Mdee, Bulaya, Jacob, Kileo, Mwago na Asenga Wanashikiliwa Polisi Sitakishari, wadaiwa kufanya fujo Segerea

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,048
2,000
Habari wana Jamvi,

CHADEMA watangaza habari mbaya usiku huu.

NUKUU:-

CHADEMA wameongea na waandishi wa habari usiku huu kutoa taarifa kuhusu waliokamatwa leo wakati wameenda kumtoa Mwenyekiti Wao (Freeman Mbowe).

"Halima Mdee na Meya Jacob wamepigwa wameumizwa sana na wapo kituo cha polisi "STAKI SHARI", hajawapelekwa hospitali, askari wanasema wanasubiri maelekezo kutoka "JUU"."

"Esther Bulaya apigwa mpaka kupoteza fahamu (azimia) pamoja na Kileo hawajulikani walipo. Chadema yataka polisi wawapeleke hospitali haraka sana."


=====

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Zuberi Chembela amesema viongozi wa Chadema wanashikiliwa katika kituo cha polisi Stakishari kwa mahojiano kwa madai ya kufanya vurugu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Kati ya wanaoshikiliwa ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe; mbunge wa Bunda, Ester Bulaya; Meya wa Ubungo, Boniface Jacob; katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo; diwani wa Tabata, Patrick Asenga na mjumbe wa baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Hadija Mwago.

Wakati Chembela akieleza hayo, naibu katibu mkuu wa Chadema (Bara), Benson Kigaila amelieleza Mwananchi leo kuwa takribani wanachama 16 wanashikiliwa na polisi.

Katika ufafanuzi wake Chembela amesema watuhumiwa hao walikwenda katika gereza la Segerea na kukuta geti limefungwa lakini walilazimisha kuingia ndani licha ya kuzuiwa na askari wa Jeshi la Magereza.

“Jambo hilo liliwafanya askari Magereza kuwadhibiti, kuwaweka chini ya ulinzi na waliwafikisha kituo cha polisi Stakishari ambako wapo wanahojiwa,” amesema Chembela.

Amebainisha kuwa dhamana kwa viongozi hao waliokwenda katika gereza hilo kumchukua mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyetoka jela baada ya kulipa faini ya Sh70 milioni, ipo wazi endapo watatimiza masharti.

“Wananchi wawe watulivu kwa amri halali zinazotolewa na vyombo vya ulinzi na usalama. Si jambo la kiungwana umekuta geti limefungwa halafu badala ya kupiga hodi unalazimisha kupita. Hata wewe ingekuwa kwako ungekubali.” Amehoji.

Katika maelezo yake Kigaila amedai, “Mbali na wanachama 16 kukamatwa wengine wanne wameumizwa baada ya kuibuka mvutano kati yao na askari Magereza.”

Hadi leo saa 1:00 ushiku viongozi hao pamoja na wanachama wengine walikuwa wakiendelea kuhojiwa katika kituo cha Polisi Stakishari.
 

Arushaone

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
14,930
2,000
Hizo nchi mnazosikia zina vita vya wenyewe kwa wenyewe zilianza hivi hivi.
Huu uonevu mpaka lini?
Kwanini nchi haina wazee wa kuwakemea watawala wanapokosea?

Haya mambo yataendelea hivi mpaka lini?

Wanadhani wanajifurahisha ila wanalea mimba na kitakachozaliwa kitawamaliza wengi.

Wakati ni sasa wa kujisahihisha before it is too late.

Mungu ibariki Tanzania.
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
127,681
2,000
Na nyie sasa dah!

Mtalia lia mpaka lini?

Mtaonewa onewa mpaka lini?

Mtaandika andika mitandaoni humu mpaka lini?

Mnajua awamu hii ilivyo, mbona mikakati na harakati zenu hazibadiliki?

Mnahitaji mikakati mipya na harakati mpya zinazoendana sawia na ngoma inayopigwa na awamu hii mpya. Wakipiga rege nanyi chezeni rege siyo wanapiga rege nyie mmekazana na mdundiko wenu miaka nenda miaka rudi....Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nima Imma

JF-Expert Member
May 14, 2015
2,324
2,000
Hatukawii kusikia taarifa za vifo au watu kupewa ulemavu kesho asubuhi. Kwa hii hali tanzania tumefikia pabaya sana.

Watanzania tunaishi kwa "UADUI BAINA YETU SISI KWA SISI". Hatari sana.
Kuna muda natamani nipate nguvu ya kuwaza a mengineyo ila yangu tu yananilemea basi mengine nasoma na kuyavuka
Ila mengine yanafikirisha
Hivi haya maisha ya mbio mbio hivi mpaka lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Abdalla mpemba

JF-Expert Member
Dec 31, 2016
484
1,000
Hizo nchi mnazosikia zina vita vya wenyewe kwa wenyewe zilianza hivi hivi.
Huu uonevu mpaka lini?
Kwanini nchi haina wazee wa kuwakemea watawala wanapokosea?

Haya mambo yataendelea hivi mpaka lini?

Wanadhani wanajifurahisha ila wanalea mimba na kitakachozaliwa kitawamaliza wengi.

Wakati ni sasa wa kujisahihisha before it is too late.

Mungu ibariki Tanzania.
Kila mzee usifikirie anabusara

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
706
1,000
Jee mnahakika huyo anayewaagiza hayo ni rafiki kweli wa jamii yenu? Akili zenu zinafanya kazi au ni just like machine tuu?
Wabunge kama Halima na Bulaya wakiwa na viongozi wengine wanaenda kumpokea kiongozi wao mkuu toka gerezani kitu gani kinawafanya muwakamate kuwapiga na kuwadhalilisha?
Mbona juzi Polepole na magari yao wameingia hadi ndani kutaka kumteka Msigwa na hakuna lililofanyika?
Hamjui mna karibisha balaa katika familia zenu? Ona sasa katika mitandao jina la askari aliye mpiga mtama Bulaya hadi kuzimia linatangazwa huku ikielezwa mkewe anapatikana gereza LA Keko eneo gani analo uza chapati. Jee hapo hajahatarisha maisha ya mkewe na watoto?
Polisi nao huko Sitaki Shari wanawatendea wabunge hao waliopigania huduma bora za nyumba, posho na uniform kama adui zao jee hiyo nayo akili?
Mnajazwa uccm vichwani hadi hamjitambui ndio maana mnajikuta mnaitwa div 4 failure!
Jipimeni kama mnastahili kuendelea kuhesabika kama MNA weledi.
Screenshot_20200314-015733.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
7,121
2,000
Hizo nchi mnazosikia zina vita vya wenyewe kwa wenyewe zilianza hivi hivi.
Huu uonevu mpaka lini?
Kwanini nchi haina wazee wa kuwakemea watawala wanapokosea?

Haya mambo yataendelea hivi mpaka lini?

Wanadhani wanajifurahisha ila wanalea mimba na kitakachozaliwa kitawamaliza wengi.

Wakati ni sasa wa kujisahihisha before it is too late.

Mungu ibariki Tanzania.
Kusema kweli kuna kipindi nilikuwa nawaunga mikono hawa wabunge. Ile kwa sasa wamenikinai, ubunge wanaupaka matope. Wao walikuwa ndan pia, mbona hatukusikia walikwenda kuwatoa wakipigwa au kalazwa rumande?
Watu wazima, hawana nidhamu, kila wanapokwenda ni vurugu kama wehu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom