Epuka Mtego huu Jakaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Epuka Mtego huu Jakaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Hunter, Mar 5, 2012.

 1. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Naamini u mzima, na najua huwa unapita hapa kama baadhi ya watendaji wako wanavyopita kwa majina bandia.

  Mgomo wa madraktari ndo ushatangazwa naamini mkuu utaweka siasa na kiburi chako pembeni katika kutatua swala hili, japo ulijaribu kuwatuliza kwa maneno yaliyojaa siasa kwenye hotuba yako ya mwisho wa mwezi amini mkuu haijasaidia kitu, kwani makubaliano ilikuwa ni within a month baadhi ya matatizo yawe yameshatatuliwa, swala la kutangaza kwamba waziri mkuu ndo kapokea faili dakika za mwisho za mwezi huo mliokubaliana ni uthibitisho wa kwamba mliwadanganya madaktari, mlitumia siasa kukubaliana nao huku mkisahau mwezi mmoja ni siku thelathini tuu.

  Chief najua wewe ni mbishi na utaacha madaktari wagome kwani wewe huumii kwa lolote, najua utataka kuweka muscle kidogo kwa kutishia kuwafuta kazi, mkuu Stuka maamuzi ya hovyo katika swala hili yatagharimu maisha ya wengi, yataibua migomo toka kada nyingine na amini nalokuhasa itakugharimu mkuu.

  Enzi za bora liende zimekwisha, fanya kazi kama ulivyoomba wananchi wakuamini na kukupa madaraka.

  Ikulu si mahali pa kupatia visa za kwenda kuzurura nje ya nchi kila kukicha, Ikulu ni nyumba inayokutanisha Pure cream and Think Tanks ya taifa.
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Swala la kuwaondoa mawaziri wako Mponda na Nkya yalikuwa juu yako kwani hao ni wateule wako, ulifahamu na unafahamu wewe ndo ulitakiwa uanze utekelezaji, kumtaja waziri mkuu wakati wewe ndo boss wake ni ishara tosha hufahamu hata hayo waliyokubaliana ama hujaona umuhimu wake
  Peleka pesa ya walipa kodi kwenye uchaguzi wa Arumeru kitakapo waka utakosa pa kutokea
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.
   
 4. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Vululu vululu
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mtoa maada, la kuvunda halina ubani. Umeona maoni ya mmoja wa "washauri" wake (anajiita maundumula) hapo juu?
   
 6. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hata yeye aondoke tu hana maana
   
 7. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,464
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Ujumbe umefika. Naunga mkono maoni yako. Huu sio wakati wa siasa kwenye maswala yanayolihusu Taifa letu. Asikilize ushauri!
   
 8. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Aende arumeru
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sijakusoma Mkuu, unashauri? unatukana? au unasikitika? Wewe ni Daktari au basi tu leo mama kakuudhi home? Pole.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  inaonekana umeandika ukiwa uelewa pombe kali ee
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mbona mnatanguliza siasa au mnajua suala hili lina wanasiasa nyuma? manake kiongozi hawezi kufanya siasa kama hajachokzwa na wanasiasa wenzake. Tumabizane wakuu akina nanihii wako na Madaktari, jambo linalomkera Mkuu? Najua ndo zao kutafuta umaarufu.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  madai ya madaktari yanafanyiwa kazi na serikali.nyie mnaotaka majibu baada ya siku tatu mjue kuwa utendaji na maamuzi ya nchi sio sawa na maamuzi ya familia ambayo wewe na mkeo mnaamka na kuamua jambo.hili ni suala la kitaifa linahitaji mambo mengi.subira inahitajika
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo ulitaka aseme amepokea faili wakati suala zima linashughulikiwa na PM. Ni umbumbumbu au nini?
   
 14. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  JAKAYA HATINGISHIKI NYIE HANGAIKEni TUU
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mtu mwenye akili timamu hawezi kushabikia mgomo wa madaktari.mleta mada we ni mchochezi na wala huishi hapa tanzania huathiriki na matokeo ya mgomo wa madaktari.
   
 16. Chihuahua

  Chihuahua New Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama miaka 45 iliyopita hamkukumbuka kweli leo mwezi mmoja mmtaweza kufanya kitu?
  Subra mnapolipana posho kubwa kubwa huwapo pia?
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mleta mada ni msaliti wa damu ya watanzania maskini ambao hawawezi kwenda kutibiwa india
   
 18. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ndugu Tamuchungu, kwanza umenihukumu nimelewa pombe, pili unaniita msaliti, kwako msaliti ni yule anaesema ukweli? ulitaka nikae kimya wakati namshuhudia mtalii wako akizurura nchi za wenzake kila uchwao? ameleta tija gani kama si kuwa hovyo toka alipoanza safari za kwenda kuomba omba kila leo?
  Mimi na wewe nani msaliti sasa?!
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi ni nini hasa kinachomfanya Kikwete ashindwe kuwaondoa Nkya na Mponda? Kama ni wazuri sana kwenye utendaji si awahamishie wizara nyingine?
   
 20. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mtu mwenye akili na ufahamu hawezi kutetea tumbo lake huku akiwa amezungukwa na ndugu jamaa na marafiki wenye shida na wasiojua kesho yao.
  Tanzania ni yetu wote, maamuzi ya hovyo na dhulma zenu zinaiathiri jamii yote. Wezi wakubwa!!
   
Loading...