Everything goes wrong (naelekea nisipotaka kuelekea)

Yaani ulipokosea ni pale Ambapo uliamua kwenda kwa mganga yaani hawa jamaa ni waongo hawana jipya
Nikukuumbusha sio jambo la kurudia
Na kwa habari ya makanisa ni kweli kabisa makanisa ya uongo ni mengi ila yupo MUNGU wa kweli mwenye uwezo thabiti wa kubadilisha maisha yako

Yaani kama ulivyo pambana na kumtafuta mganga na solution ya maisha yako ndipo kwa formula Hiyo Hiyo mtafute MUNGU

Nina uhakika na hili juu ya maisha yangu MUNGU lazima akupiganie Hakika kama ukimtafuta kwa bidii kabisa

Nitajitahidi mkuu kadri nitakavyoweza
 
Pole changamoto ni sehemu ya maisha ila pia usiwe na mawazo Sana kwamba umelogwa itakua hivyo kweli pia uwe na tabia ya kuomba Mungu wew mwenyew sio mpaka uombewe au uende kwenye makanisa ukiomba Mungu kwa bidii na kwa Imani atakusikia funga siku 3 maombi ya ester, maombi ya ester ni maombi ya kibali omba Mungu akupe kibali kwa watu uku ukiwa na Imani lazima atakufanyia

Sent using Jamii Forums mobile app

Nitajitahidi sana juu ya ilo
 
Husda ipo, Mitume nayo ilifanyiwa Husda, Josef, Isa aka Yesu, Muhammad wote walifanyiwa Husda na vijicho,..

Huyo mama alijaribu kusaidia bila ya kujali dini yako, sasa wewe hizo dawa ulizopewa zikusadie umezitupa,..

Sasa unataka usaidiwe nini? Umechanganyikiwa, Udini umekushika.,hujitambui,.. maisha yako yatakuwa hivyo hivyo.

Ahsante kwa unayotamani yaendelee kua juu yangu na mungu akakubariki
 
Ushauri wangu. Hama kabisa eneo unalojulikana sana. Hama hata mkoa. Nenda kajichanganye kwingineko kabisa. Hiyo huwa inasaidia kupunguza nguvu za wabaya wako. Na utakapoenda badili pia aina ya kazi ulizokuwa ukifanya mwanzo. Pia muombe Mwenyezi Mungu atatakufungulia njia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma stori yako ya maisha hakika machozi yamenitoka,yamenikumbusha kipindi ambacho nilikuwa sina wa kuomba msaada hata wa sh.200 nipate angalau kikombe Cha chai.

Haya maisha we yaache,kuna wengine tunapitia kipindi/nyakati ngumu sana Katika dunia hii.Lakini nyakati ngumu huwa hazidumu.
Nakushauri tafuta kitabu Cha Rorbet H Schuller~Tough times never last but tough people do"Hakika kitakupatia faraja na matumaini Katika kupambana.

Kwa upande wangu hiki kitabu kimenisaidia mengi lakini kikubwa kimenipa imani kuwa nyakati ngumu zinapita na watu imara wataendelea kuwepo.

Natamani mkuu niwe nauwezo wa kufanya yote ayo kuna mda nawaza hata nikazamie nchi za watu uko nijaribu maisha ila hali yangu kiukweli ni ngumu kula yangu tu ya mlo mmoja changamoto kubwa
 
Nimesoma stori yako ya maisha hakika machozi yamenitoka,yamenikumbusha kipindi ambacho nilikuwa sina wa kuomba msaada hata wa sh.200 nipate angalau kikombe Cha chai.

Haya maisha we yaache,kuna wengine tunapitia kipindi/nyakati ngumu sana Katika dunia hii.Lakini nyakati ngumu huwa hazidumu.
Nakushauri tafuta kitabu Cha Rorbet H Schuller~Tough times never last but tough people do"Hakika kitakupatia faraja na matumaini Katika kupambana.

Kwa upande wangu hiki kitabu kimenisaidia mengi lakini kikubwa kimenipa imani kuwa nyakati ngumu zinapita na watu imara wataendelea kuwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Shukrani mkuu nitajaribu kupitia pitia nitoke hata na chochote
 
Pole sana ndugu yangu, wanadamu tunapitia magumu sana, binafsi ningetamani kujua uko wapi kwa sasa na wewe ni mtu wa wapi yaani kijijini kwenu au chimbuko lako ni wapi...nikiyajua haya nitaweza hata kukushauri la kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sometimes u dnt have to treat life like ishu serious sanaaa utaumia.kuna muda inabid unafanya ku hustle kama unatania vile yote ili kujipa time ya gain strength.
Dats y hata gari ina minimum of 6 gears.sometimes u have to press life fast sometimes kidogo kidogo..hivyo yan..
 
Hayo mambo ni ya kawaidam. Huna tofauti na jamaa yangu ambaye ni fundi, yeye mambo hayaendi anadai kachafuliwa nyota..

Wakati kiuhalisia ni kwamba mambo tu mtaani yamechange, kakazana mimi zamani sikuwa hivyo.. Mi nikamuuliza unataka nani basi akose kazi. Juzi kaniletea habar za kwenda kusomewa kisomo nikampinga wazi wazi..

Mtoa mada amka jichanganye kivingne, changamoto za dunia wote tunapitia, wengine hatusemi tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi upo, acha kujifanya una dini sana wakati ukichunguza hizi dini zenyewe zina ushetani mwingi.

Hata hayo makanisa ya uponyaji utakayoenda yana mambo ya kiza lukuki.

Ulikosea sana kutofuata msaada alokupa huyo mama.

Mrudie huyo mama, muende tena kwa huyo mtaalamu ukaweke mambo sawa. Au tafuta kanisa ukakomae huko.

Unforgetable
 
Back
Top Bottom