila jambo
Please endelea na mapambano na kamwe usifikirie kujidhuru au kumdhuru mtu yeyote

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
32,856
2,000
Wengi waliyokushauri wanapretend kama hakuna ushirikina au uchawi,nguvu za Giza hizo dalili na maelezo yako ni ushirikina umefanyiwa na wenzako uliyokuwa unafanya nao kazi,nyakati ngumu katika maisha zinatokea lakini hata binaadamu wanaweza kukufelisha kwa njia za kichawi.....Mimi binafsi nilipotoka hayo mambo ya kurogwa yapo ndiyo maana natofautiana na wachangiaji wengi humu.

Hiyo hali ya mambo kuharibika IPO sana hata hao wachungaji wanaenda kwa waganga kusafishwa nyota,kuoshwa kuondolewa nuksi na mikosi ambayo ukitupiwa utaangaika mpaka dunia inatanduka hakuna kitakachoongoka.....cha msingi Fanya ibada sana kisha tumia dawa kuondoa hivyo vitu vibaya mwilini kwako hata ulipoenda kwa mganga ungemaliza tiba ukaendelea na ibada maisha yako yote umtegemee mungu hata hizo dawa za mganga zinategemea nguvu ya mungu.

Unakuta muafrika kabisa eti haamini uchawi!!! Labda uwe hujarogwa ndiyo utakuwa unampa mtu ushauri kulingana na maisha yako....watu wanarogwa na kurogana asiye amini ushirikina kama upo huyo ni muongo....Mimi nimeshuhudia hivi vitu sana....kuna watu walikuwa wametupiwa misukule wametibiwa na waganga wamepona lakini hawajihusishi tena na waganga.


Umeandika atafute dawa pia amtumainie Mungu...
Which is which jamni ukiamini uchawi hata kupiga chafya utahisi kuna kitu...!
Nna rafiki angu alikua successful balaa..akaingiza mishe za waganga...ful kwenda kwa waganga...ss hv ukimtumia ten anakushuKuru balaa!
Kama unaamini mganga jikite huko..usimix na habari za Mungu..mayb itaweza kukusaidia ..usiww vuguvugu bora uwe moto au baridi!
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,544
2,000
Umeandika atafute dawa pia amtumainie Mungu...
Which is which jamni ukiamini uchawi hata kupiga chafya utahisi kuna kitu...!
Nna rafiki angu alikua successful balaa..akaingiza mishe za waganga...ful kwenda kwa waganga...ss hv ukimtumia ten anakushuKuru balaa!
Kama unaamini mganga jikite huko..usimix na habari za Mungu..mayb itaweza kukusaidia ..usiww vuguvugu bora uwe moto au baridi!
Kuna matatizo hayatibiki kwa maombi....mpaka utumie dawa...kwa mfano Nuksi,mikosi kuchafuliwa nyota....mnaambiwa mkanyage mafuta sijui mambo ya upako Yale yote ni madawa.
Ukitumia dawa ukaendelea na kumuabudu mungu kwangu sioni ubaya wowote labda uanze kumtegemea mganga kwa kila kitu.
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
32,856
2,000
Kuna matatizo hayatibiki kwa maombi....mpaka utumie dawa...kwa mfano Nuksi,mikosi kuchafuliwa nyota....mnaambiwa mkanyage mafuta sijui mambo ya upako Yale yote ni madawa.
Ukitumia dawa ukaendelea na kumuabudu mungu kwangu sioni ubaya wowote labda uanze kumtegemea mganga kwa kila kitu.


Kwahyo ww unaamini kwenye nuksi..?kutembelea nyota ya mwingine!!...kweli shetani katuweza
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,544
2,000
D
Kwahyo ww unaamini kwenye nuksi..?kutembelea nyota ya mwingine!!...kweli shetani katuweza
Kwa hiyo haumini kama uchawi upo?
Haumini kama unaweza kutegewa uchawi ukakudhuru.....hata katika dini zetu haya mambo yanafahamika sijui wewe imani yako ni ya aina gani...Ila endelea kuamini hivyo hivyo mkuu.
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
32,856
2,000
D

Kwa hiyo haumini kama uchawi upo?
Haumini kama unaweza kutegewa uchawi ukakudhuru.....hata katika dini zetu haya mambo yanafahamika sijui wewe imani yako ni ya aina gani...Ila endelea kuamini hivyo hivyo mkuu.


Mimi najua uchawi upo ila naamini hakuna mtu wa kunidhuru zaidi ya Mungu jamani....nikikupa mifano ya watu waloshiriki hizo nguv ss hv wako wap utachoka...!..mm sijawah ogopa uchawi au hata kuhofu kulogwa! Never!
Hivi hapa duniani kun mtu mwenye ngv zaidi ya Mungu? Kwamba atembelee sijui nyota sijui umepata nuksi?...kuna elimu zaidi kuhusu hayo masuala ya mikosi na nuksi .ukijikagua chanzo ni ww mwenyewe
 

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,239
2,000
Nahis kwangu imezid aisee kila ninachogusa kinaenda tofauti
Kwa kuwa wewe ni Mkristo, nenda kasome stori ya Yusufu yote kwenye kitabu cha Mwanzo, utajifunza juu ya mapito, uvumilivu na uaminifu wake kwa Mungu, utaona miaka mingapi alipita kwenye taabu, kama angekuwa mtu wa short cut asingefanikiwa. Pia usome habari za Daniel, utaona uaminifu wa Mungu kwa wanaomtumainia. Habari za hao niliokwambia utazisoma na kuzimaliza ndani ya siku moja tu.

Uwe mwaminifu kwa Mungu, muombe Mungu, atakuvusha.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,544
2,000
D
Kwahyo ww unaamini kwenye nuksi..?kutembelea nyota ya mwingine!!...kweli shetani katuweza
Kwa hiyo haumini kama uchawi upo?
Haumini kama unaweza kutegewa uchawi ukakudhuru.....hata katika dini zetu haya mambo yanafahamika sijui wewe imani yako ni ya aina gani...Ila endelea kuamini hivyo hivyo mkuu.
Mimi najua uchawi upo ila naamini hakuna mtu wa kunidhuru zaidi ya Mungu jamani....nikikupa mifano ya watu waloshiriki hizo nguv ss hv wako wap utachoka...!..mm sijawah ogopa uchawi au hata kuhofu kulogwa! Never!
Hivi hapa duniani kun mtu mwenye ngv zaidi ya Mungu? Kwamba atembelee sijui nyota sijui umepata nuksi?...kuna elimu zaidi kuhusu hayo masuala ya mikosi na nuksi .ukijikagua chanzo ni ww mwenyewe
Hakuna mwenye nguvu zaidi ya mungu Ila washirikina wanatumia uchawi kuwadhuru watu.
Kama unaamini uchawi upon basi sawa.
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
32,856
2,000
D

Kwa hiyo haumini kama uchawi upo?
Haumini kama unaweza kutegewa uchawi ukakudhuru.....hata katika dini zetu haya mambo yanafahamika sijui wewe imani yako ni ya aina gani...Ila endelea kuamini hivyo hivyo mkuu.

Hakuna mwenye nguvu zaidi ya mungu Ila washirikina wanatumia uchawi kuwadhuru watu.
Kama unaamini uchawi upon basi sawa.


Kila kitu ni imani tu mkuu!
 

gilldenu

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
2,785
2,000
Mkuu kwa lolote unalopitia sasa jua hakuna hali inayodumu milele, ivo basi Mwenyezi Mungu wa wote wenye mwili mwingi wa rehema mfadhiri wetu akumulikie nuru ya uso wake,akujibu siku umuitayo,usikate tamaa maana Mungu wetu anashughulika sana na mambo yetu.....omba kwa imani Mungu ni wetu sote. Tunakuweka kwenye maombi Mungu akukumbuke....

am better here
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom