Enzi zileee

Enzi zileee

zumbemkuu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
11,362
Reaction score
9,882
1240289_301189940024147_549119256_n.jpg
 
vinasakwa vipaji vya kushiriki UMISHUMTA
 
Ha ha ha tafuta ile tairi ya gari basi yakusukuma japo kwa mkono!!
ilo tairi alikuja fundi viatu akalichukua ili akalichune nyuzi za kushonea viatu, chezea kijijini wewe.
 
kaka Maisha yalikuwa matamu sana enzi tunacheza chandimu. Nna histori tamu sana na chandimu
 
kaka Maisha yalikuwa matamu sana enzi tunacheza chandimu. Nna histori tamu sana na chandimu
mkuu mguu wangu mmoja wa kulia hadi leo ni mpana zaidi kuliko wa kushoto, kuna jamaa alinitegea jiwe nkajua ni kabumbu, akajitega sawia golini ili nimpigie penalty, dah, noma.
 
mkuu mguu wangu mmoja wa kulia hadi leo ni mpana zaidi kuliko wa kushoto, kuna jamaa alinitegea jiwe nkajua ni kabumbu, akajitega sawia golini ili nimpigie penalty, dah, noma.

Pole sana kamanda ndo u Legend huo
 
Nimecheza sana hii makitu aisee upande mmoja lazima mvue mashati bifu uwanjani huwa haliishi...
 
Nimecheza sana hii makitu aisee upande mmoja lazima mvue mashati bifu uwanjani huwa haliishi...

Sasa siku moja upande wangu tumevua,sasa kale ka pichu ka VIP si kakatika kule kunako maungio!Duh nilishtukia refa anasimamisha mpira eti kuna mtu ana jezi tofauti,kumbe kalishapanda na kugota kwenye kwapa!Duhh umenikumbusha mbali aisee!Na hapo ilikuwa mechi kati ya shule yetu na shule jirani!Na nina kidate kiko nje kinashangalia maujuzi yangu uwanjani,duhh hasikwambie mtu!
 
af ukichelewa kurudi nyumbani, unasingizia waalimu walikuchelewesheni shambani kulima mkatawanyika saa 12, kumbe Zumbemkuu alikwama hapo kati kivumbi kinatimka hadi pua inapakaa vumbi. ha ha ha ha.....
baada ya mungai kukataza hii kitu mashuleni na vipaji ndo vilianza safari ya kwenda likizo.
 
Sasa siku moja upande wangu tumevua,sasa kale ka pichu ka VIP si kakatika kule kunako maungio!Duh nilishtukia refa anasimamisha mpira eti kuna mtu ana jezi tofauti,kumbe kalishapanda na kugota kwenye kwapa!Duhh umenikumbusha mbali aisee!Na hapo ilikuwa mechi kati ya shule yetu na shule jirani!Na nina kidate kiko nje kinashangalia maujuzi yangu uwanjani,duhh hasikwambie mtu!
dah mkuu kumbu kumbu yako imenisisimua sana mkuu kama ni zama wewe ndio umenikumbusha kisawa sawa.big up
 
baada ya mungai kukataza hii kitu mashuleni na vipaji ndo vilianza safari ya kwenda likizo.

he! hivi kumbe mpira ulishakatazwa? mi sikujua hilo.... kama ni hivyo mbona itakuwa sera ya kilevi sana hiyo?!
 

Dah!! umenikumbusha kitambo mkuu,magomeni mapipa hiyo,kulikuwa na msomali nakumbuka alikuwa anaitwa Ahmed,akiingia yeye mtaani na mbaula yake ishakula mzigo tayari kwa safari ya Zambia na soka ndio inakuwa imekwisha. Kipindi hicho babu inapigwa soka mtaani kuanzia saa 4 asb siku za mwisho wa wiki.
Soka ilikuwa ikisimama kama anapita bibi au babu au mama mwenye mtoto,au gari zaidi ya hapo ni kipute tu,bibi au mama mtu mzima kama anapita,ataomba ruhusa kabla hajaingia eneo mnalocheza "naomba nipite wanangu; mmoja kati yetu ataamrisha,"mpisheni bibi apite jama; soka litasimama bibi apite.
Kabla hata hajamaliza uwanja wenyewe kupita, mziki unaendelea tena,ikifika saa sita wakati unakokota ngoma kwenda kwenye eneo la wapinzani,unasikia mwito kutoka kwa mdogo wako,'Dulaaaaaaaaa,unaitwa nyumbani;hapo ujue nguna tayari.
Hapo babu unaitikia mwito wa mdogo wako bila hata kunyanyua shingo,maana kipindi dogo anakuita ulikuwa ndio unakokota ngoma,sasa unaogopa ukinyanyua shingo tu,kumuangalia mpira utanyang`anywa.
Sasa angalia basi huo mpira unavyoisha,mmoja tu akienda chukua fulana yake na kusema;"kwa leo jama" maana yake kwa kipindi hicho mpira ndio umeisha mpk jioni hiyo,muda huo tena watu wanasambaa kwenda kupiga msosi wa mchana.Sasa sikwambii hilo vumbi lake miguuni,utasema mmetoka kucheza vanga (ngoma ya kizaramo).
Dah!! kaka umenikumbusha kitambo sana,nakumbuka mengi ya kipindi hicho,nishakula sana mbite (bakora) kutoka kwa marehem mzee wangu, sbbu ya kupenda mpira,mwenyezimungu amrehemu huko aliko mzee wangu na awarehemu wote watu wa kipindi hicho tuliopiga nao soka ya utotoni ambao kifo kimewakuta ughaibuni ktk harakati za kutafuta maisha na wale ambao pia mungu hakuwabariki kusafiri na kifo kikawakutia nyumbani TZ,na awaongezee umri wote wale walio hai na kuwapa uzima ili kuweza kutimiza malengo yao (Amin).
 
Hii kitu ilikuwa inaibua vibaji sana...
 
Back
Top Bottom