ESTIM Construction ni kampuni ya nchi gani?

ESTIM Construction ni kampuni ya nchi gani?

Mkuu hizo gharama unazitoa wapi. Pia estim ni contractor wa pili baada ya wa kwanza kufukuzwa.

Du....kweli eewe ndio hujui kitu.
Mchina hakutia mguu mradi wa Msata Bagamoyo.
Kazi ilikuwa estim mwanzo mwisho, tena kwa gharama za kutisha Tshs 2bn kwa kilometa!
Ulizia Tanroads upate facts.
Hapa si chit chat.
 
Kwa kweli nami nawawakubali wamejenga mitaa ya makumbusho Barbara zimetulia. Njoo Sasa hawa delmonte na can...wamejenga Barbara ya mbweni isharudiwa Mara mbili wapi, Makonda alikuja na mkwala wa kuzifungia akafeli, sijui alipewa Mambo ya fedha akanyamaza ama vipi
 
Katika uchunguzi wangu wa miradi ya barabara nimegundua kampuni inayojulikana kama ESTIM inajenga barabara zenye ubora wa hali ya juu sana. Cha ajabu zaidi hawa ESTIM wapo vizuri sana kwenye madaraja na majengo hasa yale makubwa.

Kuna picha nimeona wanavyo jenga barabara ya Kimara kibaha kule Dar es salaam. Kilicho nivutia ni jinsi wanavyo jali mazingira kuhakikisha kwamba sehemu ambazo wameharibu uoto wakati wanajenga wanajitahidi kurudiashia uoto huo kwa kupanda nyasi na miti hata kabla barabar haijaisha kitu ambacho sinakiona kwa kampuni nyingi za kichina.

Jambo kama hilo limeonekana hasa kwa wale jamaa wanaojenga SGR pekee.

Pamoja na hayo yote hawa jamaa wanaonekana kuleta namna mpya ya ujenzi wa barabara zenye quality.

Baadhi ya barabara niliwahi kuipita ni ile ya goba jijini dar es salaam sijui kwa sasa kama bado nzima lakink kwa ujenzi ule naamini hadi sasa itakua bado imara.

Kuna wachina walipewa kujenga barabara ya bagamoyo msata, nasikia waliopoona lile bonde walikimbia , nasikia kazi iliyo fanywa na ESTIM ya kujenga badaraja katika bonde lile ni ya kutukuka.

Sijajua kampuni hii inatoka nchi gani lakini serikali inahitaji kuitambua kwa mchango wake.

Mapendekezo

Kwenye issue za madaraja waachiwe hawa jamaa.

Barabara za magari makubwa waachiwe hawa jamaa.

Majengo ya taasisi kama vyuo etc waachiwe hawa jamaa.

Nasema kutoka moyoni, sijawahi kusikia kashfa ya kazi mbovu toka hii kampuni.

Kama ipo ni ya bahati mbaya.View attachment 1118532
Ndio wameshusha ile kitu moroccco square.
Kitu kimesimama hatari
 
Una akili mbovu sana, sema umeingilia fani isio yako. Ninapokuona juha ni kuwa hata Estim hujui ni ya wapi, na umekuja na unaa kama sio sifa za kuipigia debe. Kuanzia lini wewe ukasema Estim ndio inatakiwa iachiwe Kazi za madaraja, Kazi za majengo na barabara kampuni zingine zitafanya nini? Umekuja na hoja mufilisi kabisa eti wachina walikimbia ujenzi wa bagamoyo-msata, wakafanya Estim, umezidi kujichanganya kwamba umetumwa.
Sasa kwa taarifa yako ni ujenzi wa Kawaida sana kutokana na aina ya ujenzi wa barabara uwe na Kiwango gani. Barabara zina madaraja matano, earth road, gravel road, single surface dressing na double, la mwisho ndio premix ndio hizo wanajenga hao wanaume wako. Zitatofautia layer to za ujenzi basi kwa ajili ya kuhimili uzito tofauti tofauti.
Kwa taarifa yako ni kampuni ya hapa Tanzania, ikiwa kampuni tanzu ya Caspian.
Ili kukuweka wazi kuna kampuni kubwa zenye level moja na hiyo na zinafanya Kazi iliyotukuka sana.
Mtu wa muhimu kuhakikisha ujenzi unakuwa wa Kiwango ni specification za kwenye mkataba, na usimamizi na ukaguzi wa client na consultant.
Wafanye stage zote za ukaguzi, kabla, wakati na mwisho.
Pole na hongera kwa kuongea hisia zako hadharani.
Wewe ndio Eng. mzawa ee? Au nyie ndio maEng wa mkoa?
Wajinga kabisa.

Tanlalila nyiiiiingi. Kazi ziro.

Huyu jamaa alichokiongea kina ukweli kwa mwananchi wa kawaida regardless na elimu zenu sijui madaraja chini sijui earth road,gravel road sijui double.hayo mtajua nyie.

Kwanza tubie kwa nini mliruhusu kupitisha BRT pale jangwani bila daraja?
Jibu hilo swali.
Unavyojifanya kumpinga mleta mada unatupigia tu makelele kwa sababu hata sisi tunaona
 
Mkuu hizo gharama unazitoa wapi. Pia estim ni contractor wa pili baada ya wa kwanza kufukuzwa.

Umesema alikuwepo mchina , tupe jina.
Ya TAKOPA tunayakumbuka fika.
Gharama ulizo refer ni pamoja na madaraja matatu pale mto Ruvu?
 
Kwa uzoefu wako kama mhandisi mzawa unadhani ile kazi iliyofanyika pale kwenye lile bonde ni ya kitoto?
Umesema alikuwepo mchina , tupe jina.
Ya TAKOPA tunayakumbuka fika.
Gharama ulizo refer ni pamoja na madaraja matatu pale mto Ruvu?
 
Estim wako vizuri sana.... na kinacho nifurahisha hawa jamaa wana vitendea kazi maana hata kama mtu si mtaalam unaona wazi hapa kuna muelekeo mzuri kabisa.
 
Una akili mbovu sana, sema umeingilia fani isio yako. Ninapokuona juha ni kuwa hata Estim hujui ni ya wapi, na umekuja na unaa kama sio sifa za kuipigia debe. Kuanzia lini wewe ukasema Estim ndio inatakiwa iachiwe Kazi za madaraja, Kazi za majengo na barabara kampuni zingine zitafanya nini? Umekuja na hoja mufilisi kabisa eti wachina walikimbia ujenzi wa bagamoyo-msata, wakafanya Estim, umezidi kujichanganya kwamba umetumwa.
Sasa kwa taarifa yako ni ujenzi wa Kawaida sana kutokana na aina ya ujenzi wa barabara uwe na Kiwango gani. Barabara zina madaraja matano, earth road, gravel road, single surface dressing na double, la mwisho ndio premix ndio hizo wanajenga hao wanaume wako. Zitatofautia layer to za ujenzi basi kwa ajili ya kuhimili uzito tofauti tofauti.
Kwa taarifa yako ni kampuni ya hapa Tanzania, ikiwa kampuni tanzu ya Caspian.
Ili kukuweka wazi kuna kampuni kubwa zenye level moja na hiyo na zinafanya Kazi iliyotukuka sana.
Mtu wa muhimu kuhakikisha ujenzi unakuwa wa Kiwango ni specification za kwenye mkataba, na usimamizi na ukaguzi wa client na consultant.
Wafanye stage zote za ukaguzi, kabla, wakati na mwisho.
Pole na hongera kwa kuongea hisia zako hadharani.
Taratibu muzee bado tuko Eid pili.
 
Ni kampuni inayomilikiwa na mtanzania mwenye asili ya Uhindini (Uraia wa kusajiliwa)

Hivyo kuiwezesha kusajiliwa kama kampuni ya kizawa

Ni kampuni daraja la kwanza (1) kwenye majengo na uhandisi wa miundombinu jamii.
Uraia wa kusajiliwa ndiyo wa aina gani mkuu? Hapa nimetoka kapa mkuu😀
 
Wanachonikera hawa jamaa wanaojenga barabara ya Kimara ni kutokuwa na utaratibu wa kuweka njia mbadala ili kusiwe na msongamano. tunajua kwamba eneo hilo kuna nyumba nyingi zimebomolewa ili kupisha ujenzi wa barabara na kwa hiyo kuna nafasi kubwa sana ya kuweka njia mbadala. kuna viwanja viwili vya mpira hapo katika upana wa barabara. Sasa badala ya kujenga service road za uhakika ili kusiwe na msongamano, tumeshuhudia misururu mirefu ya magari hivi karibuni kutokana na style wanayotumia kujenga ambayo siyo rafiki kwa barabara yenye watumiaji wengi kama ilivyo morogoro road. yaani kwa hilo hawa jamaa MIMI NAWALAANI KABISA WAKAFILIE MBALI
 
Picha ya huko kimara hadi kibaha wanapojenga hio barabara ipo wapi? Na ya hayo majengo?
Kwani upo kipori mkubwa nenda mbezi mwisho kuelekea kibamba utaona picha zitakudanganya
 
Barabara yote ya zamani bado ipo labda sema kuna eneo ambalo rafiki yangu siku moja amekaa karibia saa 1 ambalo ni mbezi darajani ikitokea kibanda cha mkaa.

Back
Top Bottom