Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,915
Inasikitisha na kushangaza kuona nguvu kubwa inaelekezwa katika kusaka watumishi hewa na waliokula fedha hizo na huku wahusika wakiwa kimya kabisa kuhusu watu waliotuhumiwa kuchota mabilioni ya Escrow kupitia bank ya Stanbic kwa kutumia mifuko ya sandarusi kinyume kabisa na taratibu za kibenki!
Kinachonishangaza zaidi ni kuona maazimio ya Bunge teyari yalishawasikishwa serikalini lakini serikali inayojipambanua kupiga vita ufisadi ikiwa kimya kabisa kuhusu jambo hili alfu kila kukicha wanaimba wimbo wa kupambana na ufisadi na mafisadi.Sometimes huwa najiuliza nini hasa watu hawa wanachosimamia katika vita hii ya ufisadi.
Naanza pia kujiuliza hivi hii mahakama ya mafisadi itawahusu watu gani hasa kama hizi kashifa kubwa haziongelewi kabisa na hii serikali kama vile hazipo na hazijawahi hata kusikika.
Hivi tangu waingie madarakani ni lini mmewahi kuwasikia viongozi wa nchi hii wakitaja hadharani hizi kashifa kubwa kama vile ESCROW, EPA, RICHMOND, KAGODA,LUGUMI, n.k.Na kama hazitajwi,mahakama ya mafisadi inaundwa kwa lipi hasa?Tunachoshangilia kila siku ni nini hasa?Tunajitambua?Kama Taifa tunamjua aduai yetu kweli?Je,tumepagawa au tunasumbuliwa tu na mihemko ya kisiasa?