Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Mlaizer, unachanganya migomo miwili tofauti. Mgomo wa kwanza ni ule nitakaouita mgomo wa Mkili (Gervas) R.I.P. Huu Zitto alishiriki kikamilifu na baada ya hapo uchaguzi ulifanyika. Julius Rugemalira akawa Raisi, Flaviana Charles Makamu, Zitto Kabwe Katibu Mkuu, Albert Msando Speaker na Omar Ilyas Waziri wa Haki za Binadamu na wengineo.
Baada ya hapo uongozi wetu ukamaliza muda wake. Kayombo akachaguliwa Raisi na serikali yake. Ndio mgomo wa pili nitakaouita mgomo wa Kayombo ukafanyika. Mwanzoni haukuwa mgomo bali shinikizo la kutaka ajiuzulu kwa kushindwa kutatua matatizo ya wanafunzi haswa la hela za field kwa education nk. Ukafanyika mkutano Rev Square. Wanafunzi wakaenda Nkurumah Hall. Prof. Shivji alikuwa anafundisha Wanafunzi wa Sheria Mwaka wa pili. Akatupa mic na kutukabidhi hall. 'Uchaguzi' ukafanyika nikachaguliwa Raisi wa Muda na Siriwa Makamu wa Raisi. Kitu pekee kikubwa Zitto na Omar walichofanya ni kustrategize baada ya hayo kutokea na kushauri kutokurudi nyuma. Hawaku mastermind. Kama mgomo ule ulipangwa basi aliyepanga hakuwa Zitto wala Omar Ilyas. Ni kweli walisupport mapinduzi. Isingewezekana waache. Wao ni wanamapinduzi.
Nilijadiliana na Zitto kuhusu kuandika historia ya Daruso 1999 - 2004. Bado naamini ni muhimu ili tuwe na taarifa sahihi. Historia hiyo itasaidia kuonyesha viongozi wengi ni kina nani huko mbeleni.
Tuendelee kukumbushana.