ENZI ZILE (Tukumbushane)


Kumbe wote ni vijana? Nilifikiri tumecheza wote "Embakasi" ya Les Mangelepa?
 
Hahahahahhaha!Nimecheka kweli leo!!!:bounce:
Nimekumbuka nlivyokua std 4 kulikua na mshkaji mmoja mchokozi sana
darasani kwetu, bila kumfanya chochote akaanza kunitisha kua atanipiga.
Kila tukitoka shule ananisubiria, bahati nzuri watu nlokua natembea nao
anawaogopa.Basi namuona kwa mbali ananinyooshea kidole, tukiwa shule
ananiambia ipo siku na nikimsemea kwa mwalimu ntakoma.Vitisho vilivyozidi
badala yakusema nyumbani au shuleni nikaamua kuacha kwenda shule.So
nikawa naaga nyumbani kama naenda shule alafu najificha shambani kwetu.:behindsofa:
Nalala...nikichoka nasoma vitabu vyangu vya shule na madaftari mpaka wenzangu
watoke shule.Nikiskia kelele barabarani najua hao....natokeza barabarani najiunga
na wenzangu na mimi naenda nyumbani.Shuleni nauliziwa hamna mtu anaejua
kwanini sipo shuleni.Baada ya siku nne bibi yangu akanifuma...loh nusura nizimie.
Nilikua nasoma zangu kama kawaida ghafla mtu kanishika begani...mbona nilihaha!
Nwyz bibi yangu akanishika mkono mpaka shuleni....kuwaeleza kwanini nimefanya
hivyo hamna alietaka kuelewa...kwa mara ya kwanza na ya mwisho nikachapwa
fimbo za ukweli....yule mshkaji hakufanywa chochote!!

Muda ukapita....std 5 nikapata muda wakulipiza kisasi.
Siku moja nilikua darasani mwenyewe..(muda wa mapumziko) yule mshkaji akaja
akanikuta nakula karanga.Akaniomba nikamnyima...akataka kuninyang'anya, alivyonisogelea
nikampiga konzi alafu nikakimbia nje.....akakasirika vibaya mno so akawa ananikimbiza ili
anipige....nikaokota jiwe nikamrushia ndo kwanza akaongeza spidi.Nikakimbilia upande wa
ofisi ya walimu....kufika mlangoni nikajipaka mate machoni alafu nikachoma ndani.Kulikoni..
kulikoni nikasema fulani kanipiga.Bahati ilikua upande wangu maana mwl. wetu wazamu
alikua hapendi kweli mvulana akimpiga msichana.....akatumwa mtu amuite mi nikaondoka!
Tulivyopishana mlangoni nikamchekea.....alishikwa maskio akanyanyuliwa juu then akapewa
viboko vya haja na adhabu yakunyesha maua juu.Tangu siku hio hakunisogelea tena!!:smile-big:
 
Yaani visa vya hapa....nimecheka sana wakuu.duh,thanks
 
Cecy alikua lanne b niko a,mtoto kanizimia kashindwa kusema akavumilia we wapi
Siku moja washkaji kama wanne hivi wananifata twende B kuna ishu kufika nakuta kundi la wanafunzi wamemzingira mtu....namwona binti wa watu kajiinamia analia wamemzunguka bado sijaelewa naskia "..ntakupa upige mpaka uchoke.." bado sijaelewa nashangaa...
Kumbe aliniandikia barua na hayo maneno ndani yake sasa wakati wa kuniletea ikibambwa wakaisoma
dah mtoto wa watu alikosa amani...
Sikujua kwamba nilikua HB mpaka baadaye kidogo
 
duh mzee ukumalizia kum-do kinguo nguo?
 
Tall vipi mbona unaguna? Isije kuwa mkeo anaitwa Flora na mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya msingi!!!!? Hahahahaha!


Ohooooooooooo!

Tall kuwa na amani ndugu yangu; haya yalitokea like twenty yrs back!😱hwell:🙄
 
hahaha, watu wana mambo ya ajabu kweli, unajua ndo maana wanasema wanadamu wanazaliwa wadhambi,watoto wadogo tu wanajua dhambi ni nini, hakuna anayewafundisha...kama ulikuwa unafanya hivyo, na sasa umeokoka, ingekuwa vyema basi....yani kazikwelikweli.
 
Miye mtu akitaka kuniudhi enzi zile aguse afro langu au akanyage raba zangu mtoni "Olympus" zilikuwa bab kubwa na hakuna mtu mwingine aliyekuwa nazo na afro lilikuwa kama kibanda...LOL!
 
.........Wanaume mna vituko kweli kweli, nimesoma maoni ya watu hapa hadi na mie nimekumbuka enzi hizo. Nakumbuka mwaka 1995 nilikuwa darasa la 4 basi mwenyewe ndio mtoto sijui lolote,kuna mkaka alikuwa anasoma darasa la 6, akaandika barua kwamba ananipenda na kumpa rafiki yake aniletee. Ndani ya hiyo barua alikuwa kaweka Tsh. 100 ya noti ya enzi hizo.........basi mimi nilisoma hiyo barua na kukuta mwenyewe kachora ua na kusema kwamba ananipenda. Ila mimi kwenye akili yangu wala sikuwa na uelewa nini haswa anamaanisha, basi baada ya kuisoma ile barua nikaamua kwenda kumpa mama yangu.

Mama akaanza kuniuliza ni nani kakupa hii barua? Nikamjibu kuna mtu nasoma naye ndiye aliyonipa hiyo barua kule shuleni...........basi kesho yake asubuhi mama akanipeleka shuleni hadi kwa mkuu wa shule na kumuita yule kijana aliyetumwa kunipa barua ili amtaje ni nani aliyompa barua ili aniletee. Yule kijana akamtaja jina huyo mkaka aliyekuwa darasa la 6 kwamba ndiyo aliyompa barua. Yule kijana alikuwa akiitwa Nelly alichapwa bakora 6 kutoka kwa mkuu wa shule.
 

Duh kumbe wewe bado ni kinda hivyo....
 
.........Nyani bana sasa toka mwaka 1995 hadi leo ni miaka mingapi imepita hadi uniite kinda........Mie sasa mtu mzima bana lol.

Loh...basi labda mimi ndo babu kizee....maana mwaka 95 nilikuwa sophomore....oh shiiit I just gave my age
 
mnakumbuka raha za kuandikiana barua enzi za mwalimu? nani ana kumbukumbu hizo
 
mnakumbuka raha za kuandikiana barua enzi za mwalimu? nani ana kumbukumbu hizo

yaangu inaanza


Mtitu Shule ya msingi
Sanduku la Barua 280
Iringa

Kwa Flora

Mimi nataka uwe kidenishi changu na nitakupa peni madaftari na hata ela ya kwendea shule halafu kesho uje uchukue majalada ya kichina kama lile niliokupatiaga jana dalasani. Yako mengi tu.

Nimempa Phoibe madaftali mawili akuletee kama zawadi. Chana balua hii ukishaisoma na majibu umpe phoibe lakini iwe sili yetu!

Akupendaye

Danieli
 
unaambiwa kwa mara ya kwanza siku ile nilienda winga (kusimamisha) mpaka nilipofika home ikabidi nikae kidogo nje mpaka mashine ilipopoa (kama nusu saa hivi) ndio nikaingia home maana kikaptula chote kilikuwa kimepelekwa mbele

Yeah, I can Imagine! Ukizingatia siku hizo underwear chache, ukibahatika unavaa zile VIP.....kazi kweli kweli!
 
Naona wengi mnaenda anga za mapenzi.Hakuna kumbukumbu nyingine?
Mie nakumbuka nilivyokuwa naiba migagi na wenzangu kwenye shamba la shule.
 
duh! hyo ilikuwa kali nimecheka mpaka basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…