3squere
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 925
- 181
Na Flora Mwakasala
MAHAKAMA ya Rufaa imetupilia mbali ombi la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya Mahakama Kuu, iliyoamuru wailipe Sh bilioni 94 kampuni ya Dowans.
Katika ombi hilo Tanesco walidai kuwa fedha hizo walizoamriwa kulipa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) kutokana b kukatisha mkataba kinyume cha sheria ni nyingi na hawana uwezo wa kulipa.
Aidha wanadaia kuwa, kama watatekeleza hukumu hiyo, itaathiri uwezo wake wa kuzalisha na kusambaza umeme nchini na hivyo kusababisha tatizo kubwa la ukosefu wa umeme, ambao utaathiri uchumi wa nchi kwa jumla.
Katika hoja zao, walidai kuwa tayari walishawasilisha nia ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na ya Mahakama Kuu na wanaamini watashinda rufaa hiyo.
Akisoma uamuzi huo jana, Naibu Msajili wa mahakama hiyo Elizabeth Mkwizu, alitupa ombi hilo na kuiamuru kwa kuwa waliwasilisha ombi hilo nje ya muda unaotakiwa kisheria.
Mahakama hiyo ilikubaliana na hoja za Wakili wa Dowans Kennedy Fungamtama aliyedai ombi hilo lilipaswa liwasilishwe katika muda wa siku 60 tangu kutolewa kwa hukumu, lakini badala yake Tanesco iliwasilisha maombi hayo baada ya siku 351.
Septemba 28, mwaka juzi, Mahakama Kuu iliiamuru Tanesco kuilipa Dowans fidia ya Sh biloni 94 na riba ya asilimia 7.5 baada ya kukubali kuisajili tuzo ya Dowanc.
Katika hukumu ya Mahakama ya ICC, iliyotolewa Novemba 15 mwaka juzi, Tanesco iliamriwa kuilipa Dowans Holding SA na Dowans Tanzania Ltd (Dowans) dola za Marekani milioni 65, pamoja na riba na gharama za kuendesha kesi, baada ya kuvunja mkataba na kampuni hiyo kinyume cha sheria.
Hata hivyo, Tanesco ilipinga hukumu hiyo lakini Septemba 28 mwaka jana, Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu, alikubali kusajili tuzo ya malipo ya Dowans na kuiamuru Tanesco kulipa fedha hizo pamoja na gharama za uendeshaji kesi.
Baada ya hukumu hiyo Tanesco iliwasilisha ombi la kibali cha kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na ombi la kusimamisha utekelezwaji wa hukumu hiyo.
Hata hivyo Februari 20, mwaka jana , Mahakama ilitupilia mbali ombi la kibali cha kukata rufaa na Septemba 6, 2012, pia mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi la kusimamisha utekelezwaji wa hukumu hiyo.
Kutokana na uamuzi huo, ndipo Tanesco wakafungua ombi la kusitisha utekelezaji wa hukumu hiyo katika Mahakama ya Rufaa, huku wakitoa hoja walizozitoa katika ombi la Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa Wakili wa Dowans, Kenedy Fungamtama, hadi kufikia Novemba mwaka jana, deni la Dowans lilifikia zaidi ya Sh bilioni 122 kutokana na kuongezeka kwa riba ya asilimia 7.5 ya deni la awali la kila siku.
Mwisho.