Enzi zetu primary | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enzi zetu primary

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Ozzie, Aug 16, 2011.

 1. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Leo nilikuwa benki nikimwekea ada ya mwanangu wa kwanza, anayesoma darasa la pili shule fulani ya kimataifa Dar. Nikiwa ninahangaika na mstari mrefu wa benki nikafikiria mambo mengi niliyokumbana nayo nikiwa primary, wakati elimu ya primary ya enzi zile ikiishiaishia ile miaka ya themaninini mwishoni (Nimemaliza primary 1992).

  Hatukuhitaji kusoma international schools. Tulikuwa tunasoma na watoto wa mawaziri na yule kapuku wa kwanza mtaani. Tulikuwa tunasoma umbali zaidi ya kilometa 15, na wala hatukukosa kuchelewa namba au kufika darasani.

  Nakumbuka enzi zile tulipokuwa tunapewa madaftari kila yakijaa. Ulikuwa unapeleka daftari lilojaa kwa mwalimu, naye atalichana kidogo ili lisitumike tena na pia usidanganye, halafu unapewa daftari jingine jipya papo hapo. Walimu hawakuwa wezi hata kufikiria kwenda kuyauza stationery. Wengine walibahatika kupewa hata mikebe.

  Nakumbuka shule tulipokuwa tunakimbia mchakamchaka saa kumi na moja asubuhi halafu ukitoka hapo kuna gwaride. Walimu wetu wote walipitia JKT. Tukawa smart kiafya na kiakili pia. Mtaingia darasani na kusoma hadithi za akina Manenge na Mandawa, Heri mimi sijasema, Wagagagigikoko, na vingine kibao.

  Vitabu vilikuwa vingi kiasi na kila mtu angeweza akawa na nakala mbilimbili za kitabu kimoja. Miandiko yetu ilikuwa mizuri, maana tulikuwa tunashindanishwa na pia kutandikwa viboko ukiandika kama bata. Kweli ilikuwa Someni kwa Furaha.

  Ukihitimu LY shule inakuwa imejaa kichwani, ila sekondari zilikuwa chache, hivyo wengi wetu hatukupata nafasi za kuendelea kusoma japo tulikuwa wazuri. Kuna shule yoyote uliyosoma ambayo bado yakukumbusha mazuri kama sisi tuliosoma enzi zile primary?
   
 2. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nilisoma shule ya msingi mpechi, wilaya ya njombe, nakumbuka kwanza marafiki zangu Vinga, Sevanu na Royda na wengineo sijui leo hii wako wapi. nakumbuka tulivyokuwa tunashindana kusoma ili ufaulu uwe wa kwanza siku mnafunga shule wazazi wakija unaona fahari matokeo ya mtihani yakisomwa mbele ya wazazi wa kwanza mpaka aliyefunga mkia.

  Nakumbuka tulivyokuwa tunaenda Njosi ( njombe secondary) kuokota mavi ya ng'ombe kwa ajili ya mbolea tuliotumwa shule,

  Nakumbuka somo la sanaa na sayansi Kimu tulivyokuwa tunafanya kwa vitendo, i.e kupika, kuchonga, kusuka, usafi wa mwili na jinsi tulivyokuwa tunakaguliwa mpaka chupi.

  Nakumbuka mwaka ukianza mnapewa madaftari 12, rula ndefu pamoja na mkebe. nakumbuka Njombe ilivyokuwa na matunda ya aina mbalimbali na jinsi tulivyokuwa tunafaidi.

  Baada ya kuhamia Wilolesi primary - Iringa mjini namkumbuka mwalimu wetu mkuu mwalimu Kajiba alivyokuwa 'smart' Gwaride kila Jumatatu au Alhamisi; Nakumbuka jinsi shule ilivyokuwa na sifa ya kuponda kokoto lakini pia wanafunzi walikuwa na sifa ya kufanya vizuri katika masomo yao; Nakumbuka pia miti miwili ya mitoo tulikuwa tunaogopa kula matunda yake tukisema kuwa kwenye hiyo miti kulikuwa na majini.

  ( shule ilikuwa na sifa ya kuwa na majini na kwamba kila mwaka lazima mwanafunzi afe); Pia namkumbuka mwalimu wangu wa darasa Mwalimu matola kwa kupenda kuchapa viboko vya mgongoni lakini alikuwa mwalimu mzuri asiyependa wanafunzi wavivu alikuwa anahakikisha kila mtu lazima afanye vizuri kwenye somo lake la sayansi na hesabu bila hivyo jiandae kwa mboko, pushapu na kutembelea magoti. kwa ujumla walimu wetu wa shule ya msingi enzi hizo walikuwa wachapa kazi na hodari.

  Nakumbuka pia mchezo wa rede, uki, kiboleni, mdako, kuruka kamba, kombolela, kujipikilisha kibabababa na kimamamama tehe tehe....

  na baadhi ya nyimbo tulizokuwa tunaziimba kwenye michezo yetu kama
  kibunzi kibunzi; cha mememe; mwanambuzi kajamba kamjambia mkewe.......................

  Ukuti ukuti ...............................
  asiyependa shule ni mjinga kabisa; baarua ikija aitembezwa kote...............................
  nilikwenda kwa dada; nikamkuta shemeji anadishi ugali; nikadishi kidogo fungulia rekodi tukacheza kidogo...........................

  Halafu ikifika jumamosi saa nane kusikiliza mama na mwana na hadithi zake tamu tamu kama ua jekundu, unyoya wa kipanga azizi, binti chura, adili na nduguze, n.k wa kadhaa.
   
 3. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Yote hayo mloyasema hapo juu mengi yake yalifanyika wakati nikiwa shule ya msingi.

  Nilisoma Lusilile s/m (KKU-Manyoni)...na nawakumbuka waalimu wafuatao Mwl. Ghuliku (teacher big), Mwl. Kitundu, Mwl. Medaa pamoja na wengine wengi. Shule ilikuwa powa kinoma na masomo yalikuwa bam-bam, enzi zile unakuta Tarafa nzima wanafaulu wanafunzi 3 au 4 tu na wengi wao wanakwenda shule za ukweli.

  Nilipenda sana mpira na shule zote jirani zinazotuzunguka walikuwa wakipigwa bao si mchezo! shule kama; Kintinku, Ngaiti, Kitalalo nk nk. Siku moja kwaajili ya kupenda mpira mie na rafiki yangu mmoja tuliiba muhuri wa teacher big tukaandika barua kwenda shule jirani kuomba friend match. Looo ilikuwa balaa tulikula fimbo sita sita mbele ya wanafunzi wote, kwahakika hii siwezi kuisahau na Mwl. Kitundu ndo alituadhibu (sijui yuko wapi cku hizi).

  Kila mara nipitapo toka Mwanza kwenda Dar niionapo shule hii nakumbuka mbaali sana, kwani ipo barabarani kabisa utokapo Manyoni kwenda Dar mara tu umalizapo mlima saranda.

  Watoto enzi hizo hawakupelekwa shule za msingi za kulipia kama sasa, and still the pupils were very very bright!

  Hii imenikumbusha mbaali sana.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  those were good pld days,..primary school,class of 1993,...makurumla primary school,..mpo??
   
 5. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Saaafi saaaana!!!! Miaka gani hiyo???
   
 6. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Mambo mliyoyayaleza sio ya 1990's labda kama mlisomea vijijini sana..................................................
   
 7. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi enzi nasoma pale Mhovu ilikuwa ni sifa kubwa sana kwa sisi wavulana kutandikwa bakora kibao kwenye masaburi pasipo hata kulalama wala kushika, ukishika wenzio wanakuona we legelege kama hii serikali ya sasa.
   
 8. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe! Hayo mambo ni ya kupewa madaftari baada ya mengine kwisha nadhani yaliishia mwanzoni mwa miaka ya 80. Hata hivyo ni kumbu kumbu nzuri.
  Nilisoma Shule ya msingi Hasanga - Uyole Mbeya, the first product ya shule mwaka 1981. Kulikuwa na bwana akiitwa Divioni(RIP) huyu bwana alikuwa anaziweza hasa mbio fupi (mita 100-800). fanya ufanyalo lazima awe wa kwanza, mpaka watoto mitaani wakiwa wakimbia utasikia divioooni divioooni!!!
  walimu wa enzi hizo, Mwasembe, mama Komba, Kyamba, Mlimba, Lwila (baadaye ali-upgrade akawa mwalimu wa Mbeya day), Lazarous. those were really good days.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Dah! Ozzie Ubarikiwe sana, nikiwa primary nilikuwa mtundu wa ajabu sana! lkn home mzee alikuwa mkali sana tena sana so nilikuwa nikifika home heshima mbele! Paler jangwani pr School std one mpaka std 3, ilikuwa noma tupu, nilianza kutongoza enzi hizo huwezi amini na kuna mshkaji tulikuwa naye darasa moja sasa hivi ni mwanajeshi kikazi yuko zenji lkn kwa mienzi minne saa wapo sauzi kwa training, huyu jamaa ni balaa akinipigia simu huwa nacheka tuu, nikikumbuka jinsi tulivyokuwa wazuri wa kuandika barua za kutongoza totoz fikiria mdau std one two three tunatongoza. kuna siku nilishawahi chapwa na mwl alikuta nimesahau barua ya mchuchu kwenye daftari nililokusanya ili lisahihishwe, mbaya zaidi jina la mwl na yule denti yalikuwa yanafanana! kikaratasi kimepambwa na maua mazuri ya kuchora! ticha si akajua yeye aisee nilichezea fimbo mbayaaaa mnooo
   
 10. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />

  Mkuu mimi nimesoma s/m Mrokora huko moshi vijijini miaka ya tisini, nakumbuka mwanzoni mwa miaka hiyo tulikuwa tunapewa madaftari shuleni. Ni kumbukumbu nzuri sana nikikumbuka. Haswa namkumbuka mwl wetu wa hesabu Mshanga, huyu bwana alikuwa very smart ila tatizo lilikuwa pombe na sigara. Darasani tulikuwa tunachanga hela ili kumnunulia sigara. Alikuwa anaziita chai, akiona mmekaa muda mrefu hamjamnunulia anakuja darasani anasema siku hizi hamnipendi tena ndio maana hata hamnipi chai!!!!anafundisha vizuri kweli.

  Enzi hizo mwalimu mkuu Malamsha akitaka kukuchapa alikuwa na style yake inaitwa 'kamata masikio' yaani unajikunja fimbo zinaingia kweli, duh. ila pamoja na hayo yote tuliweza kufaulu tofauti na siku hizi ambapo watoto hata hawachapwi ila kufaulu bado tatizo!!!
   
 11. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi nimesoma Unyankhanya pr Singida vijijini,product ya kwanza ilikuwanicc,mwl mkuu.Jumbani alikuwa anaiita shule ya Mnyampaa maana yy alikuwa kidogo kazeeka.

  Shule ilikuwa mpya na tulikuwa tunafanya kazi na nje sana kusafisha viwanja vya shule n.k.
  Mpaka tunafika darasa la 4 tulikuwa na waalimu 3,wawili ni walevi wa kutupa.
  Tuliishangaza Wilaya yetu kwa kuwa wanafunzi 3 tuliongoza mtihani wa wilaya ,yaani ilikuwa ni raha maana ndio tunajitambua tupo shule na wazee vichwa vikubwa kwelikweli.
  Baadaye tukaanza kupata lunch shuleni.
  Ilikuwa raha kweli yaani tulikuwa tunakusanyana marafiki kula ,lakini sijui washkaji zangu wana hali gani sasa maana shule zetu ndio hizo ziliwapoteza ingawa walipoteza miaka yao 4.
   
 12. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  shule ya vidudu hahaha maana enzi hizo tunaita tu shule ya vidudu sio chekechea hivi sisi tulikuwa wadudu!!! 81-84 njombe kanisa la kiluteri - nakumbuka uji mtamu tuliokuwa tunakunywa shule na zile pipi tulizokuwa tunapewa zenye (ziko kama mpira) maumbo mbali mbali ya wanyama na ule udongo wenyewe tulikuwa tunaita udongo ulaya una rangi mbalimbali tulikuwa tunautumia kutengeneza vitu mbalimbali. ikifika saa tano baada ya uji michezo mbalimbali mpaka saa sita, tunakaa mstarini walimu wanatutangazia ya kututangazia halafu wimbo ............sasa sasa saaa ya kwenda kwetu ---------- kwa heri mwlimu kwa heri tutaonana kesho!

  mwaka 85 ndo la 1 Mpechi. sikumbuki Wimbo wa shule ila kama nakumbuka vinyimbo nyimbo vilivyokuwa tunaimba darasa la kwanza mpka la tatu kama: Shule yetu ni nzuri imepambwa maua; ukienda hovyo hovyo utayumba yumba wee. au na ule wimbo wa bibi tarabushi kofia nyekundu tarabushi inanipendeza mama..........................

  Ila siyo siri Tangu nihame iringa kwa ujumla nimemisi sana yale matunda ya ufudu, misaula, mikusu, maembe sindano tuliyokuwa tunakula mabishi kwa chunvi na pilipili, mitoo, peach, peas, mifurusadi, madansi, matopetope, mazambarau (mawenge), matunda damu, apple, midaa tulikuwa tunatumia sana kusukutulia meno yetu ulimi unakuwa mwekundu meno yanakuwa meupe, songwe, zabibu pori, makomamanga, n.k. kwa aujumla hayo ni matunda ambayo unakuta sehemu nyingine huwezi kuyapata na kama hujawahi kuyaona huwezi kuyajua kabisa ila watu wa Iringa, Njombe wanayajua sijui ka bado yapo kama uharibifu wa mazingira haujaingilia kati..

  Hayo matunda kwa ujumla ukiyaona kwenye supamaketi bei yake ni aghali mno. siyo raisi kuyanunua mara kwa mara na hata Tanzania hayapo sehemu zote ndio maana nasema nimeyamisi.
   
 13. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2013
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  nakumbuka Azimio Primary school katikati ya mji wa Mbeya. Nilikuwa naishi Jacaranda na hapo shule classic by then ilikuwa Azimio na Sisimba(ukiondoa Umoja ambayo ni Private)
  Nikianza la kwanza na la pili mwl mkuu alikuwa Msomba then akajahanishiwa Mbata primary tukaletewa Rwegoshora.
  The most memorable events ilikuwa ni kwenda mto Mbeya day kuchota maji ya kumwagilia maua. hapo kuna wengine walikuwa wanapiga mechi huko huko kwenye vichaka vya mianzi.
  hapo tulikuwa na upinzani wa jadi wa kimasomo na Sisimba na Mbata. usiombe siku hiyo (jmosi) mkafaulisha watu wachache kwenye mitihani ya ujirani mwema zitakavyowaka fimbo za mlingoti, yaani eneo zima linanuka milingoti iliyochanika. hapo safu nzima ya walimu ni Rwegoshara mwenyewe, Samata, Mfugale, Mayeye, Nzyungula na wengine.
  Hapo wanafunzi wote mnasoma mkishindana ili muende shule kali kama Mzumbe, Ifunda Tech, Iyunga na nyingine na hapo ukishindwa saana basi ndio Mbeya Day.
  Those were the days when education was really education na watu walikuwa wanatoka competent hata waliokosa nafasi za Sekondari.
   
Loading...