Euro 2012: The Official EURO 2012 Thread

Euro 2012: The Official EURO 2012 Thread

Mchezaji wa Italy aliyepiga bonge la shuti likagonga mwamba anaitwa Daniele De Rossi anachezea timu ya As Roma ni kiungo mkabaji lakini timu ya taifa ya Italy anachezeshwa kama beki wa kati.
 
BJ upo? Ulipotea sana vipi equilyyyyyyyyyyyyps mmeshamwondoa ICU? Wacha-na na Spain mambo yote mwaka huu yapo kwa Wajerumani khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Oooi Oooi Wacha good kukusoma...mie nipo kiaina, naona wewe ulijichimbia wapi, Emirates nini?!! Eqlypz nae sijui nae niaje labda majukumu ya maisha! Mie kwa waliobaki nashabikia Germany na Spain.
 
Mkuu msimu uliisha then Chelsick wakahonga pesa na kununua CL basi kelele za kina Invisible na Mungiki Brothers sikuziona na yule mwingine Peas of ants naona EPL ikianza wataingia tena kwenye coma na kuadimika khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeee wako kama kambale vile huonekana mvua ikinyesha .... ..... ...

BTW nipo bongo nakula kuku kidogo but soon nitakuwa kwenye makazi yangu rasmi na nitawalisha sumu hawa Chelsick khe khe he khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeee naona Manure wamepooza sana na mchezaji wao maarufu Young Diver chijui na yule mwingine Wine Romney atafanya nini leo mbele ya Super Mario.


Jamaa waliongea saana walipochukua BL... Invisible aliweka picha every where... alionyesha mpak bedroom yake ilivyopambwa kwa bendera na rangi za Chelsea... Kwa sasa wapo na wanaonekana kwa matone saana...

Kula bata kwa style ndani ya bongo kaka... Sikufundishi namna ya kuishi ila nakukumbusha tu kuwa Bongo cheche... Usijiroge kutembelea Rim kicheche cha aina yeyote ile...

Hapa naoana Scott Parker anamhandle vizuri Pirlo... So katikati ni kama Italy wamepotea flani hivi....Ila kama ujuavyo Super mario huwa yupo tu... That gay is Lethal...He is a Baller...May be he will do something kabla Dinatale hajamreplace...
 
Hii "game" inaonekana inaweza kwenda muda wa nyongeza kuzingatia England wamefanya sana mazoezi ya kupigiana Penalty.

Italy wamejaribu kutumia njia ya John Terry badala ya Joleon Lescott kwa mipira ya juu iende kwa Baloteli lakini wameshindwa.

Ila England wanaweza kufunga kwanza.
 
Pouwa kamanda Richie.....Tupo tu tunaendeleza libeneke...

Naona Giroud anakaribia Imarati.....

Forward ya Arsenal imekamilika. Na kwa kuwa France wametolewa basi medical na paperwork kwa huyu Giroud vitakwenda haraka.


Baada ya hapo kuna uwezekano wa kumsajili M'Vila kwani hali ya Jack Wilshere bado haieleweki.


Anyway kwa hapa tunajidili mambo ya Euro 2012.
 
Nipo kwenye pub1 hv, kuna jamaa anasema huu mpambano ni kati ya catholic vs anglicana.
 
Italy wameanza kucheza mpira na wanamiliki sehemu ya kiungo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom