Euro 2012: The Official EURO 2012 Thread

Euro 2012: The Official EURO 2012 Thread

Wana JF mashindano ya uero yataanza saa ngap? Npo kijijin nataka nijue niende mjn n4wah ufunguz
 
nasikia first mechi ni saa kumi na mbili jion na ya pili ni saa tatu usiku east african time....over
 
280512_the-thao_Euro-Cup_dan-viet.jpg


euro-2012-groups.jpg

Leo 08/06/2012 ndio mashindano ya kombe la Ulaya mwaka 2012 yanaanza nchini Poland na Ukraine:
Historia fupi:
Mashindano haya yalianza mnamo 1960 kutokana na wazo la Rais wa chama cha soka cha Ufaransa wakati huo Bw. Henri Delaunay alilolitoa mnamo 1927. Mwanzoni mashindano yakijulikana kama UEFA European Nations Cup ambapo yalishirikisha mataifa manne tu. Jina la sasa ambalo niUEFA European Football Championship ilianza kutumika mwaka 1968.
Itakumbukwa kuwa bingwa wa kwanza alikua ni USSR na mashindano hayo yakifanyika nchini Ufaransa.
Tokea mashindano yaanzishwe ni nchi 9 tu ndio zimefanikiwa kulibeba kombe na mpaka sasa bingwa mtetezi ni Uhispania.
Ujerumani wamebeba kombe hili mara 3(Mara mbili wakijulikana kama Ujerumani Magharibi), Ufaransa na Uhispania wamefanikiwa kulibeba mara 3.
Ufuatao ni mtiririko wa mabingwa tokea kombe lilivyoanzishwa hata sasa.

[TABLE="class: outer_border, width: 500, align: left"]
[TR]
[TD]NCHI
[/TD]
[TD]MWAKA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1960[/TD]
[TD]USSR[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1964[/TD]
[TD]Uhispania[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1968[/TD]
[TD]Italia[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1972[/TD]
[TD]Ujerumani Magharibi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1976[/TD]
[TD]Czechoslovakia[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1980[/TD]
[TD]Ujerumani Magharibi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1984[/TD]
[TD]Ufaransa[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1988[/TD]
[TD]Uholanzi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1992[/TD]
[TD]Denmark[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1996[/TD]
[TD]Ujerumani[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2000[/TD]
[TD]Ufaransa[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2004[/TD]
[TD]Ugiriki[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2008[/TD]
[TD]Uhispania[/TD]
[/TR]
[/TABLE]





















Nani ataibuka bingwa wa Euro 2012?
Ikumbukwe mpaka sasa hakuna nchi ambayo imeshawahi kutetea ubingwa.

Tuungane sote wapenzi wa soka kufuatilia mtanange huu.

Mechi za Leo: Live Score

Uholanzi 0 (FT) 1 Denmark

Ujerumani 1 (FT) 0 Ureno
 
Mechi zitaonyeshwa saa ngapi? Na leo ni nani mechi za ufunguzi. Majukumu yamekuwa mengi hadi ratiba siijui.
 
mkuu hizo tv zinazorusha huku zinapatikana kwenye package ipi?
 
Mechi zinaanza rasmi saa moja na saa nne kasoro.
 
Mechi zitaonyeshwa saa ngapi? Na leo ni nani mechi za ufunguzi. Majukumu yamekuwa mengi hadi ratiba siijui.

kwa masaa ya bongo ni saa moja kamili na saa tatu na dakika 45 usiku. Mechi ya ufunguzi Poland v/s Greec
 
Jamani leo ndo kindumbwendumbwe kinaanza Unatupia wapi karata yako
 
Heshima yenu wadau wa michezo. Naomba msaada hapa Bongo ni channel gani zaidi ya DSTV watatoonyesha mechi za Euro 2012? Naomba msaada tafadhali
 
Heshima yenu wadau wa michezo. Naomba msaada hapa Bongo ni channel gani zaidi ya DSTV watatoonyesha mechi za Euro 2012? Naomba msaada tafadhali
Gerrard Nimesikia kwa wale wenye ving'amuzi vya StarTimes wataweza kuona kupitia chaneli ya UBC - Uganda Broadcasting Corporation.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: SG8
mkuu kama una king'amuzi cha startimes tune to UBC or kama una king'amuzi cha Easy TV tune to UBC pia.
 
mkuu kama una king'amuzi cha startimes tune to UBC or kama una king'amuzi cha Easy TV tune to UBC pia.
Nashukuru Mkuu, ngoja nilipie king'amuzi changu ila kwa sasa naangalia kupitia ATN wanaonyesha live opening Ceremony
 
dah hata mie sijui. vipi zile za warabu AD sports hawaonyeshi kwani?
 
Mozambique one na two zinaonyesha mpira km unatumia dish.
 
JF leo hakuna live text commentary?

Wapi sobhuza?
 
TBC ndio kwishney kabisa jamani tangu TM aondoke basi nA TBC inajifia kabisa??huyu Mshana anafanya nini au anafuatisha bora liende bila ubunifu??kazi sana kosa kuweka Usalama kila sekta!wanaharibu sana maana sio competent wa kutosha!angalia NECTA,TBS.....
 
Mimi naangalia kupitia Agape Televison Network kwa kichadema tu
 
Dakika ya 9 Poland 0 Greece 0 game ni balanced japo Poland wanacheza vizuri zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom