Eti wazuri tu ndio waombe kazi !

Eti wazuri tu ndio waombe kazi !

Kwame Nkrumah

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2008
Posts
886
Reaction score
376
Katika mihangaiko ya maisha jana nimepita Iringa. Nikawa nasikiliza moja ya radio za hapa, sikumbuki ni ipi, lakini kulikua na tangazo la nafasi za kazi za sales people katika moja ya maduka ya hapa Iringa. Sifa za kazi ni mbili tu.

Ujue kusoma na kuandika Kiingereza na Kiswahili, na pili uwe na mwonekano mzuri.

Mwonekano maana yake uwe mzuri, ni tofauti na mtu akisema nadhifu, mtanashati au mkarimu kwa wateja.

Hii sifa ya pili ndio inanichanganya , ina maana watu wabaya wasiombe? Utajuaje kwamba fulani ametimiza kigezo cha uzuri? kwa sababu uzuri ni mtazamo wa mtu.

Je huu si ubaguzi wa waziwazi? Watu wabaya [kama wapo] kazi zao ni zipi?
 
Wabaya kazi yao kutishia watoto wanaokataa kula/kuoga/kulala.
Ref: Waziri mmojawapo wa JK
 
kigezo cha uzuri hasa kwa jinsia ya 'ke' siku hizi ni mojawapo ya vigezo vya kupata ajira hususan katika kampuni zenye mabosi wakware wa vimwana! hicho kigezo kinaweza kisitangazwe rasmi lakini ktk 'minds' za wakware kimo!
 
Duh haya sie wabaya jamani ndio tutaishia kuvitazama vyeti vyetu ndani ya kabati,apana bado siamini kama uzuri ndio unaokupatia kazi bila elimu yakutosha na uzoefu wa kazi.
 
Hilo duka wanauza nini? Itakuwa bidhaa feki za china ili kuondoa attention ya wateja.
 
mimi huwaga najiulizaga pia kwanini marketing managers wengi wanakuwa wasichana tuuu, tena warembo.
Je ni kweli wanaume hawaziwezi hizo nafasi? ni kweli wanawake wasio na mvuto wenye taaluma nzuri hawanaag hizo sifa?
 
Muonekano mzuri (good appearance) sio necessarily sura nzuri au mtu mbaya unaweza ukawa na sura nzuri ukawa na muonekano mbaya.

Kujibu swali lako je uzuri wa sura una-matter kwenye kazi ? Jibu ni ndio, lakini zaidi ni charisma na likeability ya mtu, kuna mtu ana charisma na anavutia kuwa nae (haogopeshi) hapa siangolei sura bali character, sio mtu wa kununa, amekaa kama myangani n.k., Kama sura yako na appearance ni kama mtu aliyetoka kwenye movie ya kutisha labda apply kazi ya kuwa bodyguard na sio house boy wala muangalizi wa watoto

Kuogopa kuonekana waajiri ni wanyanyapaa au wanabagua au wanatumia watu kama products hawawezi wakasema wazi wazi sura nzuri lakini wakitumia muonekano mzuri hawajafanya kosa.., na hakuna mtu atapenda kuhudumiwa na mtu mwenye muonekano mbaya (hapa from character, tabia mpaka appearance)
 
Wabaya kazi yao kutishia watoto wanaokataa kula/kuoga/kulala.
Ref: Waziri mmojawapo wa JK

Yani leo kutwa nimeshinda na hasira.. We gobore umenifanya nitabasamu. Ubarikiwe lol

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
muslim-woman-in-dress.jpg
1298046993_88565947_3-Female-Cabin-Crew-Air-hostess-at-Air-Arabia-International-Karachi-Islamabad-Hotel-Jobs-Travel-Jobs.jpg


Acheni kujitia wehu, chagueni Air Hostess hapo
 
Duh haya sie wabaya jamani ndio tutaishia kuvitazama vyeti vyetu ndani ya kabati,apana bado siamini kama uzuri ndio unaokupatia kazi bila elimu yakutosha na uzoefu wa kazi.

promiseme
Hunizidi mimi! Sijui tuandamane!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom