Enzi hizo bana...

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,211
113,520
Enzi za ma Ikarusi kumbakumba...

Enzi hizo za Bahari beach hotel, Kunduchi beach hotel, Rungwe oceanic, Silversands hotel, Africana....daah those were the days.

Nilikuwa napenda sana kwenda Africana kwa sababu walikuwaga wanafuga wanyama pori pale kwa mbele upande wa kushoto kwenye entrance. Basi siku moja mi na mdingi tukaenda pale. Mdingi alikuwa na mkutano. Basi mimi nikaenda zangu kuwacheki wanyama. Palikuwa na kila aina ya wanyama lakini mimi nilikuwa fascinated sana na simba. Ilikuwa mida ya saa kumi na mbili jioni.

Out of nowhere yule simba dume akaunguruma bana....heheheheee ebana eeh....usiambiwe na mtu. Muungurumo wa simba dume kiboko. Manake ardhi ilirindima utadhani kulikuwa na tetemeko. Mimi sikujua kilichokuwa kinaendelea maana kama vile nilipoteza fahamu kiaina. Kwa kweli sitaisahau hiyo siku maana mpaka leo hii ile sauti bado naisikia.

Oooh halafu mnakumbuka enzi zile wageni wakiwatembelea kutoka bushi mnawapeleka uwanja wa ndege kwenda kutembea...lol.....man oh man...we have come a long way....pia mnawapeleka bandarini kwenda kuangalia meli. Mimi nilikuwa lazima nivalie suruali yangu ya mchele mchele tulipokuwa tukienda uwanja wa ndege. Nilikuwa natooooka mwenyewe...lazima nipendeze.

Enzi hizo tunaenda kuazima movie pale empire....mtaani ni watu wachache tu wenye vcr....basi jumapili lazima watoto wa jirani waje kuangalia movie....movie za kihindi...Disco Dancer...akina Mithun Chakraboty, Amitah Bachan, Govinda...Amjad Khan....

Duh enzi hizo bana.
 
dah kumbe wew mtoto wa kishua eennh??
hongera sana bwana


nimecheka ile mbaya lines zako manake ni mulemule sisi tulimpeleka anko ikulu kupiga picha alisimama km anaangalia wizara ya elimu then picha ikapigwa basi naskia alienda kuiweka sebleni apo peramiho basi kila atakayeingia lazima aonyeshwe ...unaona iyo???????apo dsm ikulu!!!!!
 
mtoto wa kishua? what the hell does that even mean? haven't heard it in ages....geeeeeeez
 
Ni kama ilivyo sasa mtoto wa mjini nadhani ...mtoto wa kileo wa , kisasa...Born town

Alaaaaa watu tumezaliwa Ocean Road bana....mji twaujua huu....lol...natania tu...uwe umezaliwa Kolandoto..Somanda....KCMC....hakuna tofauti yoyote
 
Mbona hii stori iko hapa??:thinking::confused3: Nilidhan hapa ni mapenzi tu.:doh:
 
nakumbuka beki tatu wetu tulienda kumpokea tazara pale wakati tunavuka mandela road aliniuliza swali moja la ajabu sana ..''kaka hivi hii barabara ndo inaelekea dar es salaamu eeh?''.ilibidi nimjibi NDIYO
 
nakumbuka beki tatu wetu tulienda kumpokea tazara pale wakati tunavuka mandela road aliniuliza swali moja la ajabu sana ..''kaka hivi hii barabara ndo inaelekea dar es salaamu eeh?''.ilibidi nimjibi NDIYO

teh teh nimecheka sana...
 
wewe africana ulikuwa unaenda tazama wanyama,sisi tulikuwa tunaenda usiku tu kuselebuka GOGO discoteque
 
Back
Top Bottom