Eti, kweli kuwa huku ndiko tunakoelekea???

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Nilikuwa napitia Katuni za Nasani Mpangala nikakutana na kitu hiki kilichonifanya nifikirie mambo mengi sana kuhusu mustakabali wa nchi hii.
Amechora kwa kifupi na kaweka maneno machache sana lakini imenichukua nusu siku kuitafakari katuni hii.

Kiswahili.jpg
 
ziwa victoria ni jina alilotoa mzungu ingawa lipo hapa tz na lilikuwa na jina lake(silikumbuki)
 
Jamaa kafikiria mbali sana
Hawa jama wachora katuni mawazo yao huwa ayaishii pale pua zao ziishiapo, ni viona mbali vyenye uwezo mkubwa sana ambavyo kama jamii tungekuwa mbali tungevitumia iapswavyo.
Naheshimu sana kazi zao.
 
Kwa hisani ya watu wa marekani tutajifunza lugha yetu.

Hilo linawezekana, na huenda wameshakamilisha hiyo program na wanasubiri the right time to implement hiyo kitu.
Mpaka sasa hivi Tayari wana Program maalum ya kila mwaka ambapo huchukua watanzania na wakenya ambao ni Graduates kwenda kufundisha Kiswahili nchini mwao.

Hata wakati ule Mjeremani ndiye alikieneza kiswahili hapa Tanzania, kwani kule kwao walianzisha program maalum kwa ya kuwafundisha maofisa wao walioteuliwa kuja katika himaya zao nchini mwetu. Maofisa hao walifundishwa Kiswahili nchini ujeremani hivyo walikuja wakiwa tayari wanakifahamu.

Hakuishia hapo tu bali walihakikisha kiswahili kinatumika kufundisha katika shule za wakati ule. Lakini kwetu imekuwa tofauti, kwani mpaka hapa tulipofika naona kabisa Mmmarekani yupo mbioni kuichukua lugha hii, ni afadhali kama angeichukua kwani ingeonekana tumefanikiwa kuikuza , bali inaonekana sisi ufahamu wa lugha hii unatupungua kwa kasi na tupo mbioni kuunda lugha tofauti toka ubavuni mwa Kiswahili.
 
sijaelewa. hii mada nimeisoma ktk hoja mchanganyiko na mleteji akiwa lizzy, so hapa mada ni hiyohiyo mleteji mwingine .............. msaada tutani wadau......?
 
Kama leo miaka 50 baada ya uhuru wanatumia madini yetu bila ya ktunuaisha wenyewe basi elewa huko ndiyo tunakaelekea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom