Equity Bank wanahujumu uchumi wetu

Equity Bank wanahujumu uchumi wetu

hoja zuri lakini haitapata watu wa kuchangia kwa sababu wachangia wa forum hii wanapenda kujadili watu badala ya issue

Wanapenda sana ile midoli ya lara1
 
Last edited by a moderator:
Wadau,

Hata kama ni uwekezaji lazima ufuate sheria za nchi husika, lazima kuwe na win win situation.

Kwa bahati mbaya sivyo hivyo kwa haya mabenki ya nje yanayofurika nchini kila uchao, wanakuja kutuibia na kutuhujumu. Najiuliza, wanapata wapi ujasiri wa kukiuka masharti ya biashara na uwekezaji? Hivi ni kweli Benki Kuu haina mechanism ya kucheki kama haya mabenki yanafuata sheria za nchi.

Wiki tatu zilizopita nilienda Equity Bank pale Golden Jubilee kuchenji dola elfu mbili ili nipate shilingi niweze kufanya malipo mbali mbali ya kiofisi. Nilipofika Equity Bank nilielekezwa nipande ghorofani ambapo nilimpatia teller hizo dola ili anipe shilingi. Ajabu ni kuwa, nilipomwomba risiti akagoma ati hawatoagi risiti! Nikamwambia hicho kitu haiwezekani na hakipo, dada akasema ndivyo ilivyo na akamuuliza jirani yake ili nithibitishe, na mwenzake akanithibitishia! Ndipo nikawaambia wanirudishie dola zangu nikaenda kubadilishia Bureau de Change ambao baada ya kudai risiti walinipa.

Ijulikane kuwa hata hizo Bureau de Change nao ni hivyo hivyo, risiti ni hadi uidai. Wenzetu Uganda hata ukiwa unauza dola ili upate shilingi yao lazima wadai passport na wajaze fomu kadhaa na kukupa risiti yako, yaani huhitaji kuuliza.

Nachotaka kusema ni kuwa hawa Equity Bank wanahujumu uchumi wetu, wanatorosha dola zetu kupeleka kwako na hivyo kusababisha kushuka na kuporomoka kwa shilingi yetu.
Ni kweli mkuu. Kwenye hili suala la forex tunashangaza. Utadhani tupo enzi zile za barter system. Hata mimi nisiye mchumi naona twapoteza kodi katika eneo hilo...
 
Si Equity Bank tu,hapa Tanzania hakuna udhibiti wowote wa exchange ya pesa za Kigeni.Nchi za Wenzetu mfano Rwanda kuna udhibiti mkubwa wa Pesa za Kigeni,ni sehemu chache wanakopokea malipo kwa pesa yakigeni.Nenda India,ukienda India mwaka hadi Mwaka rupee 4 ni Dolar 1.Ukienda hata kwenye duka la kuuza pesa unahitaji Dolar lazima ujaze form yenye maelezo malefu kama una haraka ya Kitanzania Unaweza ukaondoka bila kuhudumiwa.Unaambiwa utoe Passi ya kusafiria, makusudi ya dola hizo labda niza matumizi ukiwa kwnye Transit nyumbani,lakini ukisema unahitaji kufanya shopping India utaambiwa utumie Rupee .

Mbona kigali fedha zinauzwa sokoni kama matunda, utakuta mtu kapanga fungu la dola tshs ushs kshs ukifika unachagua kama unataka fedha gani.
 
Risiti ina umuhimu sana. Kwanza kuiongezea mapato serikali kwa yule kukatwa ushuri. Pili kama hujaomba risiti wanachofanya wanakubadilishia kwa "Rate" tofauti ukiomba "Risiti" wanakubadilishia kwa "Rate' halali. Siku jaribu kwenda kubadilisha fedha fanya kama hutaki risiti akikupa zile hela mwambia naomba risiti utaona anapiga mahesabu upya na kukuongeza kile ambacho ungekiacha bila risiti.

Ambao hawaombi risiti wanacha change nyingi sana, ni faida kwa yule. Risiti kwa ofisini/mwajiri hazina nguvu sana kwa sababu hakuna popote zinapotunzwa akisoma, akiona rate akihakiksha fedha zipo sawa basi anaweza ichana.

Shukran sana
 
Mimi nadhani umependa tu kuipaka matope Equity benki,kwani ni Equity tu ndio inahujumu uchumi kisa hawatoi receipt unapobadilisha USD?na je mashirika ya umma ambayo yanadai yalipwe USD ili kutoa huduma wakati USD sio pesa halali ya kulipia huduma hapa Tanzania nayo unayaweka kundi gani?
 
Acha mambo yako wewe kwanza equity bank wako vizuri sana mie nina akaunti yangu pale ya dola tena wako vizuri sana kwenye rate zao sio kama mabenki yetu hapa wanatudhulumu sana sasa ukienda crdb, nmb au nbc utaambiwa dola1=1700tsh badala ya 2000tsh, lakini equity wanawazidi hata hizo bureau de change kwa rate. Watu wengi siku hz wanaenda kubadilishia fedha zao equity kwa sababu hizo, na mie risiti huwa napewa!
Ninawasiwasi wewe ni kati ya wanaosaidia kushusha thamani ya fedha yetu au unafurahia pengine uraia wako pia ni utata. Naona kama uzalendo hakuna kabisa hapa. Maelezo yako tu yanaonesha. Kama hata account yako tu ni ya dolla na huna imani na benki za ndani. Pia unashangilia kubadirisha kwa 2000 badala ya 1700 yaani unatamani ishuke zaidi. I si.ply hate people of your kind
 
Fursa hiyo nzuri sana mabenki mengine waige tu no kutoa risiti. Watz usingizi wa pono ni jadi yetu.
 
Acha mambo yako wewe kwanza equity bank wako vizuri sana mie nina akaunti yangu pale ya dola tena wako vizuri sana kwenye rate zao sio kama mabenki yetu hapa wanatudhulumu sana sasa ukienda crdb, nmb au nbc utaambiwa dola1=1700tsh badala ya 2000tsh, lakini equity wanawazidi hata hizo bureau de change kwa rate. Watu wengi siku hz wanaenda kubadilishia fedha zao equity kwa sababu hizo, na mie risiti huwa napewa!

Nimeenda jana waligoma kunipa receipt. Acha umburula wako. No research no right to speak.
 
Jamaa anajiita laki na pesa na hajui maana ya receipt.... Ni sawa na dereva asiyejua matumizi ya mafuta kwa gari! Wewe ni wa kupiga tu

Nilidhani una akili, kumbe umejaza makamasi tu kichwani!!
 
Wadau,

Hata kama ni uwekezaji lazima ufuate sheria za nchi husika, lazima kuwe na win win situation.

Kwa bahati mbaya sivyo hivyo kwa haya mabenki ya nje yanayofurika nchini kila uchao, wanakuja kutuibia na kutuhujumu. Najiuliza, wanapata wapi ujasiri wa kukiuka masharti ya biashara na uwekezaji? Hivi ni kweli Benki Kuu haina mechanism ya kucheki kama haya mabenki yanafuata sheria za nchi.

Wiki tatu zilizopita nilienda Equity Bank pale Golden Jubilee kuchenji dola elfu mbili ili nipate shilingi niweze kufanya malipo mbali mbali ya kiofisi. Nilipofika Equity Bank nilielekezwa nipande ghorofani ambapo nilimpatia teller hizo dola ili anipe shilingi. Ajabu ni kuwa, nilipomwomba risiti akagoma ati hawatoagi risiti! Nikamwambia hicho kitu haiwezekani na hakipo, dada akasema ndivyo ilivyo na akamuuliza jirani yake ili nithibitishe, na mwenzake akanithibitishia! Ndipo nikawaambia wanirudishie dola zangu nikaenda kubadilishia Bureau de Change ambao baada ya kudai risiti walinipa.

Ijulikane kuwa hata hizo Bureau de Change nao ni hivyo hivyo, risiti ni hadi uidai. Wenzetu Uganda hata ukiwa unauza dola ili upate shilingi yao lazima wadai passport na wajaze fomu kadhaa na kukupa risiti yako, yaani huhitaji kuuliza.

Nachotaka kusema ni kuwa hawa Equity Bank wanahujumu uchumi wetu, wanatorosha dola zetu kupeleka kwako na hivyo kusababisha kushuka na kuporomoka kwa shilingi yetu.

Nadhani hiyo nikazi ya TRA nasio BOT
 
Viongozi waache kulala ofisini wakati uchumi wa nchi unahujumiwa otherwise na wao wanafaidika na mchezo huo mchafu,,
 
Utamaduni wa kutoa risiti hapa nchini haujazoeleka na wafanya biashara wengi, yaani hawataki kabisa. Mimi jana nilienda duka moja la kuuza voucher za jumla mtaa wa Samora. Nikaomba risiti akaakimya , nikasisitiza ndo akaniandikia kikaratasi akaniambia eti nienda kwenye duka letu lingine pale Benjamin mkapa wataniandikia risiti! Jamani, yaani nipate huduma samora, risiti nikachukue posta mpya..!

Kuna udhaifu mkubwa sana katika kusimamia sheria kanuni na taratibu katika nchi hii. Tafadhali wahusika chukueni hatua hata ya kuwakumbusha basi wafanya biashara kutimiza wajibu wao..!
 
Kama wako hivyo wanakosea sana

Sasa mkuu, nani awajibike, na ni nani hawajibiki hapo? Mwizi umwchie fursa halafu uje kumlaumu wakati umelala mlango wazi na huilindi nyumba yako?

Vv
 
Mtoa maada umesema mwenyewe kuwa hata huko Bureau De Change ni mpaka uombe risit ndo unapewa vinginevyo hupewi....sasa hapa ni kuwaonea Equity Bank bila sababu yeyote. BOT ndo tatizo usig=dhani kwamba hawajui...wanjua kwa undani kuliko wewe ufikiriavyo na hii sio jambo jipya. Kila mradi ama bank hapa nchini vigogo na wtawala wana share zao humo kwahiyo tuwalaumu viongozi wetu kabla ya kuwalaumu Equity Bank.

Msome vizuri, asema ilbidi arudishiwe dola zake kwa kuwa walikataa kutoa risiti.

Ujue pia kwa benki risiti ni lazima unapofanya muamala wowote.

Vv
 
Kuna siku nilikuwa naenda Dubai kufika airport nikaitwa na askari
Akaniuliza umefuata nini Dubai nikamwambia biashara
Akasema twende huku,tukaingia chumba fulani akaniambia una una pesa?
Nikamwambia ndio nikampa pesa akazicheck kwenye mashine akaniruhusu nikaondoka zangu baada ya uhakiki

Na ukiwa kule ukibadili pesa lazima wakupe risti na pasi yako uwape photo copy
 
Bt kubadilisha hela kwan kuna mapato unalipia?!!cjaelewa coz zile rate zimequotiwa cdhani km kuna vat pale

Yan wanapobalidilisha pesa lazima wanapata mapato, kwa mfano, ukienda kununua dola moja utauziwa tsh 2050, ila ukienda kuuza dola moja watainunua kwa Tshs 1700, sasa haya mapato wanayopata wanatakiwa kulipia kodi, ndicho aliyomaanisha mtoa mada
 
Back
Top Bottom