Epuka Mtego huu Jakaya

Epuka Mtego huu Jakaya

Swala la kuwaondoa mawaziri wako Mponda na Nkya yalikuwa juu yako kwani hao ni wateule wako, ulifahamu na unafahamu wewe ndo ulitakiwa uanze utekelezaji, kumtaja waziri mkuu wakati wewe ndo boss wake ni ishara tosha hufahamu hata hayo waliyokubaliana ama hujaona umuhimu wake
Peleka pesa ya walipa kodi kwenye uchaguzi wa Arumeru kitakapo waka utakosa pa kutokea

Labda ndo maana anasafiri mara kwa mara kwaajili ya kutafuta mahali pakukimbilia
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.

kwani mama salma sisi tumemwajiri? Aliyeajiriwa ni jk na akina nkya na kama ndo waajiriwa tuna uamuzi wa kuwaondoa au kuwaacha madarakani
 
mtu mwenye akili timamu hawezi kushabikia mgomo wa madaktari.mleta mada we ni mchochezi na wala huishi hapa tanzania huathiriki na matokeo ya mgomo wa madaktari.

Hakuna anayeshabikia mgomo wa madaktari,na kama wapo/yupo basi ni serikali yenyewe. Walikubaliana na kupeana implementation period kwa baadhi ya madai. Iweje hadi leo kina Mponda na Nkya bado wanapeta?
 
Kweli kuna watu na viatu. Hivi sio vitu vya kushabikia hata kidogo, impact yake inagharimu maisha ya watu.
 
kabla ya kujiunga na hii forum wewe ni kati ya watu walinisisimua sana!kwa hii post ya leo umeitesa sana nafsi yangu!!labda hujajua haswa ni nini madrs wanataka ktk madai yao ya msingi.na declare interest,mimi niko ktk afya!pamoja na maslahi,hoja ya kwanza ya msingi ya madrs ni kufanyika kwa mabadiliko ya msingi kabisa ktk secta ya afya yenye lengo la kuokoa na kuboresha maisha ya watz!nitakupa scenarios ambayo naamini itakusaidia kujua mgomo huu inasababishwa na mdrs kutaka kuokoa maisha ya watu na si vinginevyo!
Mkuu sijui una access kiasi gani na mahospitali yetu,lakini watu wanaokufa kila siku kwa kukosa huduma stahiki kutokana na upungufu wa vifaa ni kubwa kuliko ambavyo mtu yeyote amewahi kusema.aisee wagonjwa wanakufa kwa kukosa vitu kama adranaline,lasix na vitu vidogo sana ingawa wewe huwezi jua.mimi binafsi nimeshatoa pesa yangu mara nyingi sana ktk juhudi ya kuokoa maisha ingawa hata malipo yangu hayaji kwa wakati na kuna wakati unakopa ili kukabiliana na hali harisi.
Hosptali kuu kama muhimbili inafikia mahali haina gloves ,thitre gowns na vinginevyo ni hali ya kawaida kabisa,fikili m/nml,temeke na amana kuna nini.!ct scan muhimbli huwa ni ishu wkt,m/nyamala ndio usahau.
Sasa sijui unalisemeaje na hili juu ya hawa watu wanaokufa kimyakimya bila ya wewe kujua.
Mi nafikili wataz tuache kuamini kauli za ki propaganda hata kwenye mambo ya kitaaluma.mimi na amini mkuu wangu uko uninformed juu ya hali halisi na unatoa maoni yako juu ya yanayotokea ndani ya kabuli na ilhali wewe si maiti.kaka matukio ya op kufanyika na tochi ni mambo ya kawaida sasa.mbaya zaidi waheshimiwa hutoa kauli kama secta ya afya imeimalika,huduma ya mama na mtt ni nzuri ilhali hali ni tofauti kabisa na wakati mwingine ma drs na wana afya wengine kutupiwa lawama.tukikaa kimya ndio watu watakufa zaidi kuliko mgomo ukifanyika tena kwa muda mrefu.lakini pia hivi kuna gharama gani hawa jamaa wakijiuzuru na kuzuia mgomo bdala ya ksbr hao wauwaji kama unavyowaita watimize azma yao ya kuua!?hivi unaweza kumtuma mtt wako apite njia ambayo unajua kuna mmbwa mkali na bado ukasema unampenda mtt wako.!?aisee kujiuzuru kunahitaji masaa mangapi!?embu nijuze wakulaumiwa atakuwa ni nani mgomo ukitokea maana hata serikali imekili madai ya drs ni ya msingi,kwa nini inakuwa vigumu kutekeleza makubaliano!!??kwa maneno mengine wewe hujali ile halaiki ya watu wanaokosa huduma stahiki na kufa hata hapa wakati mimi naandika na ambao walikosa msemaji au ku act kwa vitendo maana kama kwa maandishi imeandikwa sana na ahadi kedekede kutolewa bila utekelezaji kama inavyotokea sasa.mkuu afya ya mtu haihitaji siasa na kama unasukali na ukapiga siasa babu wa samunge atakuponya ukweli utabaki palepale!achana na propaganda na utimize wajibu wako.
umenena vema sana mkulu,'adhabu ya kaburi aijuaye maiti'
 
mleta mada ni msaliti wa damu ya watanzania maskini ambao hawawezi kwenda kutibiwa india

we ndio msaliti na tapeli mkubwa uliyetumwa na hao magamba yako,
jambo la kumshauri rais ili kuepusha matatizo kwa kuacha ulaghai wake kwenye maisha ya watu limekuwa uchochezi tena?tumekosa wazalendo nchi hii sizani kama we ni mtanzania
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.

Wow....ni heri kuwa na post hata 20 lakini za maana kwa jamii kuliko kuwa na 1,399 zilizojaa u.p.u.p.u. Hivi kweli mtu anaweza kuja tu na kukwambia umwache mkeo vinginevyo nitagoma kazi!! Kwani Kikwete na mkewe wana faida gani sasa hivi kwa watanzania? Hata wao wanaweza kuondoka vilevile kuliko wananchi kuendelea kutaabika. Mbona njia ya Msoga inajulikana!!
 
madai ya madaktari yanafanyiwa kazi na serikali.nyie mnaotaka majibu baada ya siku tatu mjue kuwa utendaji na maamuzi ya nchi sio sawa na maamuzi ya familia ambayo wewe na mkeo mnaamka na kuamua jambo.hili ni suala la kitaifa linahitaji mambo mengi.subira inahitajika
ndio maana mliwaua watu wanne songea kwa sababu walikosa subira! Walitakiwe wafe 100 ndipo waandamane sio 9! Pumbafu kabisa!
 
Kikwete,kama Mponda na mama Nkya ni wasaidizi wazuri kwako,wapeleke WAMA hapo mtashauriana na mama Mwanaasha pekee lakini sisi hatuwataki.
 
Hivi wasipoondolewa mawaziri madaktari wanakosa nini?

Hivi wakiondolea mawaziri madakatari wanapata nini?

Hivi hii habari ya nipe nikupe imetoka wapi?

Aisee ningekuwa JK..wala nisingekubali huu upuzi ..

Hawa madks imefika mahali tuwaambie ukweli kwamba mnaboa..

Hata mkilipwa milima ya dhahabu kazi ya kutibu inahitaji ubinadamu zaidi kuliko pesa oops..
 
Hivi wasipoondolewa mawaziri madaktari wanakosa nini?

Hivi wakiondolea mawaziri madakatari wanapata nini?

Hivi hii habari ya nipe nikupe imetoka wapi?

Aisee ningekuwa JK..wala nisingekubali huu upuzi ..

Hawa madks imefika mahali tuwaambie ukweli kwamba mnaboa..

Hata mkilipwa milima ya dhahabu kazi ya kutibu inahitaji ubinadamu zaidi kuliko pesa oops..
mawaziri wasipoondolewa madaktari tutakosa imani kwa wizara ya afya, na serikali kwa ujumla kwani iliahidi kufanya hivo kupitia waziri mkuu. Mawaziri wakiondolewa tutapata imani kwa serikali na pia tutapata nafasi ya kujadiliana na serikali juu ya kuimprove sekta ya afya na hivyo kuondoa vifo visivyo vya lazima kwa wagonjwa wetu kutokana na ukosefu wa vifaa na dawa muhimu, hivi unajua ni watu wangapi wanakufa kwa siku kwenye hospitali kubwa kama muhi2 kwa kukosekana adrenaline tu?4 ur info watu wanakufa daily kwa kukoseekana dawa muhimu bila hata ya mgomo
 
Rais hawezi kuwaondoa watendaji wake only kwa sababu madokta wanataka, akishamuondoa Nkya na Mponda watataka amuache na mama Salma Kikwete.
Mkuu usemalo ni kweli kabisa usemayo. Mwanzoni serikali ilitoa uamuzi wa kiserikali ambao nilidhani ulikuwa uamuzi thabiti lakini baadaye serikali ika yield na PM akawasimamisha akina Nyoni kutekeleza matakwa ya Madaktari. PM Akasema ya Waziri na Naibu amemwachia Rais awashughulikie, hapo ndipo serikali ilipoingia mtegoni. PM angesema tunawasimamisha hawa lakini viongozi wa kisiasa waachwe ili kuwe na win win situation lakini ikaonekana kana kwamba serikali imekubali kila kitu!
 
mawaziri wasipoondolewa madaktari tutakosa imani kwa wizara ya afya, na serikali kwa ujumla kwani iliahidi kufanya hivo kupitia waziri mkuu. Mawaziri wakiondolewa tutapata imani kwa serikali na pia tutapata nafasi ya kujadiliana na serikali juu ya kuimprove sekta ya afya na hivyo kuondoa vifo visivyo vya lazima kwa wagonjwa wetu kutokana na ukosefu wa vifaa na dawa muhimu, hivi unajua ni watu wangapi wanakufa kwa siku kwenye hospitali kubwa kama muhi2 kwa kukosekana adrenaline tu?4 ur info watu wanakufa daily kwa kukoseekana dawa muhimu bila hata ya mgomo
Mkuu samahano, sekta ya afya hapa nchini ilikuwa imara lini na ilianza kudorora lini?
 
Hivi wasipoondolewa mawaziri madaktari wanakosa nini?

Hivi wakiondolea mawaziri madakatari wanapata nini?

Hivi hii habari ya nipe nikupe imetoka wapi?
kwanza toa huo ujinga uliouandika hapo chini eti "mbowe for presidence" hicho ni kichaka cha kujifichia wakati tunajua wewe ni kuwadi wa serikali! Shida hapo ni dhana ya uwajibikaji ambayo ninyi hamjali. Mponda na Nkya waliwadharau madactari kama wewe unavyowadharau.Wakati wanalalamika maadam Mponda na Nkya wanaposho za kumwaga huku wakisaidiwa na Nyoni basi wasionacho wanaonekana wakilia njaa ni wajinga! "wewe hauna tofauti na yule mke wa rais aliyeambiwa wananchi wanalalamika hawana mkate akawaambia si wanunue keki? watu wote waliokufa kutokana na mgomo wa madaktari ni matokeo ya Pinda kuwasikiliza malimbukeni kama wewe! na tunasubiri matokeo mabaya zaidi maana wajinga kama nyie mnaomshauri rais ndio mko wengi serikalini. MADAKTARI ALUTA CONTINUE na mkichanganyia tu walimu tunaanza!
 
Back
Top Bottom