EU kwa sasa itakabiliwa zaidi na mfumuko wa bei za bidhaa hasa kutokana na kuongezeka kwa gharama za nishati. Kumbuka kuwa tunazungumzia athari za vikwazo, na si athari za vita.
Urusi itaathirika zaidi katika sekta karibu zote muhimu za kiuchumi ambazo zimelegwa moja kwa moja na vikwazo.
1. Sekta ya viwanda. Upatikanaji wa malighafi utaathiriwa kwa kiasi kikubwa. Maintenance bila kusahau upatikanaji wa spare parts za miundombinu mbalimbali ambapo miongoni mwa suppliers wakubwa ni nchi zilizoiwekea vikwazo.
2. Sekta ya afya. Baadhi ya kampuni zimesitisha shughuli zake nchini Urusi kutokana na vikwazo. Suppliers wa vifaa muhimu vya kitabibu kama Siemens wamesitisha mikataba yao.
3. Usafirishaji. Athari kubwa hasa ni katika uendeshaji wa mashirika ya usafirishaji kama ndege n.k. Fahamu kwamba, Airbus na Boeing ndio suppliers wao wakubwa.
4. Fedha. Vikwazo kupitia mifumo ya kifedha ya kimataifa kama SWIFT kunapelekea ugumu kwa mataifa mbalimbali duniani kufanya biashara (international trade) na Urusi.
5. Sekta zingine kama utalii, itaathirika kwa sasa hasa kutokana na mazingira yaliyopo. Upotevu wa ajira kutokana na kampuni na mashirika mbalimbali ya uwekezaji kusitisha shughuli zake nchini Urusi.
6. Mfumuko wa bei unaendelea hivi sasa sababu ya athari katika upatikanaji wa bidhaa kutokana na imports na uzalishaji kuathiriwa na vikwazo vinavyoendelea kutangazwa.
Na kadhalika!
Swali kuhusu dollar umelijibu bila facts. Umetumia zaidi hisia!
Mikataba mikubwa ya nishati ambayo ni kati ya Urusi na Ulaya ina utaratibu wa malipo kwa sarafu ya euro. Dollar inahusikaje? Na inadhurikaje endapo Urusi itakataa kulipwa kwa euro?
Mataifa yaliyo mengi duniani yanaweka akiba ya USD kama reserve currency kutokana na stability ya dollar kama factor mojawapo ukilinganisha na sarafu zingine, ndio maana inatumika zaidi katika biashara za kimataifa ama kama reserve currency ya nchi nyingi duniani, ikifuatiwa na euro.
Hakuna mfanyabiashara (internationally) anayetamani sana kufanya biashara kwa kutumia sarafu ambayo ni volatile yenye kubadilika thamani ghafla na ovyo!
Mpaka sasa hakuna sarafu yenye vigezo vya kuwa mbadala wa dollar kama major reserve currency duniani. Sarafu ya namna hiyo inahitaji sana kuwa economically stable. Pia inahitaji kuwa na kiwango kidogo cha inflation. Kwa kiswahili naweza kusema, mfumuko. Kutokuwa na sifa hizi kunaifanya hiyo ruble "isitoboe".
Hizo ni sifa chache rahisi. Vigezo muhimu ni nguvu ya kiuchumi na kisera ya nchi ambayo fedha yake ni reserve currency ya dunia. Mifumo ya kifedha na kibenki ya nchi husika inapaswa kuaminika (trusted) kimataifa.
Uaminifu (trust) unajengwa kupitia taasisi imara ndani ya nchi husika katika msingi wa utawala wa sheria. Nguvu ya uchumi wa Russia, taasisi na sera zake za ndani katika masuala ya kifedha hazitoshi kuiwezesha ruble kuwa major reserve currency ya dunia.