Epuka Mtego huu Jakaya

mawaziri wasipoondolewa madaktari tutakosa imani kwa wizara ya afya, na serikali kwa ujumla kwani iliahidi kufanya hivo kupitia waziri mkuu. Mawaziri wakiondolewa tutapata imani kwa serikali na pia tutapata nafasi ya kujadiliana na serikali juu ya kuimprove sekta ya afya na hivyo kuondoa vifo visivyo vya lazima kwa wagonjwa wetu kutokana na ukosefu wa vifaa na dawa muhimu, hivi unajua ni watu wangapi wanakufa kwa siku kwenye hospitali kubwa kama muhi2 kwa kukosekana adrenaline tu?4 ur info watu wanakufa daily kwa kukoseekana dawa muhimu bila hata ya mgomo
yaani hao makuwadi wa serikali hata mkiwaambiwa mambo ya maana wao wanaongea kishabiki tu! Biblia inawaita vipofu wenye macho na viziwi wenye masikio!
 
mkuu samahano, sekta ya afya hapa nchini ilikuwa imara lini na ilianza kudorora lini?
kwa hiyo kama mwenzako hakufanya vizuri wewe ndio unatakiwa uje kuharibu kabisa? Mseven wenzake walifanya vibaya yeye akarekebisha, kagame kutoka nchi yenye mizoga hadi maendeleo, kenya narc wanasonga mbele na uchumi wa kenya haukamatiki. Sisi hadi leo tunasingizia vita vya idi amin. Shida sio mtangulizi wewe uliyepo ungeweza kufanya zaidi.
 
Mkuu samahano, sekta ya afya hapa nchini ilikuwa imara lini na ilianza kudorora lini?
ilianza kudorora muda mrefu sana,since nimejiunga kwenye hii fani, thats why nakwambia tumechoka kuona watu wakifa mikononi mwetu kwa sababu ya ukosefu wa vifaa na dawa, its enough, come what may.
 
acha vitisho kwa mkuu wa nchi, wewe nani bwana!
lak
kuwa baba sio kulala kitanda kimoja na mama kuwa baba ni kutekeleza majukumu ya kifamilia! Kuwa mkuu wa nchi ni kuact kutokana na uhitaji wa nchi lakini kama huyo mkuu wako wa nchi hatimizi majukumu acha ameze vidonge! Kama kila wakati anamuingiza mkenge pinda halafu pinda na yeye haone! Posho mkenge, madactari mkenge, jairo mkenge oooowi! juzijuzi tb joshua (yule mchungaji maarufu wa nigeria) alitabiri kwamba kuna rais mmoja wa afrika ata-rest in peace! Watanzania tunatamani huo utabiri utimie kwetu!
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.

Wakati unaandika haya naamini ulikuwa umelewa, bandika mawazo ukiwa sober.
Salma Kikwete ni Waziri wa wizara gani? Familia; mke na watoto wanahusika vipi na mgomo wa madaktari?
 
Hivi ni nini hasa kinachomfanya Kikwete ashindwe kuwaondoa Nkya na Mponda? Kama ni wazuri sana kwenye utendaji si awahamishie wizara nyingine?

Una hakika sababu za uteuzi utendaji mzuri wa kazi? Yawezekana siyo ndiyo maana anashindwa kuwachukulia hatua stahili nadhani pengine hata kuwahoji hathubutu.
 
Madactari majibu yenu mtayapata kutoka kwa Rais atakapo shuka toka kileleni mwamlima Kilimanjaro.
huyo ndio JK bwana Rais ambae waTanzania wengi mwaka 2005 walimuamini kuliko marais wote, lakini imekuwa kinyume amekuwa Rais mbovu kuliko marais waliotangulia
 
Mtu mwenye akili na ufahamu hawezi kutetea tumbo lake huku akiwa amezungukwa na ndugu jamaa na marafiki wenye shida na wasiojua kesho yao.Tanzania ni yetu wote, maamuzi ya hovyo na dhulma zenu zinaiathiri jamii yote. Wezi wakubwa!!
Damu nzito kuliko maji,wana macho lkn hawaoni ,wanamasikio lkn hawasikii ,ujumbe umeufikisha ndg licha ya vikwazo vingi vya wapita njia
 
madai ya madaktari yanafanyiwa kazi na serikali.nyie mnaotaka majibu baada ya siku tatu mjue kuwa utendaji na maamuzi ya nchi sio sawa na maamuzi ya familia ambayo wewe na mkeo mnaamka na kuamua jambo.hili ni suala la kitaifa linahitaji mambo mengi.subira inahitajika

wewe acha unazi uliopitiliza, madai ya madaktari yanafanyiwa kazi siku ngapi? Posho za wabunge mbona hazikupitia mchakato wote huo? Au za wabunge zipo na za madaktari hazipo?
 
Najaribu kulinganisha madhara ya mgomo wa madaktari uliopita na thamani halisi ya madai yao naona kwamba watu/ndugu zetu waliopoteza maisha yao kutokana na kukosa matibabu mahospitalini ni zaidi ya hicho wanachokidai. Wanatishia kugoma tena ili wananchi waendelee kufa kana kwamba hawakuridhika na vifo vilivyotokea katika mgomo wa awali. Kwa mtu yeyote mwenye kupenda haki na kujali wenzake hawezi kudai haki yake kwa kusababisha vifo vya wengine.

Serikali isiyojali wananchi wake itazembea utekelezaji wa maazimio yake na madaktari na kupelekea kufumuka upya kwa mgomo. tafakari
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.
Mbona unajitia kiherehere!!! Wewe ndio msemaji wa Ikulu?

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom