Cathode Rays
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 1,738
- 1,495
Acha mambo yako wewe kwanza equity bank wako vizuri sana mie nina akaunti yangu pale ya dola tena wako vizuri sana kwenye rate zao sio kama mabenki yetu hapa wanatudhulumu sana sasa ukienda crdb, nmb au nbc utaambiwa dola1=1700tsh badala ya 2000tsh, lakini equity wanawazidi hata hizo bureau de change kwa rate. Watu wengi siku hz wanaenda kubadilishia fedha zao equity kwa sababu hizo, na mie risiti huwa napewa!
Mkuu hapa hakizungumzwi rate ya exchange zaidi bali kutoa receipt
Swali ni kwa nini watoe risiti kwa wengine (Kama madai yako kuwa unapewa risiti ni ya kweli) na wengine hawapewi risiti?
Twende Mbele turudi nyuma hii nchi ukusanyaji wa mapato (ukiachilia PAYE wanayoipata kilaini bila jasho kuwatoka) hauko vizuri na usimamizi wake unakosa umakini...utoaji wa risiti ni mtu/taasisi/firm akiamua atoe au asitoe na sio suala tena lazima na la kisheria