Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,259
Leo nilikuwa benki nikimwekea ada ya mwanangu wa kwanza, anayesoma darasa la pili shule fulani ya kimataifa Dar. Nikiwa ninahangaika na mstari mrefu wa benki nikafikiria mambo mengi niliyokumbana nayo nikiwa primary, wakati elimu ya primary ya enzi zile ikiishiaishia ile miaka ya themaninini mwishoni (Nimemaliza primary 1992).
Hatukuhitaji kusoma international schools. Tulikuwa tunasoma na watoto wa mawaziri na yule kapuku wa kwanza mtaani. Tulikuwa tunasoma umbali zaidi ya kilometa 15, na wala hatukukosa kuchelewa namba au kufika darasani.
Nakumbuka enzi zile tulipokuwa tunapewa madaftari kila yakijaa. Ulikuwa unapeleka daftari lilojaa kwa mwalimu, naye atalichana kidogo ili lisitumike tena na pia usidanganye, halafu unapewa daftari jingine jipya papo hapo. Walimu hawakuwa wezi hata kufikiria kwenda kuyauza stationery. Wengine walibahatika kupewa hata mikebe.
Nakumbuka shule tulipokuwa tunakimbia mchakamchaka saa kumi na moja asubuhi halafu ukitoka hapo kuna gwaride. Walimu wetu wote walipitia JKT. Tukawa smart kiafya na kiakili pia. Mtaingia darasani na kusoma hadithi za akina Manenge na Mandawa, Heri mimi sijasema, Wagagagigikoko, na vingine kibao.
Vitabu vilikuwa vingi kiasi na kila mtu angeweza akawa na nakala mbilimbili za kitabu kimoja. Miandiko yetu ilikuwa mizuri, maana tulikuwa tunashindanishwa na pia kutandikwa viboko ukiandika kama bata. Kweli ilikuwa Someni kwa Furaha.
Ukihitimu LY shule inakuwa imejaa kichwani, ila sekondari zilikuwa chache, hivyo wengi wetu hatukupata nafasi za kuendelea kusoma japo tulikuwa wazuri. Kuna shule yoyote uliyosoma ambayo bado yakukumbusha mazuri kama sisi tuliosoma enzi zile primary?