Escrow: Stanbic Bank kuchafua hali ya hewa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Nimepenyezewa taarifa na mnene mmoja wa Stanbic kuwa Viongozi waandamizi wa Stanbic Bank huko majuu wanakaribia kuchafua tena hewa ya nchi.Waandamizi hao wameagiza kuanikwa kwa majina ya waliochota malumbesa ya fedha za Escrow. Wamewaagiza wakuu wa hapa Tanzania kuhakikisha ifikapo Aprili mosi mwaka huu,majina hayo yawe public pamoja na mihamala yao ili kusafisha taswira ya Stanbic.

Ukisikia kusafisha hapa na kuchafua pale ndio huku.Siombi hilo litokee.Hawa wa Mkombozi Bank aka wa Rugemalira wametuhenyesha hivi.Wa Stanbic itakuwaje? Stanbic Bank,please and please, re-think and re-decide. Tumechoka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Hapo kuna list ya ikulu sio mchezo

Hadi wale wa mil.80 hela ya matibabu
 
Kufufuliwa upya sasa kwa kesi ya Anglo leasing ya Kenya miaka zaidi ya kumi tokea ilipoamuliwa kesi ya msingi kunanipa matumaini kuwa haya yanayofukiwa kwenye hizi kesi za kifisadi kuna siku yatafunuliwa...

Amina
 
Nimepenyezewa taarifa na mnene mmoja wa Stanbic kuwa Viongozi waandamizi wa Stanbic Bank huko majuu wanakaribia kuchafua tena hewa ya nchi.Waandamizi hao wameagiza kuanikwa kwa majina ya waliochota malumbesa ya fedha za Escrow. Wamewaagiza wakuu wa hapa Tanzania kuhakikisha ifikapo Aprili mosi mwaka huu,majina hayo yawe public pamoja na mihamala yao ili kusafisha taswira ya Stanbic.

Ukisikia kusafisha hapa na kuchafua pale ndio huku.Siombi hilo litokee.Hawa wa Mkombozi Bank aka wa Rugemalira wametuhenyesha hivi.Wa Stanbic itakuwaje? Stanbic Bank,please and please, re-think and re-decide. Tumechoka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

ni muhimu itokee
 
Tujiandae kwa misiba ya viongozi, pressure haitawaacha!
 
Kutaja ni Muhimu na Kutotajwa ni fedhea pia kwa tuliowakabidhi Madaraka ya Kuingoza nchi huku Central Bank Ikiwa Chini yao.

Kutojulikana majina ya Waliochukua fedha Kupitia Stanbic ni Wazi kuwa Wahusika wakuu ni walio na dhamana kuu. Hivyo Watajwe ili Kujisafisha na Pia Kuisafisha Bank hii ya Stanbic.

Wajulikane ili Taifa lipone na nchi itulie kwa maana huko ndiko walikochota Miela ya Kufa mtu.
 
Tuliowatuma watu je majina yetu lkn hatukuenda cc inakuwaje
 
Nimepenyezewa taarifa na mnene mmoja wa Stanbic kuwa Viongozi waandamizi wa Stanbic Bank huko majuu wanakaribia kuchafua tena hewa ya nchi.Waandamizi hao wameagiza kuanikwa kwa majina ya waliochota malumbesa ya fedha za Escrow. Wamewaagiza wakuu wa hapa Tanzania kuhakikisha ifikapo Aprili mosi mwaka huu,majina hayo yawe public pamoja na mihamala yao ili kusafisha taswira ya Stanbic.

Ukisikia kusafisha hapa na kuchafua pale ndio huku.Siombi hilo litokee.Hawa wa Mkombozi Bank aka wa Rugemalira wametuhenyesha hivi.Wa Stanbic itakuwaje? Stanbic Bank,please and please, re-think and re-decide. Tumechoka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mmechoka?

mmechoka nini?

ina maana hamchoki kuchafua jina la biashara la Stanbic bank?
 
Tujiandae kwa misiba ya viongozi, pressure haitawaacha!

100% ni Kheri Wafe kwa Pressure Kwa maana Masikini Walalahoi Wanakufa kwa Mafua tu baada ya Kukosa hata Confline... Ebu na wafe wala hatutasikitika sana.
 
Back
Top Bottom