Mahakama yaridhia Tanesco iilipe Dowans Sh111 bilioni

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,406
Mahakama yaridhia Tanesco iilipe Dowans Sh111 bilioni Send to a friend
Wednesday, 28 September 2011 20:15
0digg

werema.jpg
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema

James Magai
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imebariki malipo ya fidia ya fedha kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans ambayo ilisajili hapo, tuzo yake iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).Uamuzi huo unaonekana dhahiri kwenda sambamba na kile alichokisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema kuwa hakuna uwezekano wowote wa kisheria kuepuka malipo hayo.

Kwa uamuzi huo Tanesco sasa inatakiwa iilipe Dowans kiasi cha Sh111 bilioni, badala ya Sh94 bilioni za awali ikiwa ni pamoja na riba ya asilimia 7.5.

Wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama alisema kiasi hicho kimeongezeka kutokana na Tanesco kuchelewa kulipa fidia ya awali tangu kutolewa kwa tuzo hiyo kama pande hizo zilivyokubaliana wakati wa usuluhishi.

“Fidia ya awali katika uamuzi wa ICC ilikuwa ni Dola za Marekani 65milioni, lakini kwa sasa ukiweka na riba ya asilimia 7.5 fidia hiyo imeongezeka hadi takribani Dola za Marekani 72milioni ambazo ni kama Sh111bilioni,” alisema Fungamtama.

“Baada ya kupitia mwenendo na hoja za pande zote, nimebaini kwamba si sawa kwa mahakama hii kuingilia uamuzi wa ICC. Hivyo ninaagiza kuwa tuzo hiyo isajiliwe na iwe hukumu halali ya mahakama hii,” alisema Jaji Emilian Mushi katika uamuzi wake jana. Novemba 15, 2010 AICC, chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen akisaidiwa na wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, ICC iliiamuru Tanesco iilipe Dowans fidia ya Sh94 bilioni kwa kuvunja mkataba kati yake na kampuni hiyo kinyume cha sheria.

Januari 25, 2011 Dowans iliwasilisha maombi Mahakama Kuu ikiomba tuzo yake hiyo isajiliwe ili utaratibu wa ulipwaji wake uwe na nguvu ya kisheria.Hata hivyo, Tanesco kupitia kwa Mawakili wake, Rex Attorneys kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Februari 9, 2011, iliwasilisha mahakamani hapo pingamizi la usajili wa tuzo hiyo.

Tanesco iliwasilisha hoja kumi na moja kupinga tuzo hiyo ya ICC ikieleza kuwa ICC ilijipotosha kisheria katika kutoa tuzo hiyo kwa Dowans na hivyo kuiomba mahakama hiyo iitupilie mbali.Lakini jana, Jaji Mushi alitupilia mbali mapingamizi ya Tanesco na kuamuru tuzo hiyo isajiliwe na kuwa hukumu halali ya mahakama hiyo.

Kwa uamuzi huo, Dowans sasa itakuwa na nguvu ya kuomba mahakama itekeleze uamuzi huo ikiwa ni pamoja na kushikilia mali za Tanesco iwapo itakaidi. Mbali na mahakama kusajili tuzo, hiyo pia iliiamuru Tanesco ilipe gharama zote za uendeshaji wa kesi hiyo.Kilichoiponza Tanesco ni makubaliano yake na Dowans wakati wa usuluhishi ambapo pande zote zilikubaliana pamoja na mambo mengine, kuwa uamuzi wa ICC ndiyo utakuwa wa mwisho na kwamba kila upande utekeleze uamuzi huo mara moja.

Katika uamuzi wake jana, Jaji Mushi alitupilia mbali mapingamizi ya Tanesco akisema kuwa mahakama hiyo haiwezi kuingilia uamuzi huo wa ICC.Ingawa Jaji Mushi alikiri kuwa mahakama hiyo ina uwezo wa kuingilia uamuzi wa ICC pale inapotokea kuwa kuna makosa yaliyofanywa na mahakama hiyo, lakini alisema katika mazingira ya uamuzi wa mgogoro huo mahakama haiwezi kuingilia.

Alielezea kuridhishwa kwake na jinsi mahakama hiyo ilivyoshughulikia na kutolea uamuzi masuala yote ya kisheria yaliyoibuliwa katika mgogoro huo na kuzingatia sheria za Tanzania na za kimataifa.

“Baada ya kupitia hoja zote naomba nitoe muhtasari wa yale niliyoyabaini katika maombi haya. Pande zote ziliingia katika makubaliano (POA) na kukubaliana kutatua mgogoro kwa njia za usuluhishi na kwa mujibu wa kanuni za usuluhishi za ICC.”

“Kwa kusaini makubaliano hayo na kwa mujibu wa makubaliano ya usuluhishi pande zote zilikubaliana na katika uwezo na mamlaka ya kisheria ya ICC katika kuchunguza na mambo mbalimbali yaliyolalamikiwa na kuyaamua,” alisema Jaji Mushi.Pia kwa mujibu wa fungu la 14 (1) la POA, pande zote zilikubaliana kufungwa na kanuni za ICC.

Kwa masharti ya Ibara ya 28 (6) ya Kanuni za ICC, uamuzi wa ICC ndiyo wa mwisho na unazifunga pande zote na hazitatakiwa kukata rufaa,” alisema Jaji Mushi na kuongeza kuwa pia pande hizo zilikubaliana kutekeleza mara moja uamuzi huo.“Hivyo kwa kuzingatia kanuni za sheria zinazohusiana na usuluhishi katika nchi hii na mahali kwingineko, nimebaini kuwa haitakuwa sawia kwa mahakama hii kuingilia uamuzi wa ICC. Kwa kufanya hivyo ni kuruhusu kuhoji tena masuala ya kiukweli na ya kisheria ambayo pande husika zenyewe kupitia kwa makubaliano yake ziliyakabidhi kwa ICC kuyachunguza na kuyaamua. Kwa kusema hayo na kwa sababu nilizozieleza hapo juu maombi haya yanatupiliwa mbali na kuamuriwa kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hili,” alisema Jaji Mushi.

Ninaagiza kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya Usuluhishi (sura ya 15 marekebisho ya mwaka 2002) Tuzo ya ICC iliyowasilishwa katika mahakama hii isajiliwe na iwe uamuzi wa mahakama hii na iweze kutekelezwa,” alisema Jaji Mushi.

Zitto: Ni matokeo ya siasa mbovu
Akitoa maoni yake juu ya hukumu hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe alisema hukumu hiyo ni matokeo ya siasa mbovu.“Tumeingiza nchi hasara kwa sababu ya uongozi dhaifu na siasa za makundi ya CCM,” alisema Zitto na kuongeza:
“Hata hivyo, Tanesco hawawezi kulipa fidia hiyo kwani walilazimishwa kuingia mkataba na hata kuvunja mkataba huo.”

Alisema kamati yake imeshaagiza deni hilo lisitokee katika hesabu za Tanesco na badala yake lilipwe na Serikali.
“Hata Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amegoma kusaini hesabu za Tanesco za mwaka 2010 mpaka Serikali ikubali kubeba mzigo huo,” alisema Zitto.

Madai yalivyoanza
Suala la malipo hayo ya fidia ya Dowans lilianza Desemba 3, 2010.Wiki chache baadaye, yaani Desemba 27, Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu (AG), Jaji Fredrick Werema ilifafanua kwamba iliridhia kulipa fidia hiyo.

Jaji Werema aliwahi kunukuliwa akisema kwamba baada ya kuisoma hukumu hiyo ameridhika kuwa iko sawa na kwamba Serikali haina nia ya kukata rufaa.Januari 6, mwaka huu, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alitoa tamko la Serikali kuhusu malipo hayo akisema kuwa imekubaliana na ushauri wa Mwanasheria Mkuu.

Lakini, Januari 11, mwaka huu, mashirika 17 ya wanaharakati yakiongozwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) yaliwasilisha Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara taarifa ya kusudio la kupinga usajili wa tuzo hiyo.Hata hivyo, Januari 17, mwaka huu, ICC iliwasilisha tuzo hiyo Mahakama Kanda ya Dar es Salaam badala ya Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.

Baada ya kupata taarifa hiyo, Januari 19, mwaka huu LHRC iliwasilisha barua nyingine Mahakama Kuu ikielezea nia ya kupinga usajili wa tuzo hiyo ili isisajiliwe mahakamani hapo.

Januari 25, mwaka huu Dowans kupitia kwa Wakili wake Kennedy Fungamtana iliwasilisha mahakamani hapo maombi ya usajili wa tuzo yake hiyo ili utaratibu wa ulipwaji wa fidia hiyo uwe na nguvu ya kisheria.

Baada ya Dowans kuwasilisha mahakamani maombi hayo ya usajili, ndipo Januari 31, LHRC kwa pamoja na Chama cha Wanasheria wa Mazingira (LEAT) na Kampuni ya Sikika walipowasilisha rasmi mahakamani hapo pingamizi la usajili wa tuzo hiyo.Mbali na wanaharakati hao waliowakilishwa na Wakili Dk Sengondo Mvungi, Mwanahabari Timothy Kahoho naye aliwasilisha pingamizi la usajili wa tuzo hiyo. Pamoja na sababu nyingine, wote walidai kuwa wamechukua hatua hiyo ili kulinda maslahi ya umma.

Tanesco nayo kwa upande wake, kupitia kwa mawakili wake, Rex Attorneys kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Februari 9, mwaka huu waliwasilisha mahakamani hapo pingamizi la usajili wa tuzo hiyo.

Lakini Dowans pamoja na Tanesco waliwawekea pingamizi wanaharakati hao pamoja na sababu nyingine, wakidai kuwa hawana haki ya kisheria kuingilia suala hilo.Septemba 6, mwaka huu, Mahakama Kuu iliwaengua wanaharakati hao baada ya kutupilia mbali mapingamizi yao.Katika uamuzi wake, Jaji Emilian Mushi alikubaliana na hoja za wakili Fungamtama wa Dowans kuwa wanaharakati hao hawakutimiza matakwa ya kisheria pamoja na kanuni zinazotumika katika mashauri ya uwakilishi mahakamani.

Pia Jaji Mushi alikubaliana na hoja za pingamizi za Dowans na Tanesco kuwa maslahi ya umma yanalindwa na kutetewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikal
 
C'mon Zitto,
Tanesco is owned by the URT Government, so it won't make any difference as to who is going to pay.
It's the people either way!!
 
Wengine tulisema humu, kujidai kuzuia malipo kwa baadhi ya wanasheria uchwara ni kuwaongezea faida Dowans. Kiko wapi?

Haya mkatae kulipa muone kilicho mtoa Kanga manyoya!
 
Wengine tulisema humu, kujidai kuzuia malipo kwa baadhi ya wanasheria uchwara ni kuwaongezea faida Dowans. Kiko wapi?

Haya mkatae kulipa muone kilicho mtoa Kanga manyoya!
Ni nini kilimtoa kanga manyoya? Sio lazima ushabikie kila kitu.
 
Tiny Rowlands will never forget Tanzania, especially Nyerere.

Sio Nyerere aliyegeuzwa nyuma (alisema harudishi mali alizotaiisha za Rowlands) na Tiny Rowlands? Alirudisha? hakurudisha? ukishapata jibu utajuwa ni nani ambae hamsahau mwenzake.
 
Sio Nyerere aliyegeuzwa nyuma (alisema harudishi mali alizotaiisha za Rowlands) na Tiny Rowlands? Alirudisha? hakurudisha? ukishapata jibu utajuwa ni nani ambae hamsahau mwenzake.
AFRICA: Bye-Bye for Tiny Rowland - TIME

Multinational Monitor, February 1980


Some World Bank officials who have followed the dispute privately suggest that Lonrho's broadside against Tanzania may not make financial ' sense for the company. Tanzania's President Nyerere is well known for his willingness to sacrifice foreign aid when he believes principles are at stake. In November, Nyerere rejected an aid program proposed by the International Monetary Fund that included conditions he believed would place intolerable hardships on his country's peasant majority. "People who think that Tanzania will change her cherished policies of socialism and self-reliance because of the current economic difficulties are wasting their time," Nyerere said.
The same dynamics may be at work in the Lonrho dispute. "(t would seem to me that private negotiations are in order," said one Bank observer. "Instead of sending cables all around the world, Lonrho should be trying to quietly negotiate. I think Rowland may be making a mistake here, by underestimating Nyerere's resolve to withstand strongarm tactics." To date, the Tanzanians have maintained their equanimity in the dispute. "We promised we would negotiate fairly," says Felix Mrema, the economics officer in Taniania's United States embassy who serves as his country's lion at the World Bank. "We are in the process of negotiating. These Lonrho cables are just a way of pressuring us to accept their figure." - SOURCE, Multinational Monitor,VOL.1, nO. 1, February 1980.

Dondosha Data Shangazi langu, usibwabwaje maneno kama hujaenda shule vile.... unatuaibisha watu wa pwani, we are better than what these people think!
 
duh hii kwa kweli inatuwekapabaya sana wananchi umeme wenyewe wa magumashi halafu deni nalo ndo hilo mh
 
Back
Top Bottom