Eti mtalaka hatongozwi!

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
9,330
2,000
Habari za Jumatatu wanajamvi!!
Kwa wale wenzangu poleni na mning'inio!

Nije kwenye mada,
Jana tukiwa na washikaji tunapiga Moja-Mbili na marafiki wakiwa na wenza wao, ikaja story eti linapokuja suala la wapenzi ambao wameaacha wanapoonana kwa mara nyingine baada ya kipindi fulani kupita huwa ni rahisi sana kurudisha majeshi na kurudia raha zile mlizokuwa mkipata wakati huo kabla ya kuachana!

Basi kila mmoja alitoa ushuhuda wake hapa na pale lakini kwa asilimia kubwa ya wadau waliokuwepo hapo (wakike na wakiume) walionekana kuafiki kuwa MTALAKA HATONGOZWI!

Wanajamvi hili lina ukweli wowote?

Naomba kuwasilisha kwa mjadala!
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,169
2,000
hakuna ukweli........
unadhani mkiachana kwa vurugu na vishindo unaweza kujirudia tu?
talaka si mchezo...
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
9,330
2,000
hakuna ukweli........
unadhani mkiachana kwa vurugu na vishindo unaweza kujirudia tu?
talaka si mchezo...

Na kama hamjaachana kwa vurugu wala vishindo je?
maana kuna wapenzi huwa wanaachana kwa Amani ingawa kinyongo kinakuwepo kwa mbali!!
 
mbalu

JF-Expert Member
May 18, 2012
550
195
Talaka ya ndoa ipi, ya kukutana kona bar usiku mkadumu wiki moja au ya ndoa ya kimila, kanisani, msikitini, au bomani?
 
Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,614
0
Na kama hamjaachana kwa vurugu wala vishindo je?
maana kuna wapenzi huwa wanaachana kwa Amani ingawa kinyongo kinakuwepo kwa mbali!!

Mkuu bado inategemeana na mahusiano yenu yalikuwaje? Kama mahusiano yenu yalikuwa mje muishi kama mke na mume kisha mmoja akamess up utalaka huo unakuwa mgumu kurudisha majeshi.

Utalaka ambao unaweza kurudisha majeshi ni ule ambao kila mmoja anajua ni wa kula bata na kwa bahati mbaya mkatengana kwa amani.
 
CUTE

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
1,230
0
Habari za Jumatatu wanajamvi!!
Kwa wale wenzangu poleni na mning'inio!

Nije kwenye mada,
Jana tukiwa na washikaji tunapiga Moja-Mbili na marafiki wakiwa na wenza wao, ikaja story eti linapokuja suala la wapenzi ambao wameaacha wanapoonana kwa mara nyingine baada ya kipindi fulani kupita huwa ni rahisi sana kurudisha majeshi na kurudia raha zile mlizokuwa mkipata wakati huo kabla ya kuachana!

Basi kila mmoja alitoa ushuhuda wake hapa na pale lakini kwa asilimia kubwa ya wadau waliokuwepo hapo (wakike na wakiume) walionekana kuafiki kuwa MTALAKA HATONGOZWI!

Wanajamvi hili lina ukweli wowote?

Naomba kuwasilisha kwa mjadala!
sio kweli bana ........tukiachana ndio mazima i neva look back na hata akija halambi kitu tena
 
Yummy

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,796
1,195
Hiyo kitu inawezekana kwa wengine......na ili kitendo kifanyike mara nyingi huwa inategemea na mwanamke akitoa 'go ahead' anakula kichapo kama wako kitandani kwao kwa zamani.
Mwanamke akionyesha msimamo hicho kitu hakiwezi tokea,nna uhakika. Wanaume huwa mnakamatika kirahisi sanaaaa,labda huyo mwanamke awe amekutenda na hutaki hata kumsikia hapo ndo mnaweza kuponea.
Hivi lkn jamani nyie kaka zetu ni kitu gani huwa kinawafanya mrudi kuomba unyumba kwa mtu ambae mmeachana kwa makasheshe kibaooo hamuonagi aibuu???
 
gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,268
2,000
Hatongozwi na nani? pili ni talaka ya ngapi? kama ni talaka 3 huyu anatongozwa na kuolewa tena,kama ni talaka moja huyu hatongozeki manake yuko chini ya kifungoo cha mumewe na kama ni mbili pia. Ukitaka kumkomoa mwanamke mpe talaka moja yaani ni kifungo cha maisha haawez kuolewa tena atabaki kupaa short time tu.

kwa wale marafiki hakunaga talaka ktk urafiki bali kuna mahusiano kuvunjika tu. kurudiana ama kutokurudiana inategemea.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom