Ndege yageuza baada ya abiria kupata ugonjwa wa kuhara

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,107
49,809
Ndege yageuza baada ya Abiria mmjawapo kupata ugonjwa wa tumbo na kuanza Kujiharishia kwenye ndege 🤣🤣🤣

My Take
Nilijuaga wanaokula Kula Hovyo ni Waafrika tuu na kwamba mambo haya hutokea kwenye Mabasi pekee kumbe Hadi Kwa Wazungu

----
Ndege ya Delta Airlines kutoka Atlanta kwenda Barcelona imelazimika kugeuka baada ya abiria mmoja kupata ugonjwa wa kuharisha na kusababisha harufu mbaya iliyotanda ndani ya ndege.

Ndege hiyo DL194 ilikuwa tayari imeondoka Georgia siku ya Ijumaa saa 2:47 usiku, kulingana na sauti zilizorekodiwa kati ya rubani na mamlaka ya udhibiti wa anga, rubani aliomba kugeuka saa mbili tu baada ya kuruka katika safari ya saa nane kuelekea Uhispania.

Kwenye rekodi, rubani aliiambia mamlaka ya udhibiti wa anga, "hili ni suala la hatari ya kibiolojia. Tumekuwa na abiria ambaye amekuwa na ugonjwa wa kuhara kwenye ndege, kwa hivyo wanataka turudi Atlanta," alisema rubani.

Kwa bahati nzuri, ndege hiyo ilisafishwa vizuri na iliweza kukamilisha safari yake siku iliyofuata.
 
Ni kupotezea watu muda jamani kwanini ndege igeuze? Kuharisha tu???
Wangemsogeza karibu na choo akamalize shida zake, ajisafishe na kubadilisha nguo.
Wafanyakazi wa ndege nao wasafishe mahali palipo chafuka.
Ndege sio kama treni.choo chake watu huwa wanaingia kwa shida ndogo ndogo sio kuharisha.na harufu ya uharo inaweza ikamaliza oxygen yote ambayo imeshapimwa kabla ya ndege kuruka.Ni lazima wamshushe karibu iwezekanapo.
 
Ndege sio kama treni.choo chake watu huwa wanaingia kwa shida ndogo ndogo sio kuharisha.na harufu ya uharo inaweza ikamaliza oxygen yote ambayo imeshapimwa kabla ya ndege kuruka.Ni lazima wamshushe karibu iwezekanapo.
Walitakiwa wafikirie cases kama hizo ikitokea inakuaje, ni kupotezena muda bana.
Nilishawahi shuhudia mtu akijinyea kwenye bus, ilikuwa balaa😀😀. Gari ilisimama akashuka kwenda kujisafisha, zile nguo akaziacha porini akavaa nguo nyingine. Kimbembe ni harufu iliyobaki ndani ya bus, watu walitoa perfumes zao kupulizia lkn wapi, harufu ipo pale pale😅😅😅, tulivumilia na safari iliendelea. Nilimuonea huruma sana yule jamaa.
 
Hiyo ndege haikuwa na choo ndani yake, huduma ya kwanza nayo haikuwepo kiasi cha kugeuza? Duh! Huyo abiria alikula vyakula gani wakati tunajua vyakula vya kizungu ni visafi na si vigumugumu kama vyetu ukiacha chipsi mayai na uji
 
Hiyo ndege haikuwa na choo ndani yake, huduma ya kwanza nayo haikuwepo kiasi cha kugeuza? Duh! Huyo abiria alikula vyakula gani wakati tunajua vyakula vya kizungu ni visafi na si vigumugumu kama vyetu ukiacha chipsi mayai na uji
Mtu anaweza kupoteza maisha kwa kuhara, Kongole kwa rubani kwa ungwana.
Food poisoning inatokea kwa mtu yoyote na usafi wa chakula hauonekani kwa macho.
 
Mbona ndege zote zina vyoo ndani si angepelekwa huko kufanyiwa usafi then safari iendelee?
Vinginevyo ndege ziwe na vyumba vya Emergency vya kutoa First Aid kwa abiri wanaopatwa na changamoto hizo!
 
Back
Top Bottom