School Reg.No calling= S.135Me niliambiwa nenda bweni(jina kapuni) ukwamuulizie jamaa anaitwa Bunsen burner!!! LOH! Nilipofika hapo bwenini jamaa wanistukia kuwa
nimeingizwa mkenge nao wakanambia ametoka nimsubiri kama dakika sita hivi atarudi!! ndugu niliuza chai mpaka nikakoma, baadae ndo
wakanielewesha.. nilimind we acha tu.
Nakumbuka ndani ya Old Moshi, miaka ya 1996 kulikua na dogo mmoja hivi kwao mambo safi alikua akija anajipigilia sana sukari, blueband, kitunguu swaumu kilichokaangiwa mafuta ya mgando, e.t.c.
Na hakupenda kufanya hisani kwa wengine.
Siku moja dogo baada ya kuchukua Uji akautia Blueband na Sukari kama kawaida yake, sema sasa siku hiyo Uji ulichelewa kugaiwa hivyo mpaka kengele inagongwa hakua ameumaliza kwani Ulikua wa moto.
Basi njemba mmoja ikamuomba dogo iumalizie lakini dogo akakomaa kua anauhifadhi ataunywa baadae. Kweli dogo akafungua Tranka lake na kuuweka humo bila kuufunika kisha akaenda class.
Ile njemba ikaliinua tranka na kuligeuza geuza kwa nguvu, binua binua juu chini, chini juu, ikafanya kama inalichekecha tranka uji ukiwa ndani haujafunikwa kisha ikalirudishia tranka vile vile.
Kilichofuata baada ya dogo kuurudia uji wake baadae ni.........
Nakumbuka kuna mlinzi aliwahi ona bundi akajua simba basi akaja kutangaza kua kuna simba alikua ni mmasai .Mimi nilikua napenda kutoroka kwenda kijijini na washkaji siku moja niliwauliza wana zengo kua huku kuna simba wakasema ni bundi wakubwa tu.Basi ulipita kama mwezi siku moja nilikua natoka prepo ile mida ya saa za wasongo kama saa nane usiku hivi nilikua nakimbia kwa korido kuna jamaa akatokea mbele yangu alikua anaenda kunawa uso ili akasome akaniuliza unakimbia nini?Nikajibu simba!Aisee yule jamaa alitupa maji na kukimbilia domitory na kuanza kulia simbaaaaaaa!Shule nzima ilikimbizana yule mlinzi ndio usiseme!Basi madom yetu yalikua na kenchi yaani watu walininginia kama popo ili simba aiwangate!Kuja kuja kama wameuzwa walikua wame umia vibaya aisee members wa mkandawile mpo hapa???
Daaa loleza galz balaaa yan hasa kun shmu inaitw golgota ww ukiitw apo ni balaaaaa
Dah nimefurahi sana kuona nawe mkuu Mentor ni alumn wa Old Moshi...Old is Gold, Mawenzi, Hanang, Meru, Shengena and Kibo Forever!!!!!
Miaka hiyo ya 1994 Kolila Secondary unapandishia pale kiboriloni, Moshi kulikuaga na Ticha mmoja hivi wa Nidham akiitwaga Komba. Huyu ticha alikua mkali na mchapaji mno mno mno!!!
Sasa kwa kua Kolila ipo milamani, basi ukitaka kuja town tunaita ku-drop. Ikatokea siku moja jamaa mmoja aka drop kwa kutoroka ilikua siku ya jumanne ili kuja kiboriloni kusaula mitumba maana ndio siku ya kufungua mabeli ya mitumba.
Basi ile kurudi yuko nje ya ukuta wa shule anataka arukie ndani kumbe Mr. Komba nae yuko upande wa ndani wa ukuta huo huo sehemu hiyo hiyo.
Jamaa akarusha kwanza begi lake lenye nguo ndani na bahati nzuri au mbaya Mr. Komba nae kwa ndani akashtukia begi linarushwa kutokea nje akalidaka. Jamaa wa nje ile anapanda ukuta kichungulia anakuta begi lake limedakwa na Komba, na fimbo zake zinajulikana shule nzima.
Ikabidi jamaa asamehe tu lile begi na nguo ale kona tu mpaka night Kali. Komba nae kaja assembly kaanza kuulizia nani mwenye begi karibia siku 3 na asitokee. Mwisho wa siku akaamua kuwapa Shamba boy wake pamoja na vibarua wa shule viwalo vya jamaa.
Jamaa yetu nae alikua akinunua kiboriloni anakuja kutuuzia bwenini kisirisiri hivyo pocket money yake ndio alikua akiizungushia mtaji na ndio imekata. Ikabaki kila akiona shamba boy kavaa nguo yake ye anabaki kututajia bei tu huku anasikitika, na kuwanyang'anya hawezi maana Mr. Komba akimjua tu shule hana!!
Mi nlipo kuwa form two bana nliiba sufiria la diet ya wagonjwa wakati umeme umelatika, ile natoka Tu jikoni umeme ukawaka kumbe m/ kiti WA bwalo alikuwa karibu, akaniamuru niweke sufuria la Moto kichwani mwisho akaona haitoshi akaamua nipewe adhabu ya kuosha madishi ya shule nzima kwa muda WA mwezi mzima kitu ambacho kwangu ilikuwa neema kwani nlikula top layer kila cku mpaka nkanawiri na cku ya nyama mi naonsoka na dishi lote, we acha bana
Nakumbuka ndani ya Old Moshi, miaka ya 1996 kulikua na dogo mmoja hivi kwao mambo safi alikua akija anajipigilia sana sukari, blueband, kitunguu swaumu kilichokaangiwa mafuta ya mgando, e.t.c.
Na hakupenda kufanya hisani kwa wengine.
Siku moja dogo baada ya kuchukua Uji akautia Blueband na Sukari kama kawaida yake, sema sasa siku hiyo Uji ulichelewa kugaiwa hivyo mpaka kengele inagongwa hakua ameumaliza kwani Ulikua wa moto.
Basi njemba mmoja ikamuomba dogo iumalizie lakini dogo akakomaa kua anauhifadhi ataunywa baadae. Kweli dogo akafungua Tranka lake na kuuweka humo bila kuufunika kisha akaenda class.
Ile njemba ikaliinua tranka na kuligeuza geuza kwa nguvu, binua binua juu chini, chini juu, ikafanya kama inalichekecha tranka uji ukiwa ndani haujafunikwa kisha ikalirudishia tranka vile vile.
Kilichofuata baada ya dogo kuurudia uji wake baadae ni.........
shy bush kwa mzee "PRUDENCE" aka PURU nliwahi kupgwa zadhabu ya kufyeka uwanja, kipimo sasa.......jamaa alishika manati na kajiwe af akarusha tu pale jiwe lilipotulia ndo jamaa akanambia "ishia pale" nilichoka mwili na roho