Enzi ulipokuwa boarding

Enzi ulipokuwa boarding

Nakumbuka kuna mlinzi aliwahi ona bundi akajua simba basi akaja kutangaza kua kuna simba alikua ni mmasai .Mimi nilikua napenda kutoroka kwenda kijijini na washkaji siku moja niliwauliza wana zengo kua huku kuna simba wakasema ni bundi wakubwa tu.Basi ulipita kama mwezi siku moja nilikua natoka prepo ile mida ya saa za wasongo kama saa nane usiku hivi nilikua nakimbia kwa korido kuna jamaa akatokea mbele yangu alikua anaenda kunawa uso ili akasome akaniuliza unakimbia nini?Nikajibu simba!Aisee yule jamaa alitupa maji na kukimbilia domitory na kuanza kulia simbaaaaaaa!Shule nzima ilikimbizana yule mlinzi ndio usiseme!Basi madom yetu yalikua na kenchi yaani watu walinin‘ginia kama popo ili simba aiwan‘gate!Kuja kuja kama wameuzwa walikua wame umia vibaya aisee members wa mkandawile mpo hapa???
Yaani nimejaribu kuvuta picha ya hili tukio nimecheka mpaka mbavu zinauma!!!
 
Kwa wale waliosoma tanga tech kwa kamanda TETI the headmaster,mi nilisoma advance pale nikiishi bweni la TWIGA.Nakumbuka zile siku za wali a.k.a punje a.k.a chakula cha binadamu tulikuwa tunajiandaa kama unakwenda vitani,unapiga raba,jeans na t-shirt then unajipanga kwa foleni.Mgawaji anapokugawia,huangalii sahani,unamuangalia usoni kwa jazba yaani shari tupu.

Hii hiii, eti haungalii usoni umenifurahisha
 
Nakumbukuka niko sec Siha ,siku moja jioni kuna jamaa kutoka kigoma alienda kujisadia ,na alikuwa na Ada kwenye walet ghafla ikadondoka chooni,alikuwa form 6,akaanza kutindua choo kwa pembeni, akaingia na kuitoa ada ,bahati nzuri kulikuwa na vyoo vya kulenga set mbili.alinyoa nywele zote mpaka kwenye kope,he had a strange personality.

Heee heee this is real strange
 
siku moja tosamaganga tuko bwaloni kaja jamaa mmoja fm4 amechelewa msosi ameukosa basi kaja kwenye meza yetu kachukua msosi wangu kaweka kwenye sahani yake then kasepa mi kumfuatilia kanizaba kibao. nlilala na njaa siku ile hata sisahau
 
siku moja tosamaganga tuko bwaloni kaja jamaa mmoja fm4 amechelewa msosi ameukosa basi kaja kwenye meza yetu kachukua msosi wangu kaweka kwenye sahani yake then kasepa mi kumfuatilia kanizaba kibao. nlilala na njaa siku ile hata sisahau

Ulikuwa form gani na wewe??
 
Enz hzo nikiwa 4m one ile naenda xul boarding nkawakuta 4m 4,yan hakuna kuingia dom bila kuimba wmbo wwt ukigoma night unachezea belt za kutosha 2
 
Nipo form1, 1998 jamaa wa form3 akanipa Tsh100 akanituma nikanunue vitu vyenye thamani ya Tsh5000 na nisiponunua labda niache shule maana mateso yake sio ya kitoto...hapo nimebakiwa na pocket money 1000, dah nyie acheni2!
 
hahahaaaaaa jaman hadi machoz yanantoka. hii post kwa kweli nataman nprint kabsa ili ikae kama kumbukumbu maana ni stress free, hahaaaaaaa dah, mwalimu BUGA nouma sana
 
Umenikumbusha vyoo vya nje maarufu kama Half Mile, hivyo vyoo vipo umbali wa zaidi ya mita mia mbili. Kufanyiwa usafi kwake ni mpaka mwanafunzi akamatwe na kosa ndio akafanye usafi, sasa pata picha ya harufu ya mchanganyiko wa maharage yasiyo na viungo + bondo jeusi harufu ikoje...

Wale Alumna wa Tosamaganga High School watakumbuka ile staili tuliyokuwa tunatumia kwenda kulenga shabaha pindi ikitokea maji yamekatika kwenye vyoo vya ndani vya kuvuta.
Unavua shati na suruali mbali unabakiza bukta au chupi tu ndiyo unaingia Half mile vinginevyo ukirudi darasani watu watakukimbia kwa harufu.
 
ahahahahah....enzi hizo Tabora boyz..kulikuwa na chemba moja katika bweni la mkwawa inaitwa university..mle tulikuwa tunalala pipo kama kumi na moja hivi tukiwemo viongozi..mke wa headmasta jina la utan nyumelo alikuwa na tabia ya kuja kutuamsha asubuh na mapema mabwenini..siku hiyo kaja kakuta pipo zote zimelala naked chemban coz tulipanga tumkomoe...ahahah yule mama eti akasema wala hatishiki coz keshaona kubwa zaidi ya zetu..mwee..but atleast alipunguza kuja akawa anaishia bweni kuu...vituko vya mesini hasa siku za nyali aka ubwabwa we acha tu..

Huyo mkewe wa H/M naye alikuwa mwalimu au ndiyo yale ya mke wa Rais naye kupewa msafara na ving'ora...
 
NJOSS ilikuwa boys tu, siku ya Disco form one wote mnavalishwa mashuka kama kanga na kuwekewa vitambaa kifuani halafu unavaa shati, vitambaa viweka umbo la matiti mnaitwa wasichana ili jamaa wawe wancheza na kuwashika matiti bandia DHAMBI LAKINI maisha ya boding we acha tu
 
Enzi hizo lubala sec duh jamaa ananambia nilipe ela ya ktanda nkaona maixha magumu kpnd hcho
 
daah Karaseco siku yakusoma matokeo ya muhula aka BASHUKA ilikua nauma yaani wanasoma mpaka kumi mti mzima hautokei mbele ya ata madogo wanacheka île mbaya daah 5-6 2003
 
Mwaka 1998, tupo Same boys, kuna mshkaji alikuwa mgeni school. Sasa aliomba tochi usiku kwenda toilet za kulenga mbali na madarasa. Ile mshkaji anainama tu, wakaja fisi wawili mlangoni! Jamaa si akatoka nduki mpaka class . Tukamuuluza kulikoni? Jamaa huku akihema sana akasema eti kaona mbwa wa ajabu wenye miguu mirefu ya mbele na mifupi ya nyuma. Duu jamaa tukamwambia hao ni fisi na sio mbwa, jamaa hakuamini kama alipona!!
 
Haisee umenikumbusha mbali,kitu half mile enzi za H/master Charwe.
Nidhamu mzee Soldier.
Nakumbuka fm 2 walim-time Kahamsini na kumnyang'anya list ya wapiga kelele kwenye stairs!
Live long Tosa
Umenikumbusha vyoo vya nje maarufu kama Half Mile, hivyo vyoo vipo umbali wa zaidi ya mita mia mbili. Kufanyiwa usafi kwake ni mpaka mwanafunzi akamatwe na kosa ndio akafanye usafi, sasa pata picha ya harufu ya mchanganyiko wa maharage yasiyo na viungo + bondo jeusi harufu ikoje...

Wale Alumna wa Tosamaganga High School watakumbuka ile staili tuliyokuwa tunatumia kwenda kulenga shabaha pindi ikitokea maji yamekatika kwenye vyoo vya ndani vya kuvuta.
Unavua shati na suruali mbali unabakiza bukta au chupi tu ndiyo unaingia Half mile vinginevyo ukirudi darasani watu watakukimbia kwa harufu.
 
Sijapata kuona headmaster kma charwe, hakika wanafunzi tulimpenda sana ila PIA MUNGU na yy alimpenda

Alidirik sitasahau alivyozima issue ya muslim na wakristo mpka leo jamaa wakawa ndugu pale tosa sec
 
Inaonyesha nijinsi gani wa Tz tulikuwa namambo uniform... Ona hapa tunapiga story zinafanana ata mkikutana univasity mnakuwa mmesoma mtaala uleule .....uliza saizi mambo yalivyo. Nakumbuka enz zile boarding siku ya Nyama, wali, samaki au kande afu jamaa flani waamue kuiba dish lenu ....afu mkitafuta mnakuta limetupwa sehemu. Kwanza sikuiyo viwanja vyote vinajaa kila mtu eti yupo busy anatafuta apetite
 
nilikuwa tanga school(tanga tech) baina ya 1991-1994, nakumbuka nlipenda kupiga tizi lakini siku za punje(ubwabwa) nlizidisha dozi ya tizi ili kutengezza nafasi kwa ajili ya punje kuingia tumboni kwa wingi lakini siku za zege aaaaaarrrrgggg, ilikuwa bora liende.

nlikuwa na demu wangu KO, basi siku karibu na disco, nlikuwa napiga sana chuma pale nyati ili nitanue kifua niweze kubambia vizuri....

ni full vitukoo, boarding enzi hizo....

huwa najiuliza hivi hawa wenetu, dotcom, watawapa stori gani watoto wao?
 
nakumbuka Mazengo enzi hizo,tulikuwa tunapata uji saa kumi na moja afajiri.ilikuwa kengele ikigonga tu ukichelewa kidogo tu imekula kwako.Basi bwana kuna jamaa alikuwa analala kwenye deka juu mimi chini,siku moja kengele ya uji imelia tu mimi nikachomoka fasta kitandani,kumbe na jamaa juu alikuwa tayari amesharuka kutua chini,kilichotokea hapo sitasahau maana ilikuwa bonge la collision.daaah uji ulikuwa unaitwa "Nyuka"
 
Back
Top Bottom