Eti huyu nae anataka malipo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti huyu nae anataka malipo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Aristolicius, Sep 2, 2012.

 1. A

  Aristolicius Senior Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  habari jf!
  Kuanzia form 4 nilianza urafiki wa kawaida na binti moja jirani yetu,niliponza f5 urafiki ukageuka kuwa mapenzi ila sikuwahi kufanya nae mapenzi hadi siku moja wote tukiwa f6 ambapo ndo ilikuwa mara yangu ya 1 na yake kufanya tendo hilo ,kosa lililozua kosa jingine ambapo binti alipata mimba ila kwa bahati nzuri aliweza kufanya mitihani yake bila kugundulika,baada ya mitihani mimba ikawa kubwa wazazi wako wakahoji na mimi nikatajwa kama muhusika,baada ya vikao vya pande mbili za wazazi,wazazi wangu walikubali kumtunza binti na mtoto,na wazazi wake wakasema kama faini wazazi wangu watawajibika pia kumsomesha binti,hivyo binti alijifungua mtt wa kike na baada ya matokeo wote tulifaulu mm nikapata scholarship yy akachaguliwa udsm,wazazi wangu walikuwa wanampa hela za matumiz na kumpangia nyumba dar huku wenyewe wakabaki wakitunza mtt,wakati walikizo binti alipewa gari limsaidie kumpeleleka mtt clinic na shughuli nyingine ,cha kushangaza ni kwamba baada ya kumaliza masomo binti alihamia nyumbani akitafutiwa kazi anatoa visingizio anagoma na nyumbani amekaa tu hatki kufanya kazi hata za kumhudumia mwanetu eti anasema anataka alipwe! Na wakati huo huo anasema amilikishwe gari lile,anasema wasipo fanya hivyo ataenda na mtt nchi tusioijua na hatuta muona,
  naombeni msaada wenu nifanyeje?
   
 2. D

  DAVIES JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 513
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  damu ya mtu haipotei kaka kaona mnatekeleza kila asemacho sasa anataka kuwasumbua mpe onyo kali kama mtoto kakua mkomboe umchukue ili iwe mwisho wa usumbufu na kama unaoa oa ijulikane
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  mwambieni aende msiwe watumwa
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sasa gari la wazazi wako linamhusu vipi?

  mwambie aende popote anapotaka
  kama ana elimu ya chuo
  basi anajua anachokifanya
  hawezi shindwa kumlea mwanae
   
 5. ANKOJEI

  ANKOJEI JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  apo muda wakt anasoma na wewe uko majuu hujaeleza nini kilikuwa kinaendelea kati ya wewe na yeye, nahisi una mzungu!
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli iliyopo mchukuwe mwanao huyo kwani atakuwa amekwisha kukua vya kutosha na pongezi kwa wazazi wako walichokifanya ni zaidi ya ubinadamu
   
 7. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  BLACKMAILING!?sasa akishapewa gari ndo kinakuwa nini?hatalea tena mtoto?au ndo atamtunza mtoto vizuri?
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Hii wala sio blackmailing
  ni kumuendekeza tu....

  keshawasoma na kujua wako weak na waoga
  na wanaingizwa mjini kirahisi

  angekutana na zile familia 'za kumfukuza na mimba yake'
  unafikiri angeanzia wapi?
  wema na ustaarabu unawaponza baada ya kukutana na 'kishangingi cha mjini'
   
 9. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Tulia mkuu. Kwa uzoefu wangu, toto litakuja kukutrace tu. Nimeshaona ishu kama hizi zikitokea, lkn mwisho wa siku mtoto atarudi tu zizini. Wacha akusaidie kulea kwanza.
   
 10. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Sijaelewa hapa, malipo ya nini? Alibakwa? Alilazimishwa? Nimesoma kwa umakini sana hii thread yako sijaona sehemu yeyote iliyoonyesha ulimlazimisha kufanya hiko kitendo zaidi ya kuwa na uhusiano naye kwa muda mrefu. Mtoto aliyezaliwa ni matokea ya kosa mlilofanya wote, wewe na yeye na ktk hili sidhani kama kuna suala la Malipo.

  Naunga mkono jitihada ya wazazi wako kumshughulikia na kumsomesha huyo binti maana kwa kufanya hivyo wameonyesha ukomavu wa hali ya juu sana juu ya malezi na makosa ya watoto. Vitendo mlivyomtendea huyo binti ni vya kibinadamu kabisa ila inaonekana anataka ku-capitalize kwenye wema na wajibu wa wazazi wako kujipatia mtaji.

  Jambo la kujiuliza ni hili, je uko tayari awe mkeo? Kama jibu ni hapana hakuna sababu ya kuendelea kumbembeleza hata kidogo na kisheria hana uwezo wa kumchukua mtoto maana mlimuhudumia kwa kila kitu na hivyo mtoto ni wako. Lakini ikiwa jibu ni ndiyo, unataka awe mkeo, nafikiri una kazi ya kufanya maana mkeo huyo mtarajiwa anaonekana ni mtu mwenye tamaa, asiyependa kufanya kazi na aliyetawaliwa na uvivu na pia hana shukrani. Ni vyema utafakari mienendo yake!
   
 11. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,378
  Likes Received: 690
  Trophy Points: 280
  hili swala ni lako mzee wazazi waliingia kichwa kichwa na huyu binti anacho taka zaidi ni ndoa ila anashindwa kuwa mkweli sasa mwambie asiendelee kuwasumbua wazazi wako kwanza ameshakuwa mtu mzima kama vipi aende mahakamani kwani kuzaa na mtu tija!bora aende kama ana kuuzia mtoto kieleweke
   
 12. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hapa nilipo-underline naunga mkono hoja!
   
 13. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  Wale wa una mimba yangu?nipe niichukue mwenyewe!angejuta!
   
 14. A

  Aristolicius Senior Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wazazi wangu wanampenda mjukuu pia wanahofia malezi ya mtt wanasema kwa akili yake atamuharib
   
 15. A

  Aristolicius Senior Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  anataka malipo kwa kumuhudimia mtoto anasema sio kazi yake ni ya housegirl
   
 16. A

  Aristolicius Senior Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hapana sina mzungu most of my time nimekuwa nikimfikiria kama mke mtarajiwa,i still love her ila anayoyafanya ndo saiz yananichanganya
   
 17. A

  Aristolicius Senior Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mtoto yuko nyumbani na yy yuko hapohapo
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kudinyana nae ulikuja kutaka ushauri wetu?

  Kila mmoja atabeba msalaba wake.
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  huyo anajua uehaifu wenu anawaendesha.......
  Angekuwa nyumbani kwangu mtoto ningelea mie na mume wangu na housegirl, na yeye akakaa kama pambo la nyumba.......ale, anye anenepe.... Na mtoto akitimiza miaka saba tu namwambia akatafute ustaarabu wake nyumbani kwangu sio guest house....

  Kuna watu wanapenda ku-learn the hard way.....
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  kuna binadamu mnapenda matatizo eeeh? Huyo sio mwanamke wa kuoa
   
Loading...