Eti hili ni la kweli kuhusu bank ya CRDB?

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,043
2,000
Wakuu,naomba kuulza,eti ni kweli crdb huwa hawaajiri graduates wa vyuo vingne tofaut na sua,kama ni kweli wanatumia vigezo gani?
 
Labda graduates wa kutoka SUA uwa hawana tabia ya kuhamahama kazi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
 
graduate wa SUA hawana options nyingi hivyo wakipata kazi sehemu, hawatoki ng'o, vilevile si risk taker, lakini katika ngazi za kufikiria CRDB hawaajiri kutoka SUA.
 
Hahaha namjua dogo mmoja wa SUA alikuwa na position moja nzuri ndani CRDB lakini haitoshi kuthibitisha uyasemayo.
 
Labda mimi sijaelewa, kwa ninavyofahamu asilimia kubwa 50% na zaidi ya wafanyakazi wa crdb bank plc, ni graduates je unataka kumaanisha wote wametoka SUA? ama unataka kutuaminisha kama unavyoamini wewe kuwa graduate wa SUA ndio wana SUIT zaidi crdb bank plc?? ufafanuzi pls.
 
katika akili ya kawida kabisa,hicho kitu siyo kweli.graduate wa chuo chochote kile akikidhi vigezo vyao vya kazi mara baada ya interview,huajliwa maramoja,bila kuangalia katoka chuo gani.
 
Kuna watu walikua wanaamin kua graduate wa SUA hawana option nying kwa hiyo wakiajiliwa haondoki na baadhi ya mabenki yanataka kupunguza idadi ya wafanyakazi wanaoacha kazi mara kwa mara. Ila kwa sasa kazi zimekua ngumu hakuna tena kitu kama hicho.
 
Kozi za SUA hazina mvuto na ajira yake ngumu ndio maana wanawaajiri kwa kuwa huwa hawahami kabisaa.
 
Kozi za SUA hazina mvuto na ajira yake ngumu ndio maana wanawaajiri kwa kuwa huwa hawahami kabisaa.

Asikudanganye m2 mkuu wangu, yaani ni graduates wachache sana wa SUA ambao wanasota muda mrefu kitaa. Kozi sa SUA ziko very diversified....chukua hata wale wanaosoma purely agricultural courses, huko unakuta units za kutosha za marketing, economics, project management& evaluation,operations research as well as social science researches. Tofauti na vyuo vingine ambavyo huwa wanasoma tu qualitative research; pale wanapiga hadi quantitative na wanaifanyia kazi kwenye special project (disertation) ambapo m2 anatengeneza proposal, anaenda kukusanya data na anafanya hadi data analysis nd interpretation. Kutokana na hiyo diversification, unakuta graduates wake wana-fit sehemu nyingi mno kv serikalini, kwenye research insitution, mabenki na NGOs. Na ndio maana utakuta m2 amesoma kilimo lakini anafanya kazi as loan officer na ana-fit kutokana na hiyo diversification. Na karibu kozi zote wanapiga Biometry....hii ni advanced statistics ambayo kama haupo fit lazima ikumwage mapema kabisa na ni muhimu sana kwenye masuala ya research. Ukiacha kozi hizo ambazo ni purely agricultural courses, kuna kozi zingine kv agroeconomics, environment science as well as wildlife management.....hawa wote ni wachache sana wanasota kitaa kwa muda mrefu. Nakumbuka class ye2, ni wachache sana (tena kama wapo) ambao walimaliza miezi 18 kitaa.
 
CRDB imewekeza sana kilimo kwanza,labda ndiyo maana wanaajiri kwa wingi hao jamaa waliosomea majani SUA
 
siyo graduate wote wanatoka sua ila wanapewa kipaumbele ikitokea wawili mnavigezo vinavyofanana na anatakiwa mmoja basi atachukuliwa wa sua, ukweli kigezo ni nicho kuwa hawaondoki. mimi nimefanya kazi crdb tuliingia watu 90 mwa 2006 kwa mwaka mmoja wa sua walikuwa 30 wote hadi lea bado wapo wale wengine kati ya 60 walibaki 7 tu kwa kipindi cha miala mitatu.
 
Asikudanganye m2 mkuu wangu, yaani ni graduates wachache sana wa SUA ambao wanasota muda mrefu kitaa. Kozi sa SUA ziko very diversified....chukua hata wale wanaosoma purely agricultural courses, huko unakuta units za kutosha za marketing, economics, project management& evaluation,operations research as well as social science researches. Tofauti na vyuo vingine ambavyo huwa wanasoma tu qualitative research; pale wanapiga hadi quantitative na wanaifanyia kazi kwenye special project (disertation) ambapo m2 anatengeneza proposal, anaenda kukusanya data na anafanya hadi data analysis nd interpretation. Kutokana na hiyo diversification, unakuta graduates wake wana-fit sehemu nyingi mno kv serikalini, kwenye research insitution, mabenki na NGOs. Na ndio maana utakuta m2 amesoma kilimo lakini anafanya kazi as loan officer na ana-fit kutokana na hiyo diversification. Na karibu kozi zote wanapiga Biometry....hii ni advanced statistics ambayo kama haupo fit lazima ikumwage mapema kabisa na ni muhimu sana kwenye masuala ya research. Ukiacha kozi hizo ambazo ni purely agricultural courses, kuna kozi zingine kv agroeconomics, environment science as well as wildlife management.....hawa wote ni wachache sana wanasota kitaa kwa muda mrefu. Nakumbuka class ye2, ni wachache sana (tena kama wapo) ambao walimaliza miezi 18 kitaa.

This is same story I hear from engineers, scientist and doctors. Wengi wanaamini wamesoma vitu so diverse kwamba wanaweza kuingia popote na wakafanya maajabu. Ila mimi kama scientist/mkulima/mhandisi siamini hivyo hata kidogo. Haya mambo yakusema tunaweza kila kitu ndo yametufikisha hapa tulipo. Tumetengeneza matatizo mengi sababu tu tunajua sana kuliko wataalamu.
 
Mimi naamini graduate yeyote anapenda kufanya kazi kwenye kitu alichosomea, na ndio maana alikisomea in the first place.

Sasa kama umesomea SUA degree yako ya udongo sijui ukaishia Bank Teller CRDB nadhani lngo halijafikiwa na ni sawa kusema huyu mtu bado anasota.
 
Wakuu,naomba kuulza,eti ni kweli crdb huwa hawaajiri graduates wa vyuo vingne tofaut na sua,kama ni kweli wanatumia vigezo gani?

Sio kweli. Wapo graduates wengi tu toka vyuo vingine
 
Mimi naamini graduate yeyote anapenda kufanya kazi kwenye kitu alichosomea, na ndio maana alikisomea in the first place.

Sasa kama umesomea SUA degree yako ya udongo sijui ukaishia Bank Teller CRDB nadhani lngo halijafikiwa na ni sawa kusema huyu mtu bado anasota.

Mkuu wangu,
Kwa staili hiyo basi hapa Bongo over 50% ya employed graduates wanasota manake hilo lipo kwa wahitimu wa vyuo vyote......with exceptional of very few nd may be wale waliosoma shahada za mwelekeo wa sayansi kv doctors, engineers nd the like. Lakini kwa hawa wa social science nd art graduates wengi wanafanya kazi tofauti na kile walichosomea. By the way, mi nazani elimu ya chuo kikuu ina maana zaidi ya kufanya kazi ya ki2 ulichosomea ingawaje inakuwa vizuri maradufu ikiwa hivyo. Jambo la msingi ni namna gani mtu unaweza ku-translate kile ulichokisoma katika kukabiliana na changamoto mpya iliyopo mbele yako. Binafsi niliwahi kufanya kazi ya u-teller kwa muda mfupi.....tatizo nililokuta pale ni ku-balance. Ilikuwa ni kawaida kukuta bank hall inafungwa saa 11 lakini mtu anamaliza ku-balance saa 1 usiku. Binafsi sijasoma accounting(niliacha accounts nikiwa form ii). Lakini baada ya ku-work as a teller...enzi hizo ilikuwa unafanya purely manual balancing na tatizo kubwa lilikuwa alot of paper works...mara uandike hapa mara uandike kule kisha uchukue calculator na upuuzi mwingine kama huo. Wanaofahamu ule u-teller wa aina hiyo, teller alitakiwa kuwa na Cash Receipts na Cash Payments na ana-record humo kila ki2 na mwisho wa siku anaanza ,kujumulisha jumlisha kwa calculator. Mie nikaona taabu na hayo mambo; nika-design simple excel sheet ambayo nikaweka formulas mbali mbali na kila transaction nikawa naingiza humo. Ninapoingiza last transaction, hapo hapo napata Total Receipts na Total Payments na hapo hapo naona kama nime-balance au hapana!! Kinachobaki hapo ni kuhesabu cash na kuona kama zinawiana na net results niliyonayo kwenye excel sheet. Jamaa wakawa wanashangaa inakuwaje mara mtu wa mwisho anapotoka dirishani nakuwa tayari nimeshapata entries zote. Hiyo ndio maana ya kusoma chuo kikuu otherwise itakuwa umeenda kule kukariri tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom