Eti TANESCO nao hawalipi Dowans, hiki si kituko? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti TANESCO nao hawalipi Dowans, hiki si kituko?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mrimi, Oct 11, 2011.

 1. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Baada ya juzi Waziri wa Fedha, Mustafar Mkulo kutangaza kuwa wizara yake haipo tayari kulipa deni kwa Dowans, kwa madai kwamba deni hilo linaihusu TANESCO, Jana TANESCO wameibuka na kusema kuwa wanakusudia leo kupeleka mahakamani pingamizi dhidi ya malipo hayo.

  Walichosahau kutuambia hapa ni sababu zilizowafanya wakavunja mkataba ambao kimsingi walijua gharama yake, lakini pia hawajasema siku zote walikuwa wapi hadi uamuzi huo anafikiwa. Lakini pia ni vema wakatuambia mtu(kwa jina) aliyesaini kuingia na kuvujwa kwa mkataba huu kwa niaba ya serikali.

  Lakini pia hawa TANESCO na akina Mkulo wanamdanganya nani kwa jambo ambalo lipo wazi hata kwa kipofu?

  These people cant be serious at all.
   
 2. Bongo Pix Blog

  Bongo Pix Blog JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watuambie aliyewaingiza mkenge kwa ushauri mbovu wa kwanza kuingia katika mkataba ambao alijua ni feki na kisha baadaya nasikia mtu huyo huyo au kampuni akawashauri wauvunje mkataba feki aliowashauri waingie kabla, bila shaka akijua matokeo yake hapo baadaye, maana watawala wetu inaonesha wanasainishwaga mikataba hii na peremende mdomoni hivyo hawana muda kupitia wala kuusoma mkataba husika.

  Je ni nani mshauri huyooo????
   
 3. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapa jamaa alipiga krosi alafu akawahi mbele fasta na kupachika goli la kisigino!!!
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  atalipa EL labda na wale wote waliohusika,
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Naona umetumwa kuja kuwasafisha watu hapa, TANESCO hawakuvunja mkataba, mkataba ulivunjwa na bunge, sasa sema nani alipe hili zigo?.
   
 6. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kama Kuna Serikali ambayo Viongozi wanapata idea zao kupitia Masaburi basi ni hii ya huyu rafiki yake na 50 cents. Hivi ulishaona wapi Waziri wa Fedha anaruka kimanga kwamba hawezi kulipa deni ambalo Serikali yake inadaiwa???
  Kimantiki hata kwa elimu ya Vidudu, Inajulikana Tanesco ni Shirika la Serikali na ndo maana linaposhtakiwa Mwanasheria mkuu wa Serikali anawajibika kupeleka mawakili kwa maana ni sehemu ya kazi yake. Na inapothibtika kwamba wameshindwa kesi na wameamuliwa kulipa deni, obviously ni Serikali hiyo hiyo kupitia Wizara ya Fedha inatakiwa ilipe..Sasa nashangaa Mkulo anaposema 'mimi silipi'...
  Na kituko ni hawa Tanseco wanajifaragua kwenda Mahakamani wakati katika mkataba wao na Dowans walikubaliana kuiwa Mahakama ya Usuluhishi ndio itakuwa maamuzi ya mwisho..sasa huku mahakama ya Rufaa naona ni kupoteza muda tu..Dowans walipwe na Waliosababisha wawajibishwe..full stop!!!
   
 7. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Alipe nani kwetu hiyo siyo hoja ila, wajaribu tutakutana nao JANGWANI - itakua Tahiriri yetu ni square au triangle haijalishi mimi niko tayari nani atanifuata?
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hi kama hadithi ya abunuwasi vile, lakini part II imeanza na inaelekea mwisho ngoja tuone.
   
Loading...