Esther Bulaya: Sirro arudishwe aje kupambana na hali yake!

Hawa kina Bulaya na wasaliti wenzake inaelekea sasa wataimaliza miaka yao mitano bungeni bila shida yoyote.

Maridhiano ilikuwa janja ya kisiasa kutuzubaisha tuone mama anatuunganisha, kumbe alikuwa anatukusanya vizuri ili tukishajaa kwenye mtego atulipue.

Ok, nikirudi kwenye hoja ya Bulaya anasema Sirro arudishwe aje kujibu tuhuma dhidi yake kuhusu bil 1 iliyopotea mikononi mwake, atuambie pia, yeye na wenzake 18 pale bungeni mpaka leo wameshakula kiasi gani cha pesa kama mishahara na posho zao? je, hiki kiasi hakijapotea mikononi mwao? hawastahili kuhojiwa kwa upotevu huo?

Kwa hali hiyo hapo juu, ajiulize kama yeye na wenzake wanayo credibility yoyote ya kuhoji juu ya upotevu wa pesa utakaofanywa na serikali ya CCM, ikiwa hata nao wanatumiwa na CCM hiyo hiyo kupoteza pesa za walipa kodi kule bungeni.
Hawa hawakujileta, hapo kuna mtu aliwaleta.
 
Sirro kama namuona anavyobana pumbu,usipime uambiwe ulipe 1 b ukizingatia alihonga mademu (labda)
 
Haiwezi ikawa Mshahara wa mtumishi aliyejitoa kwa jasho na damu kama Siro lazima kunawakati tuwe na shukrani tatizo wakati wanaopiga kelele wanalala na wanaowapenda yeye alikuwa ana kesha huku anaumiza kichwa ni namna gani hali ya utulivu na amani itamalaki.

Hivi mnajua tatizo LA Ugaidi lilitosha kuvuruga amani ya nchi hii?Hivi mnakumbuka ujambazi ulifikia kiwango ambacho wananchi walifikia hatua ya kuwa machawa wa majambazi maana kulikuwa hakuna njia ya kufanya chochote mpaka Mapolisi,Mahakimu na Majaji waliamua kuungana nao.

Mimi nadhani Serikali au MTU yeyote badala ya kufikiria mambo ya kumuathiri mwamba huyu wamlipe maana taasisi yake aliiongoza katika wakati mgumu bila kuwa na msaada kwakuwa ndiyo kipindi pekee ambacho Askari walinyimwa Vyeo,walinyimwa pesa za likizo,pesa za uhamisho magari yao mabovu hayakupewa mafuta ajira zilisitishwa lakini Mwamba hakulalamika ilibadili changamoto kuwa fursa.

Rafiki zangu wa Polisi niliwashangaa kwamba walikuwa hawaoni kama walikuwa wanatekeleza majukumu yao huku wakiwa wamefungwa kamba alafu wakawa wanalalamikiwa hadharani kwenye mikuno ya hadhara wakisimangwa nyuma ya microphone. Kumbuka siku mkuu mmoja alivyo mfokea boss wa Polisi eti kwanini anakamata bodaboda wasiovaa kofia nguma kama vile yeye ndiye mtunzi wa sheria,Wanasiasa wakajizolea sifa kwa kuwaumbua Polisi bila kuwapa haki yao ya kusikilizwa.
Sasa Awamu hii imewaheshimisha Polisi angalau naona wametolewa kwenye Siasa,vyeo wanapata pesa za madeni wanalipwa magari mapya kila kona tuendelee kuwatia moyo.
 
Ila sirro alikua mbabe hatari
Sirro ni mtoto wa Mjini,alivyokuwa Mkuu wa Upelelezi Magomeni wauza unga wote walikuwa wanaripoti kwake,ilikuwa ole wako Askari mdogo umkamate muuza unga Kinondoni au Magomeni fasta atapigiwa simu na kuingilia kati kuwasaidia wauza unga,hivyo ni mtoto wa Mjini haswa
 
Kijana gani utampa ubalozi? pad au ubalozi wa nchi? Wakina dulla makabila? Au diamond? Au jokate?

Sometimes kuna vitu kabla hamjaandika hata google kwanza. Ili thread hata ipate uzito mzee mwenzangu. Tafadhari.
Hili nalo ni tatizo kuwaza kuwa vijana hawana uwezo, kwanini Umewaza wasanii ambao hawana elimu ya kujitosheleza, tuna wahitimu wazuri sana katika kusimamia rasilmali za taifa washindwe nini, uzoefu unapatikanaje sasa, hapana wewe ndiyo hujawaza kimtazamo chanya tunataka vijana wagombanie fursa hizi ubalozi sio lazima awe mzee au wastaafu bali vijana tuna uwezo mkubwa sana, kama umeji underrate basi ni wewe
 
Salim Ahmed Salim alipata kuwa Balozi akiwa na miaka 22, vijana wapo tele wenye uwezo
 
Uwepo wao Bungeni usipoteze ukweli kuwa alichohoji kina umuhimu
Hawana moral authority kuhoji hayo, na hizo kelele bungeni tunaona ni maigizo tu. Anaotaka wamchukulie Sirro hatua, ndio wanaowafumbia macho wao kuendelea kuwa bungeni.
 
Back
Top Bottom