BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 43, amethibitisha kuwa atagombea tena katika uchaguzi wa Novemba.
Makamu wa Rais, Teodoro Nguema Obiang Mangue ambaye ni mtoto wa Rais huyo, alitoa tangazo hilo kupitia Twitter siku ya Ijumaa akisema ni "Kwa sababu ya haiba yake, uongozi wake na uzoefu wake wa kisiasa."
Chama cha Obiang cha Democratic Party of Equatorial Guinea kinashikilia viti 99 kati ya 100 katika Bunge linalomaliza muda wake na viti vyote 70 vya seneti.
Kwa miaka mingi nchi imekuwa ikitegemea zaidi mafuta na gesi, ambayo huchangia asilimia 75 ya mapato, ambayo mengi yako mikononi mwa idadi ndogo ya watu.
Kulikuwa na uvumi kwamba mwanawe Obiang anaweza kuchaguliwa kuwa mgombea wa chama hicho lakini tangazo la Ijumaa lilithibitisha kuwa Rais Teodoro ana mpango wa kurefusha utawala wake ambao mara zote hukosa mshindani kutokana na aina ya utawala nchini humo.