Ethiopian Airline Boeing 767 yatua Arusha kwa dharura

Hii taarifa hat kama imetoka kwa mkurugenzi mkuu mamlaka ya usafiri wa anga, bado mimi siiamini, maneno ya kusema "pailot alisema" hayawezi kukidhi. Nitaridhika ikiwa nitaona quote za maneno ya huyo pilot.

Hapa mjini jamani acheni tu, leo nilipita kijiwe fulani kule city centre kupiga kiwi niikasikia et ndege illikuwa na mzigo drugs na ndo maana mchezo huo ulichezwa, wadau is it possible?
 
NN,
Huyo walau alitua usiku. Ila huyu wetu ilikuwa mchana kweupee na angalia picha hapo juu unaona kabisa ile mistari ya Pundamilia ipo mwanzo tu na hii ikimaanisha uwanja ni ufupi sana. Check juu nilivyomjibu Pasco.
Kukosea kutua katika uwanja inawezekana bana. Mbona hii DreamLifter ilitua kimakoa katika uwanja wa Jabara huko Wichita? Na hii imetokea mwezi jana tu!

Tuelezee kama huyo rubani hakutua katika kiwanja kisicho.....
 
NN,
Huyo walau alitua usiku. Ila huyu wetu ilikuwa mchana kweupee na angalia picha hapo juu unaona kabisa ile mistari ya Pundamilia ipo mwanzo tu na hii ikimaanisha uwanja ni ufupi sana. Check juu nilivyomjibu Pasco.

Mami, huyu wa U.S. Air Force mbona naye alitua mchana kweupee huko Tampa, FL.

Hizi mishaps hutokea bana hususan kama viwanja vipo karibu karibu. Mimi ningeona ajabu sana kama huyo rubani angeenda kutua Ouagadougou ilhali destination yake ilikuwa Arusha.

Last edited by a moderator:
wapendwa mimi nadhani hii ndege inaweza kutumia barabara kama ya kutoka dukabovu kuelekea kisongo kama running track ya kurukia kwa dharura.naomba kuwasilisha wazo langu.

Hii ndio inaitwa thinking outside the box.....kama barabara iko straight na hakuna obstacles za kuifikisha sehemu husika! Why not?
 
Haikutua Kwa dharura kisongo, rubani aliambiwa azunguke Ili KIA wakishaitoa ndege ndogo arudi kutua, KIA walipokuwa Tayari wakamuita, akasema Sawa Na runway keshaiona, KIA wakamwambia hawamuoni aeleze anatua kutoka upande gani, akawaeleza, wakamsisitiza kuwa hawamuoni ye alipowahakikishia kuwa anauona uwanja, wakamruhusu kutua. Ifahamike pia kuwa kutua ndege haihitaji umbali mrefu sn, tatizo kuruka, Hapo Sasa tusubiri kitakachotokea

Maelezo yako yana upungufu wa kitaalamu. Àir Traffic Control tower wanaiona ndege ilipo kwa kutumia radar. Pilot wa EA alitua ARK wa kufanya mawasiliano na ARK AT control tower na sio CT ya KIA.

Ukweli ni kwamba Ethopian airline ilizunguka wa muda wakati ikisubiri go ahead kutua KIA. Baada ya kuona inachukua muda zaidi na kuzingatia kiwango cha mafuta kilichopo ilikuwa vigumu kwa rubani kuendelea kuzunguka na hivyo kuomba clearance kutua kwa dharula ARK.
 
Haiwezekani ukachukua "abiria wengi/mizio mingi" kwenye ndege sababu abiria, mafuta, mizigo kila kitu kina kipimo chake cha uzito unaoruhusiwa. Haiwezekani ukapunguza kimoja na ukazidisha kingine. At any rate, ukiongeza abiria au mizigo, ina-imply mafuta itabidi yawe mengi, na siyo machache.

Du...hii thinking ni ya complete Junior physics!
 
Jamani jamani kila mtu anajifanya anajua aviation industry humu ndani kumbe wote product ya wikipedia na google unakuja unatiririiiiiika mara ohh haiwez paa tena mara hili mara lile kama ma airbus dreamlifter yanaweza ondoka in small airport hiyo itashindwa nini waachien trained professionals bwana sisi tuwe watazamaji tu wengine humu mnatiririka na huku hata airport hamjawah fika
 
Najifikirisha tu kuwa, yawezekana mpango maalumu wa kiroba cha unga 50-100Kgs kimeshushwa pale Arusha umekamilika.
 
Preta PakaJimmy Meljons LiverpoolFC

hebu tupeni mapya ya hapo uwanjani kama yapo kwa yeyote kati yenu aliyeko hapo uwanjani!

Mi nimetoka kikazi nje ya mkoa kidogo!

Wakuu, mimi nimepita na basi la Dodoma hapo maeneo ya Arusha Airport asubuhi hii majira ya saa 2 nikaliona hilo dege kwenye running track likionekana liko tayari kabisa kwa kuruka, kwa mwenye update ya kilichojiri huko nyuma hebu atujuze tafadhali?
 
Cc PakaJimmy Preta Meljons na huyu LiverpoolFC ila naona kama thread hii hajaipost kbs na matukio kama haya hakosagi.
 
Kwa ufupi kabisa, departure ya ndege hiyo iko saa 4.30 asubuhi hii.

Ni kwamba ndege hiyo baada ya kutolewa ilifanyiwa uchunguzi wa kihandisi kila eneo ambalo lingeweza kupata madhara, zaidi ikiwa ni kwenye retractables, ambapo ilionekana kuwa haijapata madhara makubwa.

Mwisho wa yote ilifanyiwa engine running/testing, na ikapasi, hivyo kuwa tayari kwa kuondoka.
Asubuhi ya leo kabla ya kuondoka kwa ndege hiyo kuna mahojiano mafupi kati ya Wakaguzi wa TCAA na marubani, ambapo marubani hao wanatarajiwa kutoa maelezo ya kina juu ya hasa ninini kilitokea hadi wakaamua ku'land Arusha.

Baada ya maelezo hayo basi wakiridhiana watakuwa wanafanya pre-flights na kuondoka.

Wakazi wa Arusha wakae mkao wa 'presha' tena leo baada ya juzi wengine kulazwa...too bad ndege itapitia city centre.
 
asante kwa kutujuza!tunasubiria ikifanikiwa kuruka tuzidi kumshukuru mungu!ila mimi huwa najiulizaga maswali jamani hadi naona saa nyingine kuna watu wanafanyaga makosa makusudi aidha kwa kutumwa au kwa kuamua tu ilimradi kuharibia wengine kazi!huyo mwongoza ndege wa KIA ,yaani utashangaa kosa afanye yeye halafu usikie waziri husika ajiuzulu!hivi jamani hawa mawaziri wanabeba vichwa vingapi vya wafanyakakzi walio chini yao?je hakuna uwezekano wa watu kutumika kuchafua majina ya watu hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi?huyo mwongoza ndege mzembe achukuliwe hatua kali mara moja!
Kwa ufupi kabisa, departure ya ndege hiyo iko saa 4.30 asubuhi hii.

Ni kwamba ndege hiyo baada ya kutolewa ilifanyiwa uchunguzi wa kihandisi kila eneo ambalo lingeweza kupata madhara, zaidi ikiwa ni kwenye retractables, ambapo ilionekana kuwa haijapata madhara makubwa.

Mwisho wa yote ilifanyiwa engine running/testing, na ikapasi, hivyo kuwa tayari kwa kuondoka.
Asubuhi ya leo kabla ya kuondoka kwa ndege hiyo kuna mahojiano mafupi kati ya Wakaguzi wa TCAA na marubani, ambapo marubani hao wanatarajiwa kutoa maelezo ya kina juu ya hasa ninini kilitokea hadi wakaamua ku'land Arusha.

Baada ya maelezo hayo basi wakiridhiana watakuwa wanafanya pre-flights na kuondoka.

Wakazi wa Arusha wakae mkao wa 'presha' tena leo baada ya juzi wengine kulazwa...too bad ndege itapitia city centre.
 
Naomba niwatoe wasiwasi wale wote wenye kujiuliza kuhusu uwezekano wa ndege hii kupaa kutumia mita 1600.

Ni kwamba marubani wa Kihabeshi wa ndege hii wala hawaongelei kabisa suala la distance hiyo kuwa fupi, wala hawajajaribu kuzungumzia. Wanachojua wao ni kwamba ndege yao ni STOL(short takeOff and Landing) system, hivyo wao wanawashangaa ninyi raia mnaobishania na kujiuliza suala hilo.

Wanasema kuwa kwao kuna viwanja vifuppi na vyenye height kubwa zaidi kutoka usawa wa bahari, lakini wanaoperate bila shida!
Arusha iko futi 4550 amsl, wakati kwao kuna hadi viwanja viko 8000+ amsl, na vifupi kama Arusha, lakini wanatua na kuondoka.

Kwahiyo tuachane na suala la kujiuliza kuhusu possibility ya kunyanyuka.
 
Naomba niwatoe wasiwasi wale wote wenye kujiuliza kuhusu uwezekano wa ndege hii kupaa kutumia mita 1600.

Ni kwamba marubani wa Kihabeshi wa ndege hii wala hawaongelei kabisa suala la distance hiyo kuwa fupi, wala hawajajaribu kuzungumzia. Wanachojua wao ni kwamba ndege yao ni STOL(short takeOff and Landing) system, hivyo wao wanawashangaa ninyi raia mnaobishania na kujiuliza suala hilo.

Wanasema kuwa kwao kuna viwanja vifuppi na vyenye height kubwa zaidi kutoka usawa wa bahari, lakini wanaoperate bila shida!
Arusha iko meta 4550 amsl, wakati kwao kuna hadi viwanja viko 8000+ amsl, na vifupi kama Arusha, lakini wanatua na kuondoka.

Kwahiyo tuachane na suala la kujiuliza kuhusu possibility ya kunyanyuka.

......No! ni futi 1387 amsl!
 
Niko hapa kwenye fensi ya Kisongo Airport, hakika kumejaa kumefurika.

Watu ni wengi sana kutoka kila kona ya mji!...si waswahili wazungu wahindi, wote wapo hapa kujionea jinsi ndege hiyo itakavyoruka.

Kuna waandishi wa BBC hapa na mitambo yao ya ajabuajabu, wakiwa wameitega ili kunasa hadi milimita ya kwanza ya muondoko, na wanasema kila kinachonaswa na wao kinaingia moja kwa moja pale London.
Kuna waandishi wa habari wa magazeti yote, TV zote na redio zote!

Eneo hili la kiwanja sasa hivi limekuwa na kituo maalum cha mabasi na teksi, bajaji, bodaboda na baiskeli kwaajili ya kufacilitate watazamaji wa sinema ya bure!

Kuna wachangamkiaji wa biashara wameweka kila aina za vinywaji na vitafunwa, na wanauza mpaka basi.

Kama ndege hii itafanikiwa kuondoka basi itakuwa ni kilio kwa wajasiriamali wengi!
 
Kwa umati unaouelezea, likigoma kuinuka si itakuwa habari kubwa tena? Anyways, tuwaachie professionals watuondolee hilo dege lao liende salama.....
 
Back
Top Bottom