Katika uchunguzi wangu wa miradi ya barabara nimegundua kampuni inayojulikana kama ESTIM inajenga barabara zenye ubora wa hali ya juu sana. Cha ajabu zaidi hawa ESTIM wapo vizuri sana kwenye madaraja na majengo hasa yale makubwa.
Kuna picha nimeona wanavyo jenga barabara ya Kimara kibaha kule Dar es salaam. Kilicho nivutia ni jinsi wanavyo jali mazingira kuhakikisha kwamba sehemu ambazo wameharibu uoto wakati wanajenga wanajitahidi kurudiashia uoto huo kwa kupanda nyasi na miti hata kabla barabara haijaisha kitu ambacho sijakiona kwa kampuni nyingi za kichina.
Jambo kama hilo limeonekana hasa kwa wale jamaa wanaojenga SGR pekee.
Pamoja na hayo yote hawa jamaa wanaonekana kuleta namna mpya ya ujenzi wa barabara zenye quality.
Baadhi ya barabara niliwahi kuipita ni ile ya Goba jijini Dar es salaam sijui kwa sasa kama bado nzima lakini kwa ujenzi ule naamini hadi sasa itakua bado imara.
Kuna wachina walipewa kujenga barabara ya Bagamoyo Msata, nasikia waliopoona lile bonde walikimbia, nasikia kazi iliyo fanywa na ESTIM ya kujenga Madaraja katika bonde lile ni ya kutukuka.
Sijajua kampuni hii inatoka nchi gani lakini serikali inahitaji kuitambua kwa mchango wake.
Mapendekezo
Kwenye issue za madaraja waachiwe hawa jamaa.
Barabara za magari makubwa waachiwe hawa jamaa.
Majengo ya taasisi kama vyuo etc waachiwe hawa jamaa.
Nasema kutoka moyoni, sijawahi kusikia kashfa ya kazi mbovu toka hii kampuni.
Kama ipo ni ya bahati mbaya.
View attachment 1118532