Mada maalum
Katika maisha huwa kuna mambo watu hufanya lakini ukiangaliwa upande wa pili au jicho la tatu hayana maana binafsi haya ni mambo ambayo huwa siyafanya au sitoyafanya.
Pengine ni huelewa wangu mdogo nafikili hapa utaniweka sawa
*sherehe za HARUSI watu utumia mamilioni ya pesa kwa ajili ya harusi na wengine uchangia michango mingi kwa ajili yasherehe harusi,ila uwa sifikiri kwamba baraka za HARUSI hutokana na SHEREHE au ndoa kutambulika machoni kwa bwana haitaji sherehe,mi napendaga kama ya anko MAGU[emoji204][emoji204][emoji204]
Ndo mfano kwangu wa kuingwa kwani hana utofauti na yule aliefanya na mamilioni ya hela na ndoa ikafa baada ya wiki,
*siku ya WAPENDANAO huwa inanipita kushoto kabisa katika mambo ambayo sipendi kuyasikia moja wapo ni siku hii ya wapendanao,,,niliwahi kuachana na mtu wangu kisa kwanini sijamjaali siku hii maalum,nilimjibu neno UPENDO ipo siku zote,na ndicho ninachokiamini,aliniambia nikae mbali nae kwa maana nitamsumbua sijuw kumjali mwanamke,
*siku ya kuzaliwa kwangu huwa ni moja tu na haitojirudia siku hii na haitaji kumbukumbu kukumbuka siku hii,binafsi sijawahi kufanya sherehe ya kuzaliwa kwangu kwa kile nnachoamini kuwa,siku nilizaliwa ilipita siku nyngi na siwezi zaliwa upya kwa kufanya sherehe.siwezi kutumia pesa kununua cake na vinywaji kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa ambayo haipunguzi wala kuongeza kitu ni bora nikachukue hela hiyo nikawape wenye mahitaji maalumu.
Wewe una mtanzamo gani unaweza kuchangia mtazamo wako..