joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 19,413
- 41,556
Umetumia kipimo gani?Vinaumiza wote, Urusi zaidi.
Umetumia kipimo gani?Vinaumiza wote, Urusi zaidi.
Yaah kawaida hata wao wameathirika sana ila kila mtu anatafuta solutions ya hali aliyokuwa nayo.Ungekuwa na ufahamu hata kidogo jinsi ya embargoes zinavyoathiri uchumi wa nchi targeted usingeongea hiko ulichokisema. Putin mwenyewe amekiri wazi kuwa vikwazo vilivyowekwa vimeiathiri Urusi.
Hakika malofa Ni wengi.Yaani Google wasepe, Coca-Cola wasepe, Pepsi, Nike, Amazon, no visa card, master card, no kuuza mafuta no kuuza makaa ya mawe afu useme Urusi haitayumba,
Vikwazo kweli kuna watu watakuwa hawana shughuli, ila gharama za nishati ipo juu kuna viwanda vinajiendesha kupitia gesi ya Russia na kama unavyojua gharama zikiongezeka za uzalishaji lazima wapunguze watu.Sasa kama wafanyakazi kwa maelfu wako jobless na familia zao hicho chakula watanunuaje?? Serikali itawapa free meals na pesa za matumizi mengine?
Dementia ya babu biden inaendeleaje?Wanatakiwa kumfanyia assassination
Wanatakiwa kumfanyia assassination
Nimeiona hiyo link. Umejaribu kupiga hesabu impact ya hizo nchi kwenye soko la kimataifa na uchumi wa dunia kwa ujumla?Nikuwekea link ya habari ya Aljazeera nchi zilizo iwekea vikwazo Russia au unapingana nayo?
Umetumia neno zuri UCHUMI WA DUNIA, now jiulize sababu kwanini sasa hivi UCHUMI WA dunia umetikiswa na nchi gani iliyo UTIKISA UCHUMI wa dunia manake si nchi za daraja la mwisho wala la kwanza kote duniani kilio kimoja.
Kwa hiyo hizo nchi nyingine ambazo wanategemea gesi ya Russia zaidi ya 40% uchumi wao hautotikisika?
Kama gap haliwezi zibwa overnight, vipi kwa wananchi wa ulaya manake wanatakiwa kuvumilia, je moyo wa kuvumilia wanao wakati gharama za maisha zimepanda maradufu. Ujue unapo iponda Russia rudi kwenye uhalisia wa hali ya sasa kwa ulaya na wananchi wake.
Kaka huku tunapoelekea hivi vikwazo watu wataviona vya kawaida na ndio maana China, America Kusini, Africa na baadhi ya nchi za Russia wapo tayari kufanya biashara na Russia, tena kwa hela zao na SI DOLA na hiki kitu cha kufanya biashara bila kugumia Dola US hakitaki na ndicho kina muumiza sana,hasa Russia kuuza bidhaa kwa hela yake ya Ruble.
Brother Ruble ukitoboa nchi nyingine rasilimali zao watauza kwa hela zao kitu ambacho US hataki kusikia na ndio maana wengi wamechagua kuto egemea upande wowote.
Udikteta wakati wananchi wao wamekubaliana na serikali yao. Ndio yale mmemwita Sadam dikteta, mkamsingizia ana silaha za kikemikali, mkampiga mkaua mamilioni ya watu.Raia wa EU wameafiki vikwazo. Wamekubali maumivu ya kiuchumi ni moja ya gharama ya kupiga vita kushamiri udikteta. Let freedom ring.
Ikifika 5,000 hata team bodaboda watasanda.Naiona lita ya petroli ikielekea kufikia Tshs.5000 na team IST wakizidi kujimwambafy...
Russia chapa kazi.Udikteta wakati wananchi wao wamekubaliana na serikali yao. Ndio yale mmemwita Sadam dikteta, mkamsingizia ana silaha za kikemikali, mkampiga mkaua mamilioni ya watu.
Matokeo mwaka juzi Tony Blair anaomba msamaha eti ilikuwa false intelligence, huku wakiwa wameua raia kibao wasio na hatia ,Bush,Blair, Sarkozy wanadunda mtaani.Us imeguswa kidogo na ICC wakawawekea vikwazo ICC.Wameiharibu Iraq matokeo yake nchi hautawaliki sasa si bora dikteta Sadam.
Njoo Libya nayo hooo dikteta Ghadafi anawaumiza watu, wamevamia wamepiga Libya nchi haitawaliki, imekuwa kama bwawa la kambale makundi zaidiya kumi kila kundi ina zone yake, bado kuna utitiri wa ISIS na kambi zao za mafunzo. Obama nae baadae anakuja kujilaumu kwamba ktk mistakes kubwa aliyo ifanya ni kumwondoa Ghadafi.
Waacheni watu waamue mambo yao na si kuwapangia, matokeo yake US na EU wameua mamilioni ya watu bila sababu ya msingi na wandunda mtaani.
Russia chapa kazi.View attachment 2177734
EU wataumia kwa Kwa kiasi Fulani kwa kipimo kipi ulichotumia?Nimeiona hiyo link. Umejaribu kupiga hesabu impact ya hizo nchi kwenye soko la kimataifa na uchumi wa dunia kwa ujumla?
Uchumi wa dunia umetikiswa kwa sababu ya mgogoro uliopo ama vita kati ya Russia na Ukraine, si kwa sababu ya nchi moja specifically.
Hata uzalishaji wa chakula na bidhaa zingine muhimu nchini Ukraine ambayo ni miongoni mwa nchi zenye uzalishaji mkubwa duniani, umeathirika. Mgogoro specifically ndiyo ulioleta mtikisiko wa kiuchumi duniani.
Nimekwisha sema sana, athari zitakuwepo kwa nchi za Ulaya kwa kiasi fulani, ila Russia itaathirika zaidi long-term kutokana na vikwazo ambavyo vitapelekea athari katika sekta mbalimbali za ndani hasa za uzalishaji.
Nina swali kuhusiana na hoja zako za mwisho: unafikiri ni kwa nini dollar inatumika zaidi katika biashara kimataifa?
Kuna vipimo vipi?Umetumia kipimo gani?
Sijui niliye muliza aliye sema "kiasi fulani ",vipi unataka kumsaidia?Kuna vipimo vipi?
Naam watulie kimyaa wkt Russia ikitembeza Kichapo heavy Kama walivyotulia wkt US/NATO/ISRAEL ikitembeza Kichapo1 mpaka 3 walikaa kimyaa na kuchekelea wanavyofanyiwa unyama.
Cha Joto,Ukimwi na malaria.Kuna vipimo vipi?
Unadhani Putin Ni Mbowe? Kwamba anaweza akafanywa chochote,Muda wowote ule?Putin yuko hatarini sana. Muda utasema.
Pole Sana mkuu , njoo ununue ndo utajua 😂😂😂Vikwazo vitaiumiza EU kwa kiasi fulani ila vitaiumiza Russia zaidi long-term. Kusema kuwa vikwazo havitoiumiza kabisa Russia si kweli.
Russia inahitaji kuuza nje hasa nishati ambapo mteja wake mkuu ni EU. Inahitaji mapato kutokana na mauzo hayo kwaajili ya kuendesha nchi kiuchumi. Hata hiyo issue ya "kununua gesi kwa hela yake" ambayo ilizua mjadala mwanzoni, haipo tena kwa sasa sababu itakwamisha mapato. Utaratibu wa sarafu ni uleule wa awali wa euro.