Eti wanaume huwa hawaonji mara moja...!

Eti wanaume huwa hawaonji mara moja...!

91331412.jpg


Upo msemo kuwa muonja asali haonji mara moja, na msemo huo hutumiwa sana kuwaelezea wanaume wanaowasaliti wenzi wao kwamba, hata wakifumaniwa, ipo siku watarudia tena.

Niliwahi kujadili jambo hilo humu wakati fulani, kama ungependa kujikumbusha unaweza kubofya hapa chini:

https://www.jamiiforums.com/mahusia...waonji-mara-moja%85%85%85%85%85%85%85%85.html

Leo nina swali kwa dada zangu wa hapa JF:

Tuchukulie kwamba, unaye mpenzi ambaye mmependana sana, ni mwanaume wa ndoto zako, ana karibu sifa zote za mwanaume uliyekuwa unamuhitaji.

Inatokea siku moja katika mazungumzo yako na huyo mwenzi wako kuhusu mahusiano yake ya nyuma anakiri kwamba, wakati fulani aliwahi kuachana na mpenzi wake aliyempenda sana baada ya kumsaliti huyo mpenzi wake na mwanamke mwingine. Anazungumza hivyo bila kuonyesha hisia za kujutia kitendo chake hicho.

Hebu niambie,

1. Je utaichukuliaje kauli yake hiyo?

2. Kama aliweza kumsaliti mpenzi wake aliyempenda sana, je hudhani kuwa hata wewe anaweza kukusaliti siku moja?

3. Je utaamua kujiondoa mapema katika huo uhusiano au utaendelea na uhusiano huo kwa ile dhana kwamba yaliyopita si ndwele?

Hebu kina dada fungukeni hapa.............
mii nadhani there is no need kuchimbua about the past because no one can change it ,
 
ntajuaje na we ulikaa mbali wakati wa doa yetu ulisikiliza maneno ya Baba V lakini basi shetani kashindwa.shikamoo.una wasi wasi kwamba atakuwa amechukua tabia zako?hapana Baba Kaizer tulipooana tuliomba na kuvunja yote mabaya ya koo zetu yasingiie kwenye familia yetu na ndivyo ilivyo.

Nimekumiss sana
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ni kweli kabisa kaka Mtambuzi, Ndiyo maana mm huwa nakataa moja kwa moja, maana kuna wanaume wengine ukimuonjesha tu , lazima ataulizia tena, na ukimwambia hapana Anakwambia mbona siku ile ulinipa, na ukimwambia nilikupa mara moja tu anakwambia anataka tena , Sasa ubaya awe ndiyo boss wako, ameitaka tena na wewe umekataa utaona Rangi zote hapo ofisini, atakufanyia visa mpk utampa tena. Ndiyo maana mm huwa nakataa kabisa tangu mwanzo kama ni hapana ni hapana na sibadilishi mtizamo.

MM NILIOLEWA NA MWANAUME AMBAYE SIKUMTEGEMEA KUWA MUME WANGU , ALIDAI YEYE ANATAKA KUONJA TU,KUMBE ALIKUWA AMENIPENDA ANATAKA KUNIACHANISHA NA MCHUMBA WANGU, BASI ALIFANYA HILA MPK YULE MCHUMBA AKAJUA. NDIPO NIKAWA SINA PA KUSHIKA IKABIDI NIMKUBALI YEYE AWE MUME.
Hivi katika hili ni nani anampa mwenzake na wa kupokea ni yupi. ni nani anaonja na yupi anaonjwa? na je usaliti ni kuacha au ni kuonja pembeni. kwa uzoefu walio wengi huonja/jwa pemben kwa siri kali na wenzi wao wanabaki kuamini hawajasalitiwa maisha yanakwenda! usaliti mbaya ni kumtosa mtu kwa kutaka chungu kipya na kutupa cha zamani
 
Kwi kwi kwi kwiiiiiii! Natumaini Mwita hatoisoma hii!

Hahaha my love mwaJ sasa natangaza rasmi kuanza kumuwinda Jiwe Linaloishi. Namuona kabisa anavyojaribu kutoka sebuleni na kutaka kuingia chumbani.
Sasa kitakachomkuta asije akamsimulia mtu ama akaja hapa kulalamika. Asidhani kukuona umependeza hivyo sura mvuto mvuto hakuna hata dalili za mkwaruzo. Asichojua ni kwamba siku hizi tumekopa mila moja ya wazaramo, ya kuwapiga wake zetu na upande wa khanga na kitenge. Ila mimi nimeboresha ninapiga na pair kadhaa za vitenge vya wax na maunyunyu ya kitaliano!
 
Last edited by a moderator:
Hahaha my love mwaJ sasa natangaza rasmi kuanza kumuwinda Jiwe Linaloishi. Namuona kabisa anavyojaribu kutoka sebuleni na kutaka kuingia chumbani.
Sasa kitakachomkuta asije akamsimulia mtu ama akaja hapa kulalamika. Asidhani kukuona umependeza hivyo sura mvuto mvuto hakuna hata dalili za mkwaruzo. Asichojua ni kwamba siku hizi tumekopa mila moja ya wazaramo, ya kuwapiga wake zetu na upande wa khanga na kitenge. Ila mimi nimeboresha ninapiga na pair kadhaa za vitenge vya wax na maunyunyu ya kitaliano!

Hapo wakurya mlipoamua kukopa mila ya wazaramo ndio nilipowapendea! Mwita Maranya utakuwa na kazi kubwa ya kumuwinda huyo Jiwe Linaloishi. Shauri yako na ubishi wako wa kikurya. Mie na mwanangu Zion Daughter tulikubembeleza twende White Party ukakataa eti unafuatilia suala la wizi wa ng'ombe. Mwenzio Jiwe Linaloishi alitinga kwenye party! Wenzio wanakushinda mambo madogo madogo kwa sababu ya unoko wako! Uwiiiiiiiii! Nimesema tu mume wangu usinipige jamani!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom