Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,482
- 9,242
Halmashauri Kuu ya Ulaya imependekeza leo vikwazo vipya dhidi ya Urusi, ikiwemo marufuku ya ununuzi wa makaa ya mawe.
Katika vikwazo vinavyopendekezwa, ambavyo mataifa ya Umoja wa Ulaya lazima yaidhinishe, vitazuia uagizaji wa bidhaa za Urusi zenye thamani ya euro bilioni 9 na uuzaji nchini Urusi wa bidhaa za thamani ya euro bilioni 10, zikiwemo kompyuta na kuzizuia meli za Urusi kuingia katika bandari za Umoja wa Ulaya.
Rais wa Halmashauri ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema wanapanga kupiga marufuku uagizaji wa mafuta pia. Hayo ni kutokana na ushahidi wa kuuawa raia katika mji wa Ukraine uliokuwa umekamatwa na Warusi.
Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya meya wa mji mkuu wa Ukraine Kyiv Vitali Klitschko kutoa wito wa kusitishwa mahusuano yote ya kibiashara na Urusi kwa kile alichokiita kuwa kusitisha usambaaji wa fedha za umwagaji damu."