Esoteric: Uhusiano wa Zitto, JK, Salim A.S, Ridhwan, Omar Ilyas & then some Islams?

Status
Not open for further replies.
Zitto, welcome back to JF, nakumbuka nilikusisitiza, wapiganaji shupavu, hawakimbii hoja kwa kukaa kimya, bali hujibu hoja kwa hoja, unless zikiwa ni za kipuuzi, zinapuuzwa.

Pia vile uliadimika kipindi kirefu, kuwa tayari kupokea makombora yoyote mazito toka kwa wana JF u prove them wewe sio Zitto jina tuu, pia ni Zitto kwenye kujibu hoja na usitukimbie tena, unless you are genuinely busy!.
 
''I have come to the conclusion that politics are too serious a matter to be left to the politicians''. Charles De Gaulle (1890 - 1970)
:redfaces:
 

Tumekuelewa, ila haya maneno yako yanahitaji kuyafanyia utafiti zaidi isije kuwa unamponda mtu humu JF kwa ww kujitafutia umaarufu au kumchafua mtu mbele ya jamiim na kwa mtu makini kama ZITTO
 
Waberoya na members, Zitto anaingia hapa ndani ya 2hrs kujibu kila tuhuma inayoelekezwa kwake na hata hii atatoa maelezo kwa kina. Naomba msiharibu mtiririko ili apate kujibu mmoja baada ya mwingine.

Ni kwa taarifa tu

Hajatuhumiwa aliyeandika hapa (mimi alikuwa anawaza) ila kama katika mawazo hayo kuna wa kusaidia ndiyo wajitokeze, I mean Zito atbaki kuwa zito ila kwa akili yangu ndogo sijaona urafiki wa nuru na giza lazima nuru itaonekana tu.

Anaweza kujibu kwa namna yoyote ile, yeye ni mwanasiasa na akae akijua tuko pamoja ila hili la juzi limenishtua sana, mwanasiasa nguli kama yeye hawezi kamwe kusema JK amepeleka maendeleo kigoma, that mean viongozi wa leo kututumikia ni options.

anyway karibu zito tuondolee hofu hii!!


Pasco kaka!

tangu nimejiunga JF miaka 3 iliyopita sijawahi kuandika negative kuhusu Zitto, mpaka kwenye dowans nilikuwa upande wake!! I believe and I fully agree kila neno hapo juu.

Pasco we need strong and good leaders (kama ulivyosema akina Omar Lyas) yes kama Ommy ana sifa hizo then ni nzuri sana kwa taifa hili, lakini hujasema kuwa anatuhumiwa kuhusu udini. Na unasahu kuwa viongozi wazuri wanaweza kuwa na kasoro ambayo inafuta uzuri wote, hukulia mfano wa Lowasa, ni mchapakazi lakini ana-tamaa kuliko mwewe anayeuona mzoga!!

Ugonjwa na kansa kubwa kabisa ya viongozi wa dunia ya tatu ni kujiona miungu watu na kamwe sio watumishi wa wananchi. Zitto anataka kuuaminisha umma kuwa JK kupeleka maendeleo kigoma ulikuwa ni msaada tu na sio wajibu wake kama rais??? sijajua Kigoma ya zitto imeendelea mpaka wapi! LMAO!

Huyo great thinker ambaye ameisha-sink kwenye mawazo ya kutu kama haya sio mzuri kabisa, na sikutegemea mtu wa aina yake aseme hivyo. Achilia mbali sifa zote alizonazo, yes, ndiyo kila aina ya sifa nzuri ulizozisema. 'powers from within' lazima iwe sensible , hawa CCM walafi, wezi, akina mama zetu wanakufa mahospitalini, EPA, RICH, n.k siasa za Tanzania hazitakiwi kuwa hapo unapotaka ziwepo..eti..urafiki wa kisiasa.

CCM ndiyo wametufikisha hapa tulipo, katiba yetu ina viraka na ina accomodate only one party, NEC ndiyo hiyo tena, hivi urafiki huu unaousema ni upi hasa? Maalim angekuwa mpole uko visiwani leo hii kungekuwa na serikali ya mseto??

Zitto anapaswa kuwa pamoja na wenzake kwenye mabadiliko ya katiba, kama yeye ni chadema basi aishi, ale,anywe, aongee kama chama, sisi ARSENAL ...I mean Simba ndiyo tunaishi hivyo.

Kauli yake ya juzi inafuta kabisa sifa nzuri zote ulizompa, ndiye yeye zito nilimtania na kusema unavyomsifia sana Mwakyembe mtasimamisha mgombea wa chadema huko Kyela? unajua kilichotokea.

Hakuna na usiwepo urafiki wowote wa CCM na mwanachadema, maana CCM sio watanzania, ni wakoloni, ni wanzungu weusi, akina mwakyembe wako wapi , juzi umesikia akisema lolote kuhusu Sita? nataka nijue Pasco urafiki unaousema ni upi kati ya mafisadi na wasio mafisadi??

Huku kwetu kariakoo mwizi tunamchoma moto!!! tena aliyeiba tu sh.1000 unataka kusema wezi wa aina ya JK wachekewe na kukumbatiwa, thenif that so then Zitto hafai!

Mtafute mtu wa aina ya Zitto zimbabwe(professor Moyo )http://en.wikipedia.org/wiki/Jonathan_Moyo; uone alifanya nini na ujue ndiye chanzo cha matatizo ya Zimbabwe ni yeye.

Hakuna siasa za urafiki na kama zipo ndio nimeuliza, mwishoni kwa kiasi gani tunawaamini wanasiasa hawa? then kwa sentensi yako wanayoyafanya akina Lyatonga Mrema ni ''urafiki wa kisiasa''!!!!

Then we should all be CCM, maana mbona ndani ya ccm wanakosoana sana tena kuliko wapinzani wanavyoikosoa CCM

Zito should change or quit! urafiki wake na JK, Ridhwan, unatutia shaka yakhe!
 
duh, mnyonge anyongwe ila haki apewe. Marehemu mkili afufuke leo na aje ayasome haya.duh, haya bwana

Zitto wewe ni mwanasiasa Mkomavu, lakini ukianza kuongelea impossibles utajishushia heshima yako,
hapo kuna hoja , basi cha muhimu ni kujibu hizo hoja, lakini ukianza kujitambilisha wewe ni mnyonge na unaonewa mara Mkili afufuke na ni kitu ambacho hakiwezekani,

naomba uwe na nguvu kama ile uliyokuwa nayo pale TBC1
 
zito tunakusubiri mkuu wetu......!

pangua hoja KWA HOJA.......!kuliko kusema mnyonge mnyongeni
 
Jamani tupotelezee the main issue... Kwa kuchanganya udini hapa lets talk the main issue; mfano zitto kuongea na vyombo vya habari kuweka wazi yaliyotokea ndani ya chama... What this good for chadema, honestly what good did it do; hata kama angetaka vyombo vya habari vijue kwamba hakukubaliana na mawazo ya wengi kwenye chama.. angewatonya media kisirisiri sio mpaka awape ammunition
 
Pasco, mie ni mwana JF mwasisi na mwandamizi. Sikukimbia nilikaa kimya ili kupisha Zitto haters waseme wapendavyo. Mara chache niliingia. Waberoya kaleta hoja muhimu yenye kunihusisha na mentors wangu kama dr. Salim na pia rafiki zangu wa karibu kama Omar.

Kwa kupotosha kaweka element ya udini na hata kutosema rafiki zangu kama imma mvula, alberto msando na karuti bugwema ambao ni wakristo. Pia aliyekuwa girlfriend wangu Mary. Hawa wote walihusika mapinduzi asemayo. Hawataji. Anapotosha. Anataka niöekane mdini. Namheshimu Waberoya. Huwa objective. Ndio mana nataka kujadiliana naye na tufikie mwafaka wa ukweli na uwongo.
 
Umefanya vizuri kufahamisha umma kuhusu zito, hata wakati aliruhusu mitambo mibovu ya dowans itumike kuzalisha umeme na kupingana na dr.harrison ndio tukawa na wasiwasi nae nafikiri hata waheshimiwa wanamtambua kuwa ni mwenzao ktk kumtumia kuivuruga chadema inasikitisha sana.

Kuna kipindi alitaka kugombania uongozi na mh. Mbowe wazee chadema wakamstopisha je walishaona madhara yake? Je wale wabunge waliokosekana wakati chadema wanagomea hotuba ya kikwete wapo pamoja nae kimtazamo? Je kafulila na yule mama aliyehamia nccr wapo pamoja nae kimtazamo? Kwahali hii viongozi wapinzani wa kweli tanzania ni wachache sana asilimia kubwa ya viongozi wapinzani wapo kwa maslahi yao binafsi na ya CCM
 

Kaka umeongea na kumaliza yote ambayo nilikuwa nawaza... people please mada ya kuongelewa ipo hapa na tusipoteze thread kwenda kwenye udini cha kujibu kipo hapa.. Zitto ulikuwa hero wa watanzania please dont spoil it
 

- Ni kweli wewe ni M-DINI?
- Kama "mentor" wako ni mwanachama wa CCM nguli, je inawezekana wewe unafuata falsafa ya CCM ukiwa ndani ya CHADEMA?
- Ni kweli Kikwete ameleta maendeloe Kigoma?
 
Hii ndio gharama ya kufanya kazi na wakristo wa nchi hii. Nani alihoji dini ya Zitto alipokwenda Kibaha, Musoma, Rukwa na kwingineko kuwapa nguvu wagombea wa Chadema. Mtafanyakazi vizuri kwa muda mrefu, utakuwa mzalendo sana lakini siku mkitofautiana ataanza kufuatilia dini yako. Nilijua kuna siku dini ya Zitto litakuwa issue humu na hata Chadema.

Si ajabu siku moja watu wakaanza kuhoji dini ya Twaha Khalfan (Jenerali Ulimwengu) au Issa Shivji.

Wewe mtoa mada unachuki na waislam na zipo post zako tulizokujibu kwa udini wako. Jambo moja mtambuwe wakristo wa nchii ni kuwa equation inabadilika; huu si wakati ambao wazee wetu akina Mwakawago (RIP) ilibidi wafiche utambulisho wa dini zao kwa kuhofia dhulma ya waliokuwa mamlakani.

Mnakotupeleka siko lakini fahamuni mmeshatambulika na moto wake hamuwezi kuuzima ninyi watu mlikosa uzalendo!.

Zitto endelea na ufafanuzi wako lakini utambue hawa ndio wakristo wa nchi hii ambao utaendelea kushirikiana nao katika harakati zako za kisiasa.
 
Zitto anza na hoja moja kwanza urafiki wa kisiasa na mipaka yake afu pili taarifa ya TBC1 nyingine zifuate
 
nilisema a fraction ya yaliyotokea. Kuhusu kura tu na mie msimamo wangu ulikuwa wapi. Unataka niwe na msimamo kisha nifiche? Huo ni unafiki. Unataka niseme kisiri siri? Siwezi. Kulikuwa kuna ulazima? Ndio na hapana. Kisiasa hapana. Kisiasa za maadili na kuwa wakweli mbele ya umma na hasa jimbo la uchaguzi, ilikuwa lazima msimamo wa kila mmoja uwe wazi.
 
Jamani Tusipotoshe issue hapa.....ISSUE SIO UDINI AU SIO MTOA HOJA....... ISSUE NI ZITTO KABWE NA UPATRIOTIC WAKE NA UKWELI WAKE KWA CHADEMA NA WANANCHI
 
Ni mambo ya kawaida, mbona wenzetu wakipiga kura huwa inajulikana wazi kama Senator X ni Republican lakini amepiga kura ku support hoja ya Democrats.

Thats kawaida pipo
 
Acha post za chuki brother,ukisema "mnakotupeleka" una maana gani na kina nani?Zitto yupo hapa mwache ajibu hoja naamini zitto ni muungwana na pengine atafafanua zaidi. Udini ni element zilizoanza kupandikizwa na CCM na sasa naona mizizi inaanza kukua,watu mashuhuri kama kina zitto ndo wanaweza ku rectfy hali ya mambo!
 
duh, mnyonge anyongwe ila haki apewe. Marehemu mkili afufuke leo na aje ayasome haya.duh, haya bwana
Bwana Mheshimiwa, tunaomba majibu yenye akili na usitufanye sie mambumbu! Hii tabia ya kuanzisha vurumai chamani kwa vile una mambo yako binafsi unayoamini nathani si jambo jema na haswa la kwenda kutoa habari ya nini kilifanyika katika kukubaliana na azimio la chama! Ungeweza kunyamaza tu na kutoenda kutoa ushuhuda wako magazetini na kukidhuru chama chako namna hiyo ukizingatia ulienda kinyume na makubaliano ya kura! unajua jinsi ulivyoua hoja nzima ya mapambano ya katiba mpya? habari kujeuka kuwa mfarakano wa wana CHADEMA na sio bold move to walk out the President's parliament inaugral speech? mbona wenzio walikosa kuhudhuria hawajaongea na magazeti? Hivi wewe una ajenda gani na CHADEMA kuhusu demokrasia? Sie wewe uliyeshambuliwa katika matokeo ya Kigoma Mjini? Ulishambuliwa kwa sababu gani? Uchakachuaji sio? Sasa leo Chama chako kinasimama kidedea kulilia mabadiliko ya Katiba na tume huru wewe unawasaliti halafu unajisifu kwa ulilo fanya! ati maamuzi binafsi unajua philosophy ya teamwork? kama maamuzi binafsi si uwe na chama binafsi pia? kwa nini masuala ya chama yenye agenda ya ukombozi wa taifa hili unayaongelea kipingamizi? Aaah bwana huo si uungwana, kuna kitu unatafuta nakuheshimu ila natia shaka na motives zako... time will tell no wonder wazee waliogopa kukupa Uenyekiti kwa undumilakuwili ulionao si haba ukavunja chama wewe! si wa kuaminika! Your true colors zinaanza kuonekana baada ya gogoro la Kafulila sasa unaanzisha zengwe lingine! Na ulaaniwe usifikie malengo yako mabaya juu ya CHADEMA!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…