Equity Bank wanahujumu uchumi wetu

Equity Bank wanahujumu uchumi wetu

hoja zuri lakini haitapata watu wa kuchangia kwa sababu wachangia wa forum hii wanapenda kujadili watu badala ya issue

Sasa mbona wewe hujaijadili umeanza kulaumu watu?

Mfumo wa kutoa na kudai risiti TZ haupo vizuri kabisaa. Watu hatuna utamaduni wa kudai risiti na wafanya biashara hawana utamaduni wa kutoa risiti. Inahitajika elimu kwa pande zote kujua umuhimu wa risiti. Tumezoea magumashi tu
 
Wadau,

Ijulikane kuwa hata hizo Bureau de Change nao ni hivyo hivyo, risiti ni hadi uidai. Wenzetu Uganda hata ukiwa unauza dola ili upate shilingi yao lazima wadai passport na wajaze fomu kadhaa na kukupa risiti yako, yaani huhitaji kuuliza.

Nachotaka kusema ni kuwa hawa Equity Bank wanahujumu uchumi wetu, wanatorosha dola zetu kupeleka kwako na hivyo kusababisha kushuka na kuporomoka kwa shilingi yetu.

Watoroshaji Dollar wako kibao-mmoja wao ndiyo kama hayo Ma Bureau De Change.
Tatizo BOT msimamizi mkuu wa haya Mambo wako likizo siku nyingi.
 
BOT imebaki jina mambo ya msingi ya pesa wanajibu kisiasa ----- mtupu
 
pALE BENKI KUU WAMEJAZA WATOTO WAO TU
 
Acha mambo yako wewe kwanza equity bank wako vizuri sana mie nina akaunti yangu pale ya dola tena wako vizuri sana kwenye rate zao sio kama mabenki yetu hapa wanatudhulumu sana sasa ukienda crdb, nmb au nbc utaambiwa dola1=1700tsh badala ya 2000tsh, lakini equity wanawazidi hata hizo bureau de change kwa rate. Watu wengi siku hz wanaenda kubadilishia fedha zao equity kwa sababu hizo, na mie risiti huwa napewa!
Nafikiri wewe si Mtanzania. Suala ni kuwa hawatoi risiti ambalo ni takwa la kisheria wanapokuwa na kununua hizo dola. Pengine wanaweka bei kubwa unayoishangilia kwa sababu wanataka kununua dola zote na kuzitorosha kimagendo ndiyo maana hawatoi risiti.

Hata hivyo tatizo ni vyombo vyetu vya usimamizi, BOT kwa mabenki na hata TRA kwa wafanyabiashara. Ukipata huduma au kununua vitu kutoka kwa haya makampuni ya kigeni - ya kichina, kituruki, kihindi na hata kitanzania una pewa option ya ama kutoa fedha na kuchukua mzigo bila risiti au ukitaka risiti unatakiwa kuongeza fedha za kodi. Ukiwapa watu option hii ni dhairi hawatatoa fedha za kodi kwani badala ya Mfanyabiashara kulipa unamlipisha manunuzi tena kwa kumpa option ya kuweza kuacha kulipa!
 
Yan wanapobalidilisha pesa lazima wanapata mapato, kwa mfano, ukienda kununua dola moja utauziwa tsh 2050, ila ukienda kuuza dola moja watainunua kwa Tshs 1700, sasa haya mapato wanayopata wanatakiwa kulipia kodi, ndicho aliyomaanisha mtoa mada

Thank u hapo numekupata
 
Wadau,

Hata kama ni uwekezaji lazima ufuate sheria za nchi husika, lazima kuwe na win win situation.

Kwa bahati mbaya sivyo hivyo kwa haya mabenki ya nje yanayofurika nchini kila uchao, wanakuja kutuibia na kutuhujumu. Najiuliza, wanapata wapi ujasiri wa kukiuka masharti ya biashara na uwekezaji? Hivi ni kweli Benki Kuu haina mechanism ya kucheki kama haya mabenki yanafuata sheria za nchi.

Wiki tatu zilizopita nilienda Equity Bank pale Golden Jubilee kuchenji dola elfu mbili ili nipate shilingi niweze kufanya malipo mbali mbali ya kiofisi. Nilipofika Equity Bank nilielekezwa nipande ghorofani ambapo nilimpatia teller hizo dola ili anipe shilingi. Ajabu ni kuwa, nilipomwomba risiti akagoma ati hawatoagi risiti! Nikamwambia hicho kitu haiwezekani na hakipo, dada akasema ndivyo ilivyo na akamuuliza jirani yake ili nithibitishe, na mwenzake akanithibitishia! Ndipo nikawaambia wanirudishie dola zangu nikaenda kubadilishia Bureau de Change ambao baada ya kudai risiti walinipa.

Ijulikane kuwa hata hizo Bureau de Change nao ni hivyo hivyo, risiti ni hadi uidai. Wenzetu Uganda hata ukiwa unauza dola ili upate shilingi yao lazima wadai passport na wajaze fomu kadhaa na kukupa risiti yako, yaani huhitaji kuuliza.

Nachotaka kusema ni kuwa hawa Equity Bank wanahujumu uchumi wetu, wanatorosha dola zetu kupeleka kwako na hivyo kusababisha kushuka na kuporomoka kwa shilingi yetu.

Ndugu yangu iko hivi,
Tellers wanacheza deal, yaani unapoenda kuuza wanakupa kwa rate iliyopo tehn hawaziingizi kwenye system yaani hawapost na baada ya hapo wanawapigia wanunu ambao wanawauzia kwa bei ya juu. Hapo wanakuwa wamepata ile diff ndo pesa yao ya mfukoni.....pata picha watu wangapi wanaenda kubadirisha dola....ndo maana huwezi kupewa risti.
wakikupa risti ni lazima wapost kwenye system na hapo deal inakuwa imekufa.....
Equity kama taasisi hailijui hili coz linafanywa na wafanyakazi wa ngazi za chini so wakubwa hawajui. Hapa yatupasa kuhakikisha tunapewa risti...
 
Wadau,

Hata kama ni uwekezaji lazima ufuate sheria za nchi husika, lazima kuwe na win win situation.

Kwa bahati mbaya sivyo hivyo kwa haya mabenki ya nje yanayofurika nchini kila uchao, wanakuja kutuibia na kutuhujumu. Najiuliza, wanapata wapi ujasiri wa kukiuka masharti ya biashara na uwekezaji? Hivi ni kweli Benki Kuu haina mechanism ya kucheki kama haya mabenki yanafuata sheria za nchi.

Wiki tatu zilizopita nilienda Equity Bank pale Golden Jubilee kuchenji dola elfu mbili ili nipate shilingi niweze kufanya malipo mbali mbali ya kiofisi. Nilipofika Equity Bank nilielekezwa nipande ghorofani ambapo nilimpatia teller hizo dola ili anipe shilingi. Ajabu ni kuwa, nilipomwomba risiti akagoma ati hawatoagi risiti! Nikamwambia hicho kitu haiwezekani na hakipo, dada akasema ndivyo ilivyo na akamuuliza jirani yake ili nithibitishe, na mwenzake akanithibitishia! Ndipo nikawaambia wanirudishie dola zangu nikaenda kubadilishia Bureau de Change ambao baada ya kudai risiti walinipa.

Ijulikane kuwa hata hizo Bureau de Change nao ni hivyo hivyo, risiti ni hadi uidai. Wenzetu Uganda hata ukiwa unauza dola ili upate shilingi yao lazima wadai passport na wajaze fomu kadhaa na kukupa risiti yako, yaani huhitaji kuuliza.

Nachotaka kusema ni kuwa hawa Equity Bank wanahujumu uchumi wetu, wanatorosha dola zetu kupeleka kwako na hivyo kusababisha kushuka na kuporomoka kwa shilingi yetu.

Sio hiyo tu! Kuna libenki linaitwa BOA, Inakula hela za watu vibaya sana, wafanyakazi wake wanakula rushwa, Wanakata hela za watu hovyo, bila mpangilio ukiziacha benki.Wasumbufu, wafanyakazi wake ni wasanii wasanii tu.
 
Mtoa maada umesema mwenyewe kuwa hata huko Bureau De Change ni mpaka uombe risit ndo unapewa vinginevyo hupewi....sasa hapa ni kuwaonea Equity Bank bila sababu yeyote. BOT ndo tatizo usig=dhani kwamba hawajui...wanjua kwa undani kuliko wewe ufikiriavyo na hii sio jambo jipya. Kila mradi ama bank hapa nchini vigogo na wtawala wana share zao humo kwahiyo tuwalaumu viongozi wetu kabla ya kuwalaumu Equity Bank.

Ni kweli mkuu ila katika bank zinazofanya vizuri Hawa wakenya wapo serious wanafungua matawi kila kukichwa pia hawana makato yasiyo na maana
 
Equity ndo bank pekee mteja unaweza kufungua account bila hata kuwa na shilingi moja, ndo bank pekee unaweza kutoa 1000/= kwenye ATM hii ndo bank ya makabwela ndio maana inakua kwa kasi ya ajabu. Mabenki ya kizalendo yamekaa kiwiziwizi ndio maana hata hawana matawi nje ya Tanzania. Hilo tatizo ulilokutana nalo ni la kiinchi siyo equity tu. Mimi mwenyewe sijawahi kuchange hela ya kigeni nikapewa risit kwanza hii biashara inafanywa kienyeji sana. Equity ni bank nzuri Kuliko bank zote za kitanzania.
 
Nadhani hiyo nikazi ya TRA nasio BOT
Wa kwanza kuwajibika hapa ni BoT maana ndio regulator wa Mabenki yote na ndiye Banker wa Mabenki yote. TRA wao hawana ujanja maana BOT wakiwapelekea hesabu za Benki fulani kama regulators, TRA hawawezi kuwa na jeuri yoyote.Issue kubwa hapa ni kuwa Equity Bank watakuwa wanatorosha dola zetu na hivyo kuchangia ktk kushuka thamani ya shilingi yetu.Vv
 
Equity ndo bank pekee mteja unaweza kufungua account bila hata kuwa na shilingi moja, ndo bank pekee unaweza kutoa 1000/= kwenye ATM hii ndo bank ya makabwela ndio maana inakua kwa kasi ya ajabu. Mabenki ya kizalendo yamekaa kiwiziwizi ndio maana hata hawana matawi nje ya Tanzania. Hilo tatizo ulilokutana nalo ni la kiinchi siyo equity tu. Mimi mwenyewe sijawahi kuchange hela ya kigeni nikapewa risit kwanza hii biashara inafanywa kienyeji sana. Equity ni bank nzuri Kuliko bank zote za kitanzania.

Duuuh
Usionge mambo usiyo kuwa na uhakika !
CRDB Ina branch nje ya tanzania .
Kama ulikua hujui basi fahamu Hilo na inafanya vizuri .
 
Duuuh
Usionge mambo usiyo kuwa na uhakika !
CRDB Ina branch nje ya tanzania .
Kama ulikua hujui basi fahamu Hilo na inafanya vizuri .

Kuwa na branchi nje sio issue,issue ni performance yao huko nje.Equity ni moja ya bank zinazokua kwa kasi sana hapa Tanzaniw
 
Lengo la kuficha risit ni ili TRA wasijue wanapata faida kiasi gani . Nchi ya hovyo hovyo kabisa hii

Halafu hao TRA wnwhangaika na kiusafiri cha mtu binafsi-babysitter wapate mikodi kibao!
Atakayepokea hii nchi ana kazi kubwa sana,atakuta imeoza kila kona.
 
Back
Top Bottom