Epuka kufanya mambo yasiyokuwa ya msingi

Epuka kufanya mambo yasiyokuwa ya msingi

Bullshit

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
1,369
Reaction score
1,641
Mada maalum
Katika maisha huwa kuna mambo watu hufanya lakini ukiangaliwa upande wa pili au jicho la tatu hayana maana binafsi haya ni mambo ambayo huwa siyafanya au sitoyafanya.
Pengine ni huelewa wangu mdogo nafikili hapa utaniweka sawa

*sherehe za HARUSI watu utumia mamilioni ya pesa kwa ajili ya harusi na wengine uchangia michango mingi kwa ajili yasherehe harusi,ila uwa sifikiri kwamba baraka za HARUSI hutokana na SHEREHE au ndoa kutambulika machoni kwa bwana haitaji sherehe,mi napendaga kama ya anko MAGU[emoji204][emoji204][emoji204]
Ndo mfano kwangu wa kuingwa kwani hana utofauti na yule aliefanya na mamilioni ya hela na ndoa ikafa baada ya wiki,

*siku ya WAPENDANAO huwa inanipita kushoto kabisa katika mambo ambayo sipendi kuyasikia moja wapo ni siku hii ya wapendanao,,,niliwahi kuachana na mtu wangu kisa kwanini sijamjaali siku hii maalum,nilimjibu neno UPENDO ipo siku zote,na ndicho ninachokiamini,aliniambia nikae mbali nae kwa maana nitamsumbua sijuw kumjali mwanamke,

*siku ya kuzaliwa kwangu huwa ni moja tu na haitojirudia siku hii na haitaji kumbukumbu kukumbuka siku hii,binafsi sijawahi kufanya sherehe ya kuzaliwa kwangu kwa kile nnachoamini kuwa,siku nilizaliwa ilipita siku nyngi na siwezi zaliwa upya kwa kufanya sherehe.siwezi kutumia pesa kununua cake na vinywaji kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa ambayo haipunguzi wala kuongeza kitu ni bora nikachukue hela hiyo nikawape wenye mahitaji maalumu.

Wewe una mtanzamo gani unaweza kuchangia mtazamo wako..
 
Umenena vema sana [emoji122], ila nikuulize swali dogo tu "ni siku zipi kwako ambazo unazithamin au ni siku special za kuzienzi"?? Maana kwa maoni yako unatak kilasiku ziwe sawa yan flaaati
 
Kweli Aisee ukiwa na pesa itakufundisha jinsi ya kuitumia
Unaweza kuitumia kwa vitu vyenye faida mkuu
Kupeleka watoto shule ni bora kuliko michango ya harusi.
Lakin ajabu ni kwamba tz wanthamini michango ya harusi kuliko ada yashule

Unaweza kutumia hela kusaidia watu wenye maitaji kulko kuzipeleka kwenye mambo ya anasa
 
Ukiwa huna mifereji ya uhakika na pesa lazma uwaze Kama jamaa, ila ukiwa nazo pesa kwelikweli na uhakika wa mifereji yake.... serious inaongea yenyewe na inakufundisha jinsi ya kuitumia yenyewe.
Jarbu kuicotrol pesa sio pesa kukucotrol wwe mkuu
 
Unaweza kuitumia kwa vitu vyenye faida mkuu
Kupeleka watoto shule ni bora kuliko michango ya harusi.
Lakin ajabu ni kwamba tz wanthamini michango ya harusi kuliko ada yashule

Unaweza kutumia hela kusaidia watu wenye maitaji kulko kuzipeleka kwenye mambo ya anasa
Mkuu ukiwa na pesa, Ada ya shule huwezi kuiwazia ni kitu kidogo mno, sanasana utawaza umpeleke mwanao shule gani bora hapa duniani, tunaowaza Ada za watoto ni sisi tusio na uhakika na hela
 
Una mitazamo mizuri, ila usilazimishe mtu akufuate au akuone upo sawa.

Keep that to yourself.
Ndomana nimesema unawezakuwa na mtazamo wko pia ukachangia naamini binadamu wote hatuko sawa.au hatufikirii sawa
 
Mkuu ukiwa na pesa, Ada ya shule huwezi kuiwazia ni kitu kidogo mno, sanasana utawaza umpeleke mwanao shule gani bora hapa duniani, tunaowaza Ada za watoto ni sisi tusio na uhakika na hela
Ila bila bajeti mkuu mambo hayaendi,hata bill gate anabajeti anatoa mkuu ili kuendleza mambo yake maalumu,hivi ushwahi kumuona bill anavaa nguo za bei ghal licha pesa anazo,

Kuwa na nizamu ya pesa inafaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom