Eti huyu nae anataka malipo!

mkuu sasa mbona huyo binti anawaendesha? Makubaliano ya wazazi ilikua kwamba wamsomeshe na mtoto watamlea sasa mbona huyo binti anafanya vitu vya hovyo kabisa?
Mkumbushe makubaliano kati ya wazazi wenu na asiende kinyume ya hayo
 
pole mkuu ila huyo mwanamke sio kabisa ameanza kuwashefua wazaz anadhan watakubali awe mkwe mayb kwasababu tayari mna mtoo ndio anachukulia hicho kigezo
 
ndio ni mtoto wake ila unafikiri mtu huyu asiependa kazi na anaependa cheap money anaweza kumraise mtoto in good morals
Bw mwache aende unamng'ang'ania wa nini kwanza unadai umechovya mara moja, mara bahati mbaya, mara anadai gari, mara watakugongea siku ukichacha ww umeshaona mvivu tafuta mwingine oa.
Umetuomba ushauri, tunakupa kumbe unampenda sie tunapoteza MB kukushauri MWAAAACHEEE HAFAIIII
 
Piga tumakofi tuwili tu tatu akili ikae sawa labda kuna ka kaspring kame fyatuka kichwani!
 
habari jf!
Kuanzia form 4 nilianza urafiki wa kawaida na binti moja jirani yetu,niliponza f5 urafiki ukageuka kuwa mapenzi ila sikuwahi kufanya nae mapenzi hadi siku moja wote tukiwa f6 ambapo ndo ilikuwa mara yangu ya 1 na yake kufanya tendo hilo ,kosa lililozua kosa jingine ambapo binti alipata mimba ila kwa bahati nzuri aliweza kufanya mitihani yake bila kugundulika,baada ya mitihani mimba ikawa kubwa wazazi wako wakahoji na mimi nikatajwa kama muhusika,baada ya vikao vya pande mbili za wazazi,wazazi wangu walikubali kumtunza binti na mtoto,na wazazi wake wakasema kama faini wazazi wangu watawajibika pia kumsomesha binti,hivyo binti alijifungua mtt wa kike na baada ya matokeo wote tulifaulu mm nikapata scholarship yy akachaguliwa udsm,wazazi wangu walikuwa wanampa hela za matumiz na kumpangia nyumba dar huku wenyewe wakabaki wakitunza mtt,wakati walikizo binti alipewa gari limsaidie kumpeleleka mtt clinic na shughuli nyingine ,cha kushangaza ni kwamba baada ya kumaliza masomo binti alihamia nyumbani akitafutiwa kazi anatoa visingizio anagoma na nyumbani amekaa tu hatki kufanya kazi hata za kumhudumia mwanetu eti anasema anataka alipwe! Na wakati huo huo anasema amilikishwe gari lile,anasema wasipo fanya hivyo ataenda na mtt nchi tusioijua na hatuta muona,
naombeni msaada wenu nifanyeje?

Huyu dada wa ajabu, usomeshwe na kazi utaftiwe bado hutaki kweli kusoma sio kuelimika. Huyu hata badae atakuwa mzigo sana kwako tena kwelikweli kazi unayo.
 
kwanza pole mkuu....pia hongera kwa kumlea mtoto na kumsomesha huyo binti....ushauri wa bure hafai kuwa mke coz yupo kimaslahi zaidi,na atakufanya ujutie hyo ndoa,achana nae na uchukue mtoto ,km hataki mwambie aondoke nae uone km ataendelea na huo ujinga
...pili muweke wazi kuwa huna mpango nae na aendelee na maisha yake...trust me hawezi kuendelea kuwasumbua km kweli mtakuwa serious
 
Huyu dada wa ajabu, usomeshwe na kazi utaftiwe bado hutaki kweli kusoma sio kuelimika. Huyu hata badae atakuwa mzigo sana kwako tena kwelikweli kazi unayo.
.......tena wa ajabu haswaaa,piga chini tafuta mwingine wa kuoa huyo atawaendesha ww na familia kiujumla
 
Back
Top Bottom